Wakuu, Je Mnajua ya Kuwa Katika Shule Zetu za Msingi za Serikali......

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Kuna upungufu wa madawati 1,836,402. Hii ni sawa na asilimia 49.1 ya mahitaji. Kwa maneno mengine karibu nusu ya watoto wetu katika shule hizo za msingi wanakaa chini kama si kukaa watoto wanne katika dawati moja ambalo linatakiwa likaliwe na wanafunzi wawili tu. Kazi ipo. Katika shule ambazo si za Serikali wana upungufu wa madawati 43,404 ambayo ni sawa na asilimia 28.7 ya mahitaji.
 
Wala sishangai kwani hata Shule ya mtaani kwetu (Ndumbwi Pr. School), Mbezi Beach - Jogoo (DSM) wadogo zetu wamekaa chini sana...
 
Naona inahitaji muugiza kuweza kubadili hali hii kwani Wakuu wetu inaonekana hali hii haiwasumbui hata kidogo.
 
Kuna upungufu wa madawati 1,836,402. Hii ni sawa na asilimia 49.1 ya mahitaji. Kwa maneno mengine karibu nusu ya watoto wetu katika shule hizo za msingi wanakaa chini kama si kukaa watoto wanne katika dawati moja ambalo linatakiwa likaliwe na wanafunzi wawili tu. Kazi ipo. Katika shule ambazo si za Serikali wana upungufu wa madawati 43,404 ambayo ni sawa na asilimia 28.7 ya mahitaji.

ccm hoyeeee! kikwete hoyeeee! Hayo ni maendeleo na hamtakiwi kuyabeza. Kuna nchi hapa duniani hata hapo hawajafikia
 
Viongozi hawawezi kuona tatizo hilo sababu watoto wao hawasomi shule hizo,kazi yao kusafirisha magogo na mbao kwenda nchi nyingine badala ya kutumika kutengeneza madawati
 
Back
Top Bottom