WAKUU naombeni Msaada wa Mawazo nifanyeje.

Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Kwanza poleni na majumukumu, mwenzenu nina tatizo..tena tatzo kubwa ktk familia, ni juzi juzi tu nimekuwa zikisoma na kusikia habari za zinazozagaa flan anakula unga mara msanii Fulani kawa teja, sasa aysee hii kitu ishapiga hodi had kwenye familia yangu, na sio kupiga hod tu ...nashituka sasa tatzo ni kubwa.
Iko hiv mimi naishi Dar Ila mama yangu yupo mkoani kikazi, kule anakaa na mdogo wng ambaye nimekuwa nalalamikiwa kawa na tabia korofi, kwanza kabisa licha ya kuwa na matokeo mazuri kidato cha 6 kakataa kuendelea na chuo, akaanza sigara na pombe, mara wizi wa vitu vya ndani.

Nilijaribu kumleta Dar kwng, ili afanye taratibu za chuo, akatulia na kuonyesha ushirikiano Ila baada muda alibadilika na kutoroka kwenda kusikojulikana had alipotokea tena mkoani kwa mama miez sita baadae akiwa na tabia chafu zaidi mara mbili ya mwanzo.
Ikafikia hatua had mama kakonda kaisha kwa maumivu juu ya mtoto wake huyu wa mwisho. Ni mdogo kiumbo ila tabia sasa, anaiba vitu ndani, anashikia watu kisu, Mtaa mzima wanamgwaya..

Sasa hamad, mwezi huu nimekuwa kumtembelea mama, sabab moja wapo ikiwa pia kujua kulikoni huyu Dogo kawa hiv, ayseee siku amini...kumbe Dogo anakula poda, unga, heroin!! tena alikuwa anavutia had ndani...sio tena mtu wa zile sigaret au pombe au banhi kama wengi wanavyodhan hapa mtaaani..huyu Dogo anapiga teli, Uzuri wa bahati mimi ananijua kuwa sio mtu wa mchezo mchezo toka nifike akawa mpole nikamwita chini nikamuuliza nini kinachomsibu akanambia toka miez ilee akimbie kwangu alijiingiza kwenye utumiaji wa unga ndo matokeo yake hayo. Mwanzo sikutaka kuamin kama hata huku shamba kuna unga, Ila upo aysee... Nikamshauri aache mara moja, akasema sawa maana hata yeye anajuta..sasa wakuu matokeo yake ndani ya siku tatu tu dogo akakimbia nyumbani...hayupo! nikaanza msako chaka kwa chaka..chimbo kwa chimbo..nikatokezea kila sehemu ambapo huwa ananijua sawa zake..naambiwa huwa anatokea usiku anachukua kete 2 ( kipimo cha huo unga wao) kuonekana had kesho yake tena bas nikamuwekea mtego, Jana nimemkamata akawa mbishi nimepiga sana ngumi za shingo mpaka Kanyoka, nikafunga kamba mpaka mornii full kummwagia maji, asubuhi mwemyewe kaomba poo...kadai niondoke nae Dar maana huku hawez badilika, mimi unaogopa kujidhamini kwa Mteja japo mpaka sasa hajatumia chochote zaid dawa za maumivu na chakula..na maziwa..Ila mama nae ananililia niondoke nae tu nikamdhibiti na ampunguzie kero na aibu... mama yetu hajui chochote kuhusu unga, masikin yeye anahis Dogo anawenge au bangi tu imemchanganya , anaomba nifanyeje kila niwezalo maana anaamin huyu Dogo hunickiliza mie hasa kuliko mtu mwingne yeyote.

Naombeni ushauri ndugu zangu. Nifanyeje?? Au nitamsaidiaje huyu Dogo wngu na mama yangu ili walau maumivu yake yapungue.

Je, unaweza pata wapi dawa za kumfanya walau asijickie vibaya pasipo Kula unga..maana naamini hajawa Mteja saana kivilee.

