matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,570
- 15,319
Tulizoea zamani mtu akienda Ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania.
Jana baada ya miezi kama tisa hivi kukaa upande mmoja wa jiji LA DSM bila kuzunguka niliachwa mdomo wazi.
1: Kuna Majengo Mapya makubwa mazuri hatari. Mfano mitaa ya Makumbusho Victoria yaani hadi unatabasamu tu kwa jinsi miundombinu na design zilivyosambazwa pale. Lililoniacha hoi ni jengo moja hivi maeneo ya palm beach. Ile kitu ni matata sana. What a design!
2: Kale kadaraja ka masaki baharini mwanzoni nilidhani ni vile kama vya Miti chini kwa chini Jana nimeshangