babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 13,056
- 15,917
kipindi cha nyuma niliwahi kuwa na mahusiano na binti mmoja wa kimarangu hapo mujini bongo,kweli tulipendana sana na baada ya kujitambulisha kwao tu akapata mimba,baada ya hapo ikawa haina jinsi tuangalie mimba kwanza mpaka mtoto akizaliwa ndio tuendelee na mipango mingine ya ndoa,haya kilichotokea toka kipindi ana mimba binti akaanzisha visa vya ajabu ajabu nyumbani mpaka alifikia kunipeleka polisi usiku akasingizia nilimtishia kumuua,haya hayo yakaisha mimi nikaendelea tu kumvumilia nikijua labda ni mimba inamsumbua,baada ya kujifungua tu mama akaanza vituko tena si vya kawaida,ukirudi nyumbani usiku kutoka mihangaikoni unamkuta hayupo,mtoto mdogo kabisa kaachiwa housegirl,ukienda mango garden mida hiyo unamkuta na marafiki zake mda mwingine na mijamaa lakini mi nilikua na chill tu,akiniona anakuja anajidai kanifumania kesho yake yeye wa kwanza kupiga simu moshi kuwaeleza kanishindwa mara kanifumania kumbe mimi ndio nimemfuma usiku nje,haya tuachane na hayo,baadaye nikaja sikia kapata kibwana mdogo kimoja hapo kino kilikua kinauzauza unga basi ndo kinampagawisha,mi nilipoona anazidi kuniumiza kichwa nikaamua kutafuta kazi ya mbali kabisa nayeye,nikichukulia at least akinikosa kwa muda atanikumbuka,atatulia,wacha bwana,nikapata mkataba na jamaa fulani walikua wanafanya reseach ya wanyama na kupiga picha mbuga zote za kusini mwa afrika,nikapata mkataba mzuri miezi 8,baada ya kuondoka na hao jamaa huku nyuma mama ulingo ukawa wake,mtoto kambwaga moshi,ikawa ni yeye na club,club nayeye mimi ananidanganya mtoto yuko nae dar natuma pesa matumizi kilakitu,huku na kule kazini nikapata kawiki ka kupumzika namimi nikarudi dar ghafla,nikampigia simu tayari nishafika nyumbani nakuta nyumba kafunga hayupo nikiuliza majirani wakasema kwanza sikuhizi hapo akija ni kubadili nguo na kuanza,nikampigia simu hakuamini kama nipo dar,haya akarudi homu,kapiga kimini cha kufa mtu,halafu hizo dharau alizonionyesha aliporudi dooh,haya hayo yakapita siku hiyo nililazwa polisi tena baada yakubishana nae kidogo tu,nilipotoka kesho yake nikarudi homu tena yeye sasa akawa ndio mtawala nikisema jambo tu anakimbilia kunipeleka polisi,baada ya kunilaza polisi tena mara ingine nikaona sasa basi,nikaamua kuondoka kabisaaa nikaendelee na maisha kivyangu,alipoona nimeondoka huku nyuma nilikua nimeacha kila kitu nyumbani basi akasaka certificate zangu original akazichana zote,nia yake ili nilost huko nilikoenda,haya mi nikatymia uzoefu tu wa mujini nikapata kazi tena na baadae kidogo alhamdulilah nikampata binti mwingine safii ambaye sio siri alinisaidia sana kipindi hicho kimawazo na kiuwezo kwani yeye alikua anajiweza tu.huyu mama watoto nilipoachana nae akaanza kuishi na huyo jamaa yake kabisa,haya mimi niliendelea na maisha yangu sikuwajali sana licha ya yeye kuendelea kunisumbua kuja kufanya mafujo kwangu,kuniletea mapolisi nyumbani kuvunja vioo vya gari,kupasua simu zangu au kukimbia nazo,kumtukana mama yangu mzazi,na mtoto akanza kumjaza ujinga kama yule jamaa anayeishi naye ndio baba yake!,haya turudi kwenye pointi,mimi nilipoona anazidi kusumbua nikaamua kuondoka kabisa hapo tz,nikaenda ughaibuni,kufika huku kama mnavyojua nimehangaika na box na nikapata mke nimeoa,sasa bahati nzuri huyu mke wangu anapenda sana watoto na akampenda sana mtoto wangu alipoomuona tu kwenye picha,anataka tufanye jitihada za haraka mtoto aje huku asome pamoja na kukaa na sisi hapa,na anataka tukija tu huko likizo hii turudi naye,tatizo nimeongea na mamayake naona tayari kashaanza kuweka migogoro kama kawaida yake,anaanza kuongelea maswala ya pesa bila kuangalia future ya mtoto,ukizingatia mtoto hata yeye mwenyewe hakai naye kwani baada ya mimi kuondoka nayeye huwa mara nyingi yuko china kwa madai anafanya biashara,mtoto yuko kwa mdogo wake,sasa sijui nifanyeje hapo wakuu maana nimeshaona haki ya mtoto sasa inataka kunipotea hivihivi nikiwa kama baba.nishaurini