Asanteni.
20170105_134001.jpg
 
kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,540
2,000
Pole sana mpeleke sober atapata msaada before is too late. Ila na yeye awe tayari kubadilika.akitoka huko kama atakubali kurudi shule arudi shule ila awe na kitu cha kum keep busy. Hao marafiki zake wote ambayo wenye tabia as kuvuta unga aachane nao. It won't be an easy road ila uwe nae bega kwa bega
 
Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Huyo Dawa Yake Ni Moja, Kaongee Na Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Au Bwana Jela Ili Awekwe Jela Kama Miaka 2 , Usimwonee Huruma Utampoteza - Akikaa Gereza Ambalo Halina Access Na Madawa Atapona.
Unafahamu mtu aliyekuwa addicted na haya makitu akiyakosa zaidi ya siku mbili anakuwaje? kinachofuatia ni kifo, Na atasumbua tu Wafungwa wenzie hili sio suluhisho.

Ampeleke tu sober, akaanze dozi.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,402

Unachosema Ni Sahihi, Ila Kuna Jamaa Nimewahi Kumsikia Akisimulia Alikuwa Anakula Sana Madawa, Siku Alivyokamatwa Na Polisi Akafungwa Miaka 2 Akatoka Amepona Na Kuacha Kabisa.

- Ila Alipata Shida Sana, Maana Alikuwa Anazimia Hata Siku Nzima Hajitambui ~ Kiasi Kwamba Kama Ni Mwanao Na Yuko Kwako Unaweza Hata Kumtafutia Kwa Kumwonea Huruma Tu.
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Huyo Dawa Yake Ni Moja, Kaongee Na Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Au Bwana Jela Ili Awekwe Jela Kama Miaka 2 , Usimwonee Huruma Utampoteza - Akikaa Gereza Ambalo Halina Access Na Madawa Atapona.
Asanteni mkuu kwa ushauri..mwanzo niliwaza hivyo ila nikawa naogopa tu asitoke huko ndo kaharibiwa kabsa na tabia nyingne...km ushoga!
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Pole sana mpeleke sober atapata msaada before is too late. Ila na yeye awe tayari kubadilika.akitoka huko kama atakubali kurudi shule arudi shule ila awe na kitu cha kum keep busy. Hao marafiki zake wote ambayo wenye tabia as kuvuta unga aachane nao. It won't be an easy road ila uwe nae bega kwa bega
Asante sana mkuu...ngoja nikifika Dar nitajaribu kufanya utafiti wa sober camp. ..ya bagamoyo, tatzo nawaza hiyo tabia yake ya alibadilika badilika, na je nikifika nae Dar akitaka huo unga wao nimpe hela au??
 
SoberHouse Inafanya Kazi Ikiwa Mla Madawa Mwenyewe Anayo Nia Ya Dhati Kabisa Ya Kuacha, Kama Hana Nia Hiyo Sober Haisaidii Ni Kuingia Gharama Tu Bure. Kuna Kituo Fulani Nakijua Kuna Mateja Kibao Huwa Wanapewa Methadone Na 5000 Kila Siku, Ila Wakishapewa Wanaendelea Kula Ngada Kama Kawaida
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Unafahamu mtu aliyekuwa addicted na haya makitu akiyakosa zaidi ya siku mbili anakuwaje? kinachofuatia ni kifo, Na atasumbua tu Wafungwa wenzie hili sio suluhisho.

Ampeleke tu sober, akaanze dozi.
Shukran mkuu kwa kunielewesha zaid, naomba kuuliza Hiv sober camp kuna gharama zozote, zikoje??
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,402
2,000
Asanteni mkuu kwa ushauri..mwanzo niliwaza hivyo ila nikawa naogopa tu asitoke huko ndo kaharibiwa kabsa na tabia nyingne...km ushoga!
Ni Kweli Ndugu, Gerezani Siyo Kuzuri ( Speaking From Experience ) Nimeishi Kwenye Kambi Za Wafungwa Kwa Muda Mrefu Nafahamu, Muda Anaweza Kuharibika Akiwa Gerezani. Vitu Kibao Wafungwa Wanaingiza Ndani
 
