Wakuu, Mwenzenu Uvimilivu Umenishinda!

Mkuu mbona unajichosha hivyo? Hukusikia hilo dubwasha lenu lilisema linatamani malaika ashuke afungie mitandao yote? Wacha lifunge wala hatuna shida!
 
Pole pole katuma barua Twitter kwa kutumia VPN, akiomba isambazwe iwafikie wana CCM wote! Hata hakumbuki kama wanaichi hawana internet sijui ujumbe kama utafika
 
Wakuu natumai wote ni wazima wa afya tele.

Moja kwa moja rejea kichwa cha habari hapo juu.

Kwanza, mimi ni mfuasi mtiifu wa Jiwe, ila hili la kufungia mitandao (zaidi ya wiki sasa) najisikia vibaya.

VPN yenyewe kuipata na kuitumia shida.

Jamani kwa anaejua Mitandao itafunguliwa lini atujuze au ndio tuendelee kuisoma namba tukitembea (Kifua mbele)

Uzi tayari
S. Kide Mtoto wa Mama Shamte ana msemo wake anapenda saana kuutumia kwenye nyimbo zake.

"Wataelewa tu".

Hivi tulivyokuwa tunapigia kelele serikali kubana uhuru mlikuwa hamuelewi kwamba itafikia huku siku moja?
 
Pole sana mfuasi mtiifu wa Jiwe.

We endelea kutembea kifua mbele hadi 2025 huku mtandao hamna!
 
Back
Top Bottom