Wakuu naomba kujuzwa nini kilichosababisha sukari kupanda bei ukanda wa Afrika Mashariki

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,142
5,634
Wana JF siku za karibuni sukari imepanda bei sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Takwimu zinaonyesha sukari TANZANIA inauzwa kati ya Tsh 2,200/=($1.35)/ na Tsh 2,500/=($1.54) per 1-kg, KENYA Ksh 200 ($2.2) per 1-kg , UGANDA Ush 6,000/=($2.2)per 1-kg,na BURUNDI Fr 2,000/=($1.64)per 1-kg. Inashangaza kuona nchi zote za Afrika Mashari bei ya sukari ni ya juu sana. Wakuu naombeni kujuzwa ni kilichosababisha bei kupanda sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
 
Wana JF siku za karibuni sukari imepanda bei sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Takwimu zinaonyesha sukari TANZANIA inauzwa kati ya Tsh 2,200/=($1.35)/ na Tsh 2,500/=($1.54) per 1-kg, KENYA Ksh 200 ($2.2) per 1-kg , UGANDA Ush 6,000/=(2.2)per 1-kg,na BURUNDI Fr 2,000/=(1.64)per 1-kg. Inashangaza kuona nchi zote za Afrika Mashari bei ya sukari ni ya juu sana. Wakuu naombeni kujuzwa ni kilichosababisha bei kupanda sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Kuna soko jipya South Sudan, hawa jamaa baada ya kupata Uhuru wakaacha kutegeme exports za North Sudan. Wajasiri amali wa eneo hili, hasa kutoka Uganda na Kenya walivamia soko hili jipya na kukausha baadhi ya bidhaa kwenye masoko yetu. Iwapo viwanda vyetu wangekuwa wamejipanga vizuri, basi hapa ndio ilikuwa nafasi ya kuwekeza zaidi lakini badala yake watawala wetu watakibilia majibu ya muda mfupi kama kudhibiti export ya sukari.
 
Mkuu Kakalende hapo ndipo ninapowachoka viongozi wetu. Wakati hamna masoko unakuta wanahaha kutafuta masoko. Soko likipatikana badala ya kuangalia namna ya kuviwezesha viwanda vyetu kuzalisha zaidi na kuuza zaidi , unakuta ndio wanakumbwa na mgawo wa umeme, uzalishaji unakuwa duni, uchumi unazidi kudorora, wakiulizwa wanampango gani wa kutatua tatizo majibu waliyo nayo ni ya kitoto, " hawana uwezo wa kunyesha mvua"
 
Back
Top Bottom