Wakuu naona sheria ya mtandao ipo Facebook na Whatsapp tu lakini INSTAGRAM wamechemka!

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,097
10,998
Kwakweli baada ya hii sheria kuanza kuwabana watumiaji wa facebook na whasapp kwa wale wanaosambaza jumbe za uwongo na lugha chafu
Sasa vurugu zote zimeamia Instagram,kwakweli insta kwa sasa umekuwa ni mtandao ambao watu wanautumia vibaya,Ikiwemo picha na video za uchi,kutukanana matusi makubwa,insta now kumeibuka mashoga ambayo yanajitangaza hadharani kutaka wanaume wenzao mfano mzuri ni wa #jamesdelicious anayejitamba kumpokonya vanessa mdee jux
Watu wanatukanana mitusi mikubwa,picha za uchi now insta ndio mahali pake. Karibuni mchangie
 
Mkuu sheria ya mtandao inafanya kazi pale mkulu anapoguswa tu, huko Instagram wapo vichaa wanaopunguziana presha na wengine kuongezeana presha, wala hawahusiki na mambo ya siasa.
 
Instagram kule hakuna Siasa, kule ziko team zisizo na viwanja
team James delicious
Team Wema
Team mtoto wa mama
Team mtoto wa watu
 
WhatsApp kuna end to end encryption. No third party can read or listen to your conversations
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom