Wakuu naomba msaada wa mawaz tafadhali; rafiki angependa kwenda kujifungulia Marekani

Jan 22, 2014
65
38
Wakuu habari za sasa hivi, natumaini nyote mu wazima. Ninaomba kuleta mada hii kwenu ili mnipe msaada wa kimawazo kwa ajili ya rafiki yangu. Rafiki huyu ana boyfriend ambaye ana makaratasi na anaishi Marekani kwa muda mrefu sasa. Rafiki yangu bado tunakula naye vumbi hapa Bongo. Wao walishapanga kufunga ndoa kule mwisho wa mwaka huu kama Mungu atajalia. Hivi karibuni jamaa alikuja bongo na kwa bahati nzuri rafiki yangu hivi sasa ni mjamzito. Hali ya jamaa kule ni ya kawaida sana tu, ni mbeba box mwenye kipato cha kawaida. Rafiki huyu angependa kufahamu iwapo akitaka kwenda kujifungulia kule ni hatua gani atapitia, gharama na namna ya kujiandikisha hospitalini kwa ajili hiyo. Yeye anayo visa ambayo itakwisha muda wake mwakani wakati ambao atakuwa amekwisha jifungua. Anaomba ushauri kwani angependa kujiunga na mumewe mtarajiwa kwe da kubeba box huko. Mumewe mtarajiwa si mtu wa kufahamu mambo mengi. Angependa kufahamu mambo mengi ambayo nyie wakuu mnayafahamu au mna uzoefu nayo. Nafahamu wapo ma-diaspora wengi humu ndani wanaoishi Marekani au waliowahi kuishi huko ambao wanafahamu mambo mengi. Ninaomba mawazo yenu wakuu. Asanteni sana.
 
Wishiful thinking........
She was married by the prince and they lived happily there after. FAIRY TALES
 
miss neddy...it's not 1 sz fits all. Kila situation ina differ. Ila nijuze privately kama kuna issue USA u need a thorough understanding. Karibu!
 
Last edited by a moderator:
Mlavumbi na mwenzako mbona hamrudi kutoa feedback au ndio mmeamua kutongozana kbs huko chemba?
 
Kwa marekani akienda na mimba asahau huyo mtoto bado anakuwa Mtz tu, khs kujifungua sina idea ila huenda bima yake itamsaidia (ingawa hata bima haishughuliki na situation iliyoanza before kuwa ndani ya nchi husika) kama angeconcive akiwa huko!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom