Wakuu, jambo hili limenitikisa

lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,168
2,657
Kiasili sina maadui niwajuao direct humu duniani labda haters wa hapa na pale pamoja na yoooote sijawahi kubeba vinyongo kwenye moyo wangu sipendi mtu anidharau wala sidharau mtu,nikipita salamu simpiti mtu, kazini ndani siyo mtu wa vijiwe, bar wala chochote cha hivyo. Hizi social meetings labda msiba, jumuiya, sherehe ndio utanikuta na bado sina maneno mengi. Bhasiii bhana, ikaenda ikaenda nyie watu wazima wenzangu mtakuwa mmeshajua.

Kuna jambo nikawa nahisi muda mrefu linaendelea ila Mimi sina ushahidi nilihangaika nalo mwisho nikasema sifi na tai shingoni nikaingia mtaani nichukue data nikaongea na watu karibuni 9 hivi wote wakanambia mbona hiyo kitu inajulikana na MTT hata wa miaka 7 iko uchi ndio hivyo nikatajiwa hadi eneo pendwa la huo uovu unapofanyikia.

Kumbe watu walikuwa wanajisemea eti nilikuwa najua nikaamua tu kunyamaza! Nasikia mwenzangu aliwahi kuitwa akaonywa alichojibu ni kila mtu na maisha yake. Sijawahi kuvunjika moyo kiasi hicho, mtaani nikitembea kila mtu ananitizama kwa jicho ambalo silielewi mbaya zaidi aliyenifanyia ushenzi ni Jirani yangu pua na mdomo yaan sukari na Chai.

Hii kitu imeondoka na kilo zangu nyingi,nimeloose appetite kabisa wakuu najefeel soso down yaan sijui nielezeje sina hata hamu ya kupita barabarani kuna siku nilishindwa kuandika mikono ilinitetemeka plus machozi. Huyo mwenzangu ameniomba msamaha ,bado nafikiri cha kufanya moyo wangu umejeruhika mno kuliko maelezo najua kuna psychologist humu, kuna watu wenye maarifa na wasomi nifanyeje nirudie furaha yangu ya zamani.

Naomba kama utanikebehi don't comment maana itakuwa kunitilia chumvi kidondani msaada wenu wakuu, mahusiano hayo ni rasmi mbele za Mungu na wanadamu. Kwa Mara ya kwanza sisalimiani na huyo ibilisi aliyenizunguka! Bado sijajua nifanyeje na yeye nimuumize kama alivyoniumiza. Maumivu Niliyo nayo bora uchapwe fimbo kinachouma zaidi uaminifu uliotukuka nilio nao!
 
Aiseee pole sana dada
Dunia inaa mambo yanaumiza san na kukutoa kwenye furaha kabisa.

Jaribu kwenda kuishi mbali na hapo na ikiwezekana kwa mazingira yako muache tuu huy jamaa it may be worthy
 
Mbona umeandika kwa jazba sana , vuta punzi punguza asila hafu edit post yako Tena. Ila fahamu mwanaume dudu haitanuki so ruksa kugonga nje ndani muhimu kujali afya yako na mke wa ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, pole sana, inaonesha umeumizwa sana, jipe moyo na hiki ni kipindi cha kuwa karibu na Mungu wako, maombi zaidi yana hitajika mno, omba kwa imani utaona miujiza, achilia tu roho ya msamaha kwa huyo aliekukosea!!

Kila la heri mkuu, pole sana!!
 
Mkuu kuna tiger within me ameamka sielewi alipotokea nataka tu watesi wangu niwarudishie maumivu na aibu waliyoniletea....sijui how mwenzangu ameomba msamaha ambayo ni pending kwangu.
 
Pole sana, in this Life I learn kutokuwekeza hisia kwa binadamu na kumwamini pia nimejifunza no one is perfect, na mengine huwa ni kuteleza tu, pia nimejifunza kuji limit kujipatia furaha yangu ninapotaka jambo la ku satify akili yangu na mwili siji limit.

Duh pole sana
 
Mkuu kuna tiger within me ameamka sielewi alipotokea nataka tu watesi wangu niwarudishie maumivu na aibu waliyoniletea....sijui how mwenzangu ameomba msamaha ambayo ni pending kwangu.
Saa nyingine ka waweza revenge do it moyo utapata amani ka ni mtu wa kusamehe na haumii fanya hvo ka waendelea kuumia revenge huwa inaponya pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom