Wakuu Msaada tafadhali, nitumie dawa gani kurejesha mzunguko wa hedhi?

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Naomba kusaidiwa, ni dawa gani zinaweza saidia kurudisha mzunguko wa hedhi katika hali yake ya kawaida.

Mzunguko umevurugika, Pia dawa zinazoweza saidia kupangilia siku vizuri.

Asanteni
 
Kwanini uvurugike umetumia uzazi wa mpango? Nenda kwa Gynaecologist huko Ndio utapata Tiba sahihi Humu Mara utaambiwa sijui meza Nini Mara chemsha mchaichai unywe!!!

Typed Using KIDOLE
 
Kwanini uvurugike umetumia uzazi wa mpango!?? Nenda kwa Gynaecologist huko Ndio utapata Tiba sahihi Humu Mara utaambiwa sijui meza Nini Mara chemsha mchaichai unywe!!!

Typed Using KIDOLE

Asante mkuu
 
Naomba kusaidiwa, ni dawa gani zinaweza saidia kurudisha mzunguko wa hedhi katika hali yake ya kawaida.

Mzunguko umevurugika, Pia dawa zinazoweza saidia kupangilia siku vizuri.

Asanteni
Dulphaston ila nenda kamwone gyno hormone kuvurugika kuna mengi

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Kwanza tungejua chanzo kilichopelekea. Hakuna mtu professionally anaweza kukupata dawa au kukusaidia tiba bila kujua chanzo cha tatizo. Mazingira Mapya, Vyakula, Uzazi wa mpango haswa P2, Kutoa Mimba bila kusafishwa na N.K

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatumia njia za uzazi wa mpango?
Ulimeza P2?
Kama umetumia hayo madude hakuna dawa we tulia tu upate hasara yake....

Kingine hujasema mzunguko umevurugika vipi kwamba dates zinawahi/ kuchelewa, unapata damu kidogo/ nyingi...
Unaenda siku chache/nyingi tofauti na mwanzoni au kimekusibu nini?
 
Ck zimekuw chache, zimekuwa 21 badala ya 28 nilivozoea
 
Ck zimekuw chache, zimekuwa 21 badala ya 28 nilivozoea
Ulimeza P2? Kama ulimeza basi chanzo ndio hicho maana yenyewe uwa inaweza kukuwaishia ama kuchelewesha.

Pia wakati mwingine uwa ni hali ya hewa tu in case kama ulibadilisha mazingira. Halafu umenotice kwa kipindi cha muda upi? I mean zimechange kwa mwezi huu tu au ishazidi 3? Kama imeshazidi ongoza kwa gyno usiende pharmacy
 
Back
Top Bottom