WAKUU naombeni Msaada wa Mawazo nifanyeje.

Ya bagamoyo no, nimeishi bagamoyo naifahamu hiyo Sober ni ya wajanja wachache wanaopata fedha za wafadhili/watalii wanaofika Katika huo mji, bagamoyo ni rahisi kupata hayo madude hamna msaada, Ushauri wangu kwanza Mtafutie Mtaalamu wa Saikolojia aweze kumtoa huko mana ameshakuwa addicted hii kazi hata daktari anaiweza kule bagamoyo awe anaenda kufata dawa tu mana hizi dawa ni gharama na asiwe mbali na wewe na awe anameza chini ya usimamizi wako, mara nyingi anapoanza kuachana na haya madude ndio anapoanza kusikia maumivu makali so jiandae mana unaweza muonea huruma, cha msingi awe tayari kukabiliana nayo akiweza ndani ya Mwezi mmoja tu kutokutumoa from now ni rahisi sasa kuacha na atakuwa maeshajitambua ila hii kitu sio nzuri hata kidogo, ni mbaya ikishaingia kwenye Damu na Ubongo
Duh aysee....asante sana mkuu kwa ushauri,
AF et kuna viongozi wa kubwa wanamlaumi Yule Rais wa kule wapi sijui anaewaua ma drug dealer, awaue tu aysee.
.namwombea kwa Mungu ambariiki!
 
Pole sana. ..mwambie mama yako asali na kutubu kwa Muumba wake. ..mtoto atapona. ..imani ya mama ina nguvu sana kwa mwanae....Mwenye Enzi Mungu akutangulie. .
 
Mnunulie tramado pia usisafiri nae kwanza. Kaanae hadi arosto ni masaa 75alafu muongezee tena masaa 75ili mwili uwe fresh asitumie dawa za usingizi kabisa!!
Msaada mkubwa sana Mkuu naomba nikufuate chemba...
 
Pole sana. ..mwambie mama yako asali na kutubu kwa Muumba wake. ..mtoto atapona. ..imani ya mama ina nguvu sana kwa mwanae....Mwenye Enzi Mungu akutangulie. .
Asanteni mkuu
 
Heroin,
Cocaine,
Crack,
Hallucinogen,
Amphetamines,
Marijuana,
Alcohol,
Inhalant,
Prescription drug.

Hapo juu ni aina za madawa za kulevya.

Kama ametumia Heroin sio mbaya kivile anaweza kupona kama atapata tiba nzuri.
ila cocaine ndio hatari sana.

( king pusha )
 
Kitu kingine Kumbuka katika vitu vyote unga ndio kali yao. Kama tayari anajua raha yake inaweza ikawa ngumu kuacha. Bali kama anaonyesha ushirikiano komaa nae kabla aijakolea ndugu yangu.
 
muombee visa ya Ufilipino umpeleke huko ndio dawa pekee Kwani hamna namna nyingine!
 
Kitu kingine Kumbuka katika vitu vyote unga ndio kali yao. Kama tayari anajua raha yake inaweza ikawa ngumu kuacha. Bali kama anaonyesha ushirikiano komaa nae kabla aijakolea ndugu yangu.
Huyu inaonyesha haijamkolea...maana toka jana,...Yupo pouwa nimempa tu zile tramado, leo.....naona anazngua et anahis maumivu, nimruhusu akanunua hata kimoja af akikate nusu...nimemwambia nitamuongeza dawa tu...nimejaribu kugoogle kweli tramado zipo pouwa, japo nazo mtu huweza kuwa addict
 
Mwambie aoge kila baada lisaa kama kuna mto karibu mwambie akae mtoni mda wote. Au kama yuko nyumbani na ni mambo safi kidogo bafu sio ya kusubiria mwambie atumie muda mwingi bafuni
 
Dawa yake ni maji kuoga na kunywa. Kuanza kula sembe ni kazi rahisi lakini kuacha ni vigumu sana. Unga mwisho duniani
 
Mwambie aoge kila baada lisaa kama kuna mto karibu mwambie akae mtoni mda wote. Au kama yuko nyumbani na ni mambo safi kidogo bafu sio ya kusubiria mwambie atumie muda mwingi bafuni
Dah hapa yenyewe nimemvurumisha akaoge...hayo usemayo ni tru mkuu, hata yeye wanakiri ndio dawa. Sema mwoga saana kuoga maji ya bariidi
 
Back
Top Bottom