Wakuu hivi rafiki akifa ndani kwako Sheria inasemaje kuhusu hilo?

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
1,955
2,166
Heshima kwenu wakuu.

Naomba twende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Tuchukulie nina rafiki yangu amelala ndani kwangu then ikatokea bahati mbaya akafa akiwa usingizini, sheria inasemaje kuhusiana na hilo wakuu?

Naombeni muongozo tafadhali. Thanks.
 
Utatoa Ripoti kwa Viongozi wa Eneo Lako Then Wao Watakusaidia Kutoa Taarifa Polisi, watakuja kufanya upelelezi wao then Watampeleka Hospital Kufanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi na Madaktari.

Ila Kumbuka Suspect wa Kwanza Ni Wewe
Hivyo Utasaidia Zoezi la Upelelezi Kukamilika.
Itakuwa Usumbufu Kidogo Itakubidi Kuvumilia.

Pia Tunakuaga na Tendency ya Kukaribisha Wageni Bila Kutoa Taarifa kwa Viongozi wa Mtaa, Au Kuhama Mtaa Flani Bila Kutoa Taarifa.
Umuhimu wa Kutoa Taarifa ndio Utauona Tukio Kama Hill Likitokea.

Wajuvi Zaidi Nawasubiri Nami Najifunza.
 
Utatoa Ripoti kwa Viongozi wa Eneo Lako Then Wao Watakusaidia Kutoa Taarifa Polisi,Watakuja Kufanya Upelelezi Wao Then Watampeleka Hospital Kufanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi na Madaktari.

Ila Kumbuka Suspect wa Kwanza Ni Wewe
Hivyo Utasaidia Zoezi la Upelelezi Kukamilika.
Itakuwa Usumbufu Kidogo Itakubidi Kuvumilia.

Pia Tunakuaga na Tendency ya Kukaribisha Wageni Bila Kutoa Taarifa kwa Viongozi wa Mtaa,Au Kuhama Mtaa Flani Bila Kutoa Taarifa.
Umuhimu wa Kutoa Taarifa ndo Utauona Tukio Kama Hill Likitokea.

Wajuvi Zaidi Nawasubiri Nami Najifunza.
Mkuu wewe huwa unafanyaa hivo?? Kutoa taarifa kwa mjumbe kila upatapo mgeni??
 
Dadeki kafa nini jamaa ndani kwako! ... By the way uchunguzi wa dactari ndio utaonesha amekufa kwa sababu gani, Ikionesha kuna viashiria vya kuasababishiwa kifo au kuuawa lazima uwe na kesi ya kujibu kwa kosa la mauaji. Sasa hukumu itakuja kwamba ulimuuaje huyo mtu kwa kukusudia au bila kukusudia nyundo ya maisha au 30 jela inakuhusu.
Ila kama alikufa bahati mbaya huna kesi wala.
 
Hivi kwa mfano kama huyo mtu akawa njiani huko alikula kitu kisichofaa (poison) na safari yake ya mwisho ndio akaja "ghetto " na akarudisha namba. Uchunguzi ukionesha kuna viambata hatarishi mwilini mwake, je hali itakuwaje kwa mwenyeji?

NB: siku hizi watu wanabugia tu vitu hovyo hovyo barabarani, mara madawa ya asili, mara supu+juice na dawa nyinginezo na vinywaji nishati. Vitu hivi ni hatari sana kwa afya na vikimuondoa mtu lazima viache trace tatanishi.
 
Hapo unafungwa tu
Hamna jinsi
 
Back
Top Bottom