Wakuu naomba msaada wa mawazo kwenye hili

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Mdogo wangu anayefanya kazi mpesa amekutana na wakati mgumu baada ya kumtolea hela mtu asiyemfahamu.

Ishu yote ipo hivi, polisi walitoka Mbeya hadi kuja kwa wakala Bagamoyo baada ya kuona hela imetolewa hapo, huyo aliyeenda kutoa hela alitumiwa bahati mbaya yeye akawahi kutoa na hakupatikana tena hewani.

Sasa hivi ni karibia mwezi na nusu, tulipata dhamana lakini aliitwa tena wakamweka ndani, hela iliyotolewa ni laki 4 na nusu lakini hawa polisi mara waseme wanampeleka mahakamani Mbeya huko hela ilipotokea.

Kumpeleka hawampeleki mara wamzungushe wamalizane atoe mil 4.

Kuna mwenye experience kwenye hili naomba ushauri wa namna ya kutoka kwenye hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viol, una uhakika kwamba hela ilitolewa na mteja aliyekuja au ilitumwa kwa wakala moja kwa moja kutokea mbeya
 
Hao polisi Wanataka wakala awe anamhoji kila mteja anaekuja kutoa hela kuwa hiyo hela umeitoa wapi?
Utajuaje mteja anaetoa hela anatoa hela ya wizi???

Kizibo
 
Hao polisi Wanataka wakala awe anamhoji kila mteja anaekuja kutoa hela kuwa hiyo hela umeitoa wapi?
Utajuaje mteja anaetoa hela anatoa hela ya wizi???

Kizibo
Kuna kitu Wakala wengi hawafanyi. Kujaza kitabu cha kutoa hela. Ukitoa hela kuna kitabu unajaza jina lako,namba yako na inabidi utoe kitambulisho aandike namba.

Kuna sehemu huwa natoa mara kwa mara wananiambia niandike jina na namba tu kitambulisho hawaulizi,leo nimeenda Tigo shop wameniomba kitambulisho.

Viol mdogo wako alimwambia huyo alietoa hela ajaze kitabu na kitambulisho alitoa?
 
mimi ushauri wangu km una uhakika alikuja tu na simu yake kutoa pesa then akaondoka then polisi wasumbue hivyo
lkn km una uhakika maelezo ndio hayo hakuna ya ziada unayoficha
unatakiwa wewe upeleke kesi mahakamani usitoe hata sh kumi rushwa 7bu hakuna kosa alofanya mdogo wako
ndugu usiogope mahakama mahakama inamkuta mtu na hatia kwa ushaidi ulochukuliwa pande zote hvyo nenda ufungue shauli upeleke kesi mahakamani yaan laki 4 na nusu utoe rushwa mln 4 kwa jambo ambalo huna kosa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu Wakala wengi hawafanyi. Kujaza kitabu cha kutoa hela. Ukitoa hela kuna kitabu unajaza jina lako,namba yako na inabidi utoe kitambulisho aandike namba.

Kuna sehemu huwa natoa mara kwa mara wananiambia niandike jina na namba tu kitambulisho hawaulizi,leo nimeenda Tigo shop wameniomba kitambulisho.

Viol mdogo wako alimwambia huyo alietoa hela ajaze kitabu na kitambulisho alitoa?
kwanza hiyo mitandao yenyewe vitabu hawatoi sa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaani wana madaftari, Tigo shop wana vitabu vyao
namaanisha zamani kulikuwa na vitabu kabisa km hvyo vya tigoshop ulivyojaza ww
vikijaa kujaza unaenda unapewa vingne lkn kwa sasa tangu wawe hawa wanaoitwa mawakala wakuu hakuna tena vitabu ukienda unaongeza tu "front: tena na hili swala la kupunguziana "front" ndo limezidi kutia uvivu wa kupata vitabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajajanza details za aliyetoa hela
Kuna kitu Wakala wengi hawafanyi. Kujaza kitabu cha kutoa hela. Ukitoa hela kuna kitabu unajaza jina lako,namba yako na inabidi utoe kitambulisho aandike namba.

Kuna sehemu huwa natoa mara kwa mara wananiambia niandike jina na namba tu kitambulisho hawaulizi,leo nimeenda Tigo shop wameniomba kitambulisho.

Viol mdogo wako alimwambia huyo alietoa hela ajaze kitabu na kitambulisho alitoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndio wanapombana.
Hajajanza details za aliyetoa hela

Sent using Jamii Forums mobile app
bado hana kosa linalohusiana na kutoa pesa iloyotumwa kimakosa kupitia laini yake ya uwakala inapaswa hao polisi wadeal na mtandao husika si wakala

kujaza details kwenye kitabu ni Policy za mtandao husika hivyo tigo au voda ndo watampa adhabu muhusika eidha kwa kumfungia laini ya uwakala au kumlipisha faini kwa kuruhusu kutoa pesa bila kujaza details nk
polisi hawana mamlaka yoyote ya kumkamata kisa ametoa pesa iliyotumwa kimakosa
hvyo ndugu bado hana kosa
peleka shauri mahakamani usiogope hao polisi wanatengeneza mazingira ya kupata pesa toka kwako

Hamna sheria inayomtaka Wakala kuweka taarifa za kila anaetoa hela?
 
Back
Top Bottom