Wakuu hivi huwa mnaishi vipi na aina hii ya watu?

sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,873
2,000
Wakuu habari

CHANGAMOTO SANA KUISHI NA WATU WASIOJITAMBUA.

Sijui niitengeneze vipi hoja yangu ila nahisi nitaeleweka...Ipo hivi kuna baadhi ya watu nahisi kama huwa hawajitambui/wana matatizo hivi.. na hii ni kwa level zote haijalishi ni wasomi au wasio wasomi.

Nianze hivi... ulishawahi kukaa/kuzungumza na mtu ndani ya dk 1 tuu ukamchukia hata hutaki kumuona tena?....au wakati mwingine ukimuona kwa mbali unabadilisha muelekeo wa barabara?...aseew yaani kuna watu wanazungumza hovyo alafu wanakera

Kwa ufupi huwa sina haiba ya kuzungumza zungumza au kuzungumza na simu ndio sipendi kabisa... sabbu hata mara ya mwisho kujiunga dk ilikuwa mwaka jana mwezi wa 12...Kibaya mtu anazungumza na wewe alafu ni maneno ya umbea umbea tuu + uongo mwingi hauna maana yoyote...na hizo haiba hazipo damuni kabisa ila unakuta jitu lina nang'aniza tuu

Kibaya zaidi hata nikijikwepa au kutulia masimu yanapigwa tuu hovyo hovyo mara huyu mara yule nikiizima nakuta messages ...

Nahisi kuna baadhi ya watu huwa hawajitambui hata ile kumsoma mtu emotion + facial expression inamuwia ugumu.

Huwa natamani kuwaambia ukweli ila nahisi wakati mwingine maisha ya kuambiana ukweli muda mwingine ni kutengeneza uadui au waseme nina jeuri,kujiona,kujisikia nk

1:Vipi kwenu wakuu ni tabia zipi huwa zinawakera kutoka kwenye hili kundi la hawa watu na jinsi gani mnazikabili?

2:Au njia zipi nifanye ili hata nikikutana/kuzungumza nao zinifanikishe?

Ila yote kwa yote sina haiba ya kujichanganya na mtu/watu kabisa...dk 5 ni nyingi sana.
 
binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,584
2,000
Mkuu sio kwamba tatizo ni wewe? kwanini usiwe appreciative? kwamba kumkubali mtu au kumvumilia mtu na mapungufu yake. Au mbinu nyingine ni kutokuwa serious na watu.

Swali je kuna watu unawafurahia? kama wapo ni watu wa aina gani? kama ndivyo hao uliowaita kuwa hawajitambui unawavumilia tu siku ziende sababu naona pengine huwezi kuwaepuka.
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,118
2,000
Sijui hata kama umesoma nilichokiandika...

Kwa sabbu naona ninachokihitaji na ulichonijibu ni tofauti kabisa!
Ishu ni kuwa hupendi kuchangamana na watu

Kuna namna fulani hivi unajihisi wewe ni special/una majivuno

Una u anti social fulani hivi + kiburi

Kama maisha ni kurekebishana iweje uogope kumwambia ukweli mtu pale ambapo unaamini amekosea?

Sababu ya kumchukia mtu kwa madhaifu yake sijaona logic au kuchukia mtu for no reason!
Naamini watu tunatofautiana, na ndio maana watu wote hawawezi kuwa kama wewe..

Mungu ana malengo yake kuumba watu tofauti, hatutakaa tufanane kimawazo, kimatendo, kimtazamo n.k
 
TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
381
500
Mkuu Mimi nilikuw Kiongozi na nimeongoz na dizan ya watu Kam hao ikabd nijiuzulu tuuu

Maan wanajua wanajifany hawajui
 
sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,873
2,000
Ishu ni kuwa hupendi kuchangamana na watu

Kuna namna fulani hivi unajihisi wewe ni special/una majivuno

Una u anti social fulani hivi + kiburi

Kama maisha ni kurekebishana iweje uogope kumwambia ukweli mtu pale ambapo unaamini amekosea?

Sababu ya kumchukia mtu kwa madhaifu yake sijaona logic au kuchukia mtu for no reason!
Naamini watu tunatofautiana, na ndio maana watu wote hawawezi kuwa kama wewe..

Mungu ana malengo yake kuumba watu tofauti, hatutakaa tufanane kimawazo, kimatendo, kimtazamo n.k
Nahisi ni mitamo yako tuu hii au hisia...ila kiukweli hata tukikutana leo huwezi kunishuku kwa lolote uliyoyataja hapo.

Jua kuwa sipendi kabisa kuonekana machoni pa watu.
 
sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,873
2,000
Hatua ya kwanza zima simu kabisa au iuze hutapigiwa wala hutaona SMS tena maishani mwako

Hao unaokutana nao njiani akianza mtu umbea mwambie twende polisi ukanielezee huko
Utakua huru katika dunia hii ya mola
Mkuu unazungumza simpo sana.

Sasa niuze simu ilihali nina mambo ya kufanya Chief
 
sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,873
2,000
Mkuu sio kwamba tatizo ni wewe? kwanini usiwe appreciative? kwamba kumkubali mtu au kumvumilia mtu na mapungufu yake. Au mbinu nyingine ni kutokuwa serious na watu.

Swali je kuna watu unawafurahia? kama wapo ni watu wa aina gani? kama ndivyo hao uliowaita kuwa hawajitambui unawavumilia tu siku ziende sababu naona pengine huwezi kuwaepuka.
NIELEWEKE:Ndio maana mimeandika baadhi...
Kwenye issue ya mapungufu sina napo tatizo nalifahamu hilo.

Ila kuna watu viwembe bhana...yaani kuzungumza umbea umbea muda wote alaf anaona sichangangii bado anaendeleza tuu Aah.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom