Wakuu naomba mnielekeze huyu anaweza kusoma au kupata shahada?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Habari zenu wana JF? nisiwachoshe kama mnavyojua leo Baraza la Mitihani hapa nchini limetangaza matokeo ya kidato cha sita. Mungu ni Mwema mimi ni mmoja wa waliopokea matokeo hayo vizuri maana nilikuwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu.

Ila huzuni yangu ni kwa best amepata three ya 16 na tulikuwa na mipango ya pamoja hata kusoma chuo kimoja

Swali langu...Huyu mtu anaweza kusoma program yeyote ili kupata degree na kama haiwezekani anatakiwa afanyeje?

Nawasilisha
 
Division 3 anasoma degree, ila inategemea na chuo na pia ajiandae kujilipia ada.
 
Veta ni option nzuri zaidi kama yupo upande wa Arts nina mifano hai mingi sana kusupport hii hoja yangu
 
Sas kwa taarifa yako dogo huyo aliepata point 16 na weeuoipata cjui one. Sas huwend aakakushinda kimasha na kukuacha kwa mbali kilomita elf moja if and only if atajikita kwenye vyuoo hv za kat na kupata utaaalmu Kama wa ardhi,maji misitu nk
 
Baada ya kusoma comment chache hapo juu nimegundua watu wengi hupenda kuonekana kila jambo kulijua bila kuwa na uhakika nalo.

Ndugu Mtoa mada huyo hataweza soma degree yoyote maana hana vigezo ambavyo ni kupata D mbili au zaidi. Sasa huyo hapo ana E mbili na S moja kama hajapata F, Hapo anakuwa amepata vigezo vya Diploma ila siyo Degree.

Hata iwe chuo Binafsi hatapata nafasi ya kusoma Degree.( ingekuwa Kabla ya 2016 angesoma degree maana walikuwa wanachuku E mbili).

Pia hata vyuo vya njee anaeza soma hiyo Degree ila TCU hawataitambua degree yake kwasababu hajakidhi vigezo.
 
Maada juu ya mada.
Naomba kufahamu,mwaka jana mdogo wng alifanya mtihani kidato cha 6 akapata S ya history na S ya kiswahili,akaamua kurisiti hivyo mwaka huu amepata tena E ya histori.Je anaweza omba diploma kwa kuunganisha matokeo aliyopata ktk vikao viliwi alivyorisiti!
#Regards
 
Sas kwa taarifa yako dogo huyo aliepata point 16 na weeuoipata cjui one. Sas huwend aakakushinda kimasha na kukuacha kwa mbali kilomita elf moja if and only if atajikita kwenye vyuoo hv za kat na kupata utaaalmu Kama wa ardhi,maji misitu nk
Maisha sio mashindano wala hakuna guarantee kuwa ukifeli mtihani unafanikiwa au unafeli maisha. Watu niliowaacha la saba, form 2, form 4, form 6 hadi leo hawana kitu chochote cha kunizidi.
Mwenyewe sina chochote cha kuonesha.

Kuna watu hopeless, jitu unafanya nalo mtihani linafeli kisha linasema kusoma haina umuhimu kama elimu ya maisha.
Kama kusoma si muhimu si usifanye mitihani kabisa, ya nini kuwa candidate kisha kubeba sufuria ndo ugeuze maneno?
 
Umetoka form six na hujui vigezo vya kwenda chuo?
Haya mambo si huwa yanajadiriwa kila siku shuleni. Yani points 16 achana na wazo la University kabisa kabisa. Sijawahi kuwa shabiki wa VETA, maybe sijawahi ona wanufaika wake. Naona efforts hizohizo unaweza tumia kwenye issue nyingine ukafanikiwa kabisa.
 
Maada juu ya mada.
Naomba kufahamu,mwaka jana mdogo wng alifanya mtihani kidato cha 6 akapata S ya history na S ya kiwashili,akaamua kurisiti hivyo mwaka huu amepata tena E ya histori.Je anaweza omba diploma kwa kuunganisha matokeo aliyopata ktk vikao viliwi alivyorisiti!
#Regards
I might sound rude to you but to be honest inaonesha wazi huyo mdogo wako mfumo rasmi wa kupitia sekondari hauwezi!

Kwavile siku hizi madogo wanamaliza Six wakiwa wadogo, aende tu pale Chuo cha Mahakama Lushoto akaanze hata certificate kama Diploma atakosa! Hayo mambo ya ku-reseat atakuwa anaendelea kupoteza muda tu kwa sababu huwezi ku-reseat from S kisha unapata E!

Isitoshe, sidhani kama unaweza kuunganisha vyeti kwa kufanya somo moja au mawili!

Na cha kuunganisha chenyewe kipo wapi hapo?! Si bora asome tu certificate ili officially ifahamike baada ya kumaliza Form IV akaenda kusoma certificate kuliko unakuwa na ma-vyeti ya kuunganisha unganisha lakini bado yana ma-E!
 
Back
Top Bottom