Wakuu hivi IMF/WORLD BANK kuna ngozi nyeusi yoyote ishawahi kuongoza

Wakuu ni swali za kizushu hivi haya mashirika ngozi nyeusi kwanini hatupewi kuongoza?

Edwin Mtei alishawahi kuwa Asst. MD wa IMF.

Anyway, kama walivyosema wengine, ni UTAMADUNI kuwa WB inaongozwa na US na IMF na Eurozone. Kwa sasa hivi, wanajaribu kuangalia uwezekano wa kuondokana na utamaduni huu kwa kumchangua IMF Boss kutoka; Brazil, Turkey, SA, India au Mexico kwa sababu mataifa haya emergent (pamoja na BRICS) yamevunja ile dhana ya kuwa uchumi bora uko US na Europe pekee.

Kwa Afrika, kiukweli sidhani kuwa tunaweza hata kuongoza FIFA.
 
kama mmeona kuna sheria kandamizi na hakuna la kufanya kubadilisha ndo maana mdau hapo juu akakwambia tuanzishe vyombo vyetu na sio lazima viitwe wb au imf,..tunaweza kuviita blacks bank kama unavyotaka weusi wako uwe priority,.hivi koffi anaan alipokuwa bosi wa UN alifanya nini kuwasaidia watu weusi zaidi ya kuwa kibaraka mpole kama msukule!obama je?anamwaga madola africa au??

WB na IMF ni vyombo pekee katika Uchumi wa dunia. Hauwezi ukatunga tuu chombo kingine kufanya kazi hizo. Zina kazi mbili;

1. IMF

Mataifa yanapofanya biasahara kuna kitu kinaitwa Mizania ya Biashara (balance of trade). Nchi moja inaponunua vitu vingi kuliko inavyouza nje, inleta hali ya hii nchi kubidi kukopa kulipia hii ziada. Kimsingi hii siyo mbaya - mpaka pale madeni yanapokuwa makubwa mno. Ikitokea hii, hiyo nchi hupoteza uwezo wake wa kukopa na kwa hiyo wadeni wake nao wanaumia. Uchumi wa dunia unakuwa hatarini.

Kazi ya IMF ni kukopesha kwa mataifa yaliyofikia hatua hii ya kutokopeka. IMF inapokukopa hela, itakuambia ubadilishe namna unavyoishi, ili uweze kurejesha uchumi wako katika hali nzuri. Watakuambia uache kununua vitu nje, uongeze uzalishaji, upunguze matumizi yasiyo na msingi. Masharti haya ndiyo yanafanya watu wasizimie sana IMF - lakini wanapaswa kukumbuka kuwa wamejiweka katika halii hii wenyewe kwa kuendekeza anasa.

2. World Bank

World Bank ipo kwa ajili ya kutoa misaada kwa mataifa ambayo ni mazembe tu. Mataifa ambayo yameshindwa kutoa huduma kwa wananchi wake, k.m elimu, afya, miundombinu. Missada hii hulenga zaidi kuleta ahueni kwa wananchi - na ndiyo maana watu wanaipenda-penda WB.

WB na IMF zipo kikazi zaidi. Hazipo kwa ajili ya kugawana vyeo. Vyeo ni lazima vijazwe, lakini utaonekana ni mtu wa ajabu sana ukitoka kwenye nchi iliyoshindwa kujiendesha na kuanza kudai eti unataka MD awe anatoka kwenye nchi zembe.

Edwin Mtei alishawahi kuwa Asst. MD wa IMF.

Anyway, kama walivyosema wengine, ni UTAMADUNI kuwa WB inaongozwa na US na IMF na Eurozone. Kwa sasa hivi, wanajaribu kuangalia uwezekano wa kuondokana na utamaduni huu kwa kumchangua IMF Boss kutoka; Brazil, Turkey, SA, India au Mexico kwa sababu mataifa haya emergent (pamoja na BRICS) yamevunja ile dhana ya kuwa uchumi bora uko US na Europe pekee.

Kwa Afrika, kiukweli sidhani kuwa tunaweza hata kuongoza FIFA.

mkuu tunaweza sema tatizo hatujiamini
 
WB na IMF ni vyombo pekee katika Uchumi wa dunia. Hauwezi ukatunga tuu chombo kingine kufanya kazi hizo. Zina kazi mbili;

1. IMF

Mataifa yanapofanya biasahara kuna kitu kinaitwa Mizania ya Biashara (balance of trade). Nchi moja inaponunua vitu vingi kuliko inavyouza nje, inleta hali ya hii nchi kubidi kukopa kulipia hii ziada. Kimsingi hii siyo mbaya - mpaka pale madeni yanapokuwa makubwa mno. Ikitokea hii, hiyo nchi hupoteza uwezo wake wa kukopa na kwa hiyo wadeni wake nao wanaumia. Uchumi wa dunia unakuwa hatarini.

Kazi ya IMF ni kukopesha kwa mataifa yaliyofikia hatua hii ya kutokopeka. IMF inapokukopa hela, itakuambia ubadilishe namna unavyoishi, ili uweze kurejesha uchumi wako katika hali nzuri. Watakuambia uache kununua vitu nje, uongeze uzalishaji, upunguze matumizi yasiyo na msingi. Masharti haya ndiyo yanafanya watu wasizimie sana IMF - lakini wanapaswa kukumbuka kuwa wamejiweka katika halii hii wenyewe kwa kuendekeza anasa.

2. World Bank

World Bank ipo kwa ajili ya kutoa misaada kwa mataifa ambayo ni mazembe tu. Mataifa ambayo yameshindwa kutoa huduma kwa wananchi wake, k.m elimu, afya, miundombinu. Missada hii hulenga zaidi kuleta ahueni kwa wananchi - na ndiyo maana watu wanaipenda-penda WB.

WB na IMF zipo kikazi zaidi. Hazipo kwa ajili ya kugawana vyeo. Vyeo ni lazima vijazwe, lakini utaonekana ni mtu wa ajabu sana ukitoka kwenye nchi iliyoshindwa kujiendesha na kuanza kudai eti unataka MD awe anatoka kwenye nchi zembe.

kwahiyo mkuu nchi zembe haziwez kutoa mtu haiwezekani ndugu mbona kuna watu wako vizuri sana
 
mimi nafikiria labda hawatuamini,lakini kweli tumekaa kama hatujiamini kabisaaaa

avatar44021_1.gif

Samahani Mtorii, japo ni nje ya mada.,hivi hii avatar yako inamaanisha nini, naona kama huyo jamaa ana miguu 3 au ni macho yangu ndio yananipoteza?
 
Maisha ni vita jipiganie uwezavyo.sisi tumeendekeza uchawi badala ya kupiga kazi.tokomeza ushirikina kwanza
 
Tangu WB ianzishwe haijawahi kuwa na President ambaye sio US citizen and reason is US is the largest shareholder in the bank,ni swala la citizenship sio race ya mtu
 
mimi nayaona ni mashirika kandamizi

..wako makini na mikopo yao na hawatoi bila masharti la sivyo magamba wangechukua na kuishia kupigia kampeni za udiwani,ni kandamizi kwa sababu wanakupa masharti lakini interest zao ni karibu na bure ukilinganisha na traditional banks.
 
Tangu WB ianzishwe haijawahi kuwa na President ambaye sio US citizen and reason is US is the largest shareholder in the bank,ni swala la citizenship sio race ya mtu

This is critical thnking! Kiukweli ukiwa una hisa kubwa mahali, ni lazima uwe kiongozi ili kulinda hisa zako zifanye kazi iliyokusudiwa, pia kulinda maslah yako. Mfano, kwenye makampuni binafsi mengi sana MD huwa ni yule mwenye hisa kubwa. Hvyo, kwa raia wa Marekani kuwa ndio MD wa mashirika hayo, naona ni sawa tu, labda itokee mataifa mengine yawe hisa kushinda Marekani
 
..wako makini na mikopo yao na hawatoi bila masharti la sivyo magamba wangechukua na kuishia kupigia kampeni za udiwani,ni kandamizi kwa sababu wanakupa masharti lakini interest zao ni karibu na bure ukilinganisha na traditional banks.

Upo sawa mkuu
 
Back
Top Bottom