BlessedHope

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,970
2,000
Pole sanasa Mungu aingiie kati Kigamboni pia kuna vituo vya Sober na vijana wengi wanawekwa huko jaribu kufuatilia kulinganisha gharama na mazingira na pia mitaala yao katika vituo huwa wanaenda madaktari na wanatibiwa pia wanapewa ushauri na kazi mbalimbali
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
SoberHouse Inafanya Kazi Ikiwa Mla Madawa Mwenyewe Anayo Nia Ya Dhati Kabisa Ya Kuacha, Kama Hana Nia Hiyo Sober Haisaidii Ni Kuingia Gharama Tu Bure. Kuna Kituo Fulani Nakijua Kuna Mateja Kibao Huwa Wanapewa Methadone Na 5000 Kila Siku, Ila Wakishapewa Wanaendelea Kula Ngada Kama Kawaida
Dah nielekeze mkuu, hizo meth mbona atatumia huyu, toka nimbonge displine imerud 99%. Tatzo naona je kama akiwa anauhitaji wa shinikizo sabab ni addict..nitafanyaje kwa sasa nilivyompiga pin...Ila naona bado hajawa mteja yule wa kumbea kabsa
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Pole sanasa Mungu aingiie kati Kigamboni pia kuna vituo vya Sober na vijana wengi wanawekwa huko jaribu kufuatilia kulinganisha gharama na mazingira na pia mitaala yao katika vituo huwa wanaenda madaktari na wanatibiwa pia wanapewa ushauri na kazi mbalimbali
Thanks chief, ushauri mzuri!
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
mwalimu mzuri ni ulimwengu mpotezeeni kwa muda umfunze buY a solid heart tu
Huyu rabda tuandae na hela ya mazishi aysee...maana sio pouwa, Ila nikishindwa kabsa hata baada kufuata ushauri huu naopewa itabid movie iishie hivyo tu no way out
 
certified mdokozi

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
1,404
2,000
Huyu rabda tuandae na hela ya mazishi aysee...maana sio pouwa, Ila nikishindwa kabsa hata baada kufuata ushauri huu naopewa itabid movie iishie hivyo tu no way out
Trust maana sober house huanza MoYon mwa mtu nakaa MwanaNYamala naona vijana wengi wakichukua methadon ila hakuna kinachobadirika mpk wao wa amue cha msingi ni kuwaachia tu walimwengu na watu wa namna hii mkishow kucare ndo huFanYa mengi Ya maudhi speakin from experience
 
Vieloon

JF-Expert Member
May 5, 2012
1,520
2,000
Trust maana sober house huanza MoYon mwa mtu nakaa MwanaNYamala naona vijana wengi wakichukua methadon ila hakuna kinachobadirika mpk wao wa amue cha msingi ni kuwaachia tu walimwengu na watu wa namna hii mkishow kucare ndo huFanYa mengi Ya maudhi speakin from experience
Duh...unapita mule mule mkuu, yaani mama akilia kesho anafanya bonge la timbwili...Ila naamini haijafikia huko! Huyu acha niseme nae...siwez kubali kirahis kuona Mzungu anatokea shavu kwa hela ya Dogo, huku yeye dogo akiangamia..
 
Newfame

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
483
1,000
Asante sana mkuu...ngoja nikifika Dar nitajaribu kufanya utafiti wa sober camp. ..ya bagamoyo, tatzo nawaza hiyo tabia yake ya alibadilika badilika, na je nikifika nae Dar akitaka huo unga wao nimpe hela au??
Ya bagamoyo no, nimeishi bagamoyo naifahamu hiyo Sober ni ya wajanja wachache wanaopata fedha za wafadhili/watalii wanaofika Katika huo mji, bagamoyo ni rahisi kupata hayo madude hamna msaada, Ushauri wangu kwanza Mtafutie Mtaalamu wa Saikolojia aweze kumtoa huko mana ameshakuwa addicted hii kazi hata daktari anaiweza kule bagamoyo awe anaenda kufata dawa tu mana hizi dawa ni gharama na asiwe mbali na wewe na awe anameza chini ya usimamizi wako, mara nyingi anapoanza kuachana na haya madude ndio anapoanza kusikia maumivu makali so jiandae mana unaweza muonea huruma, cha msingi awe tayari kukabiliana nayo akiweza ndani ya Mwezi mmoja tu kutokutumoa from now ni rahisi sasa kuacha na atakuwa maeshajitambua ila hii kitu sio nzuri hata kidogo, ni mbaya ikishaingia kwenye Damu na Ubongo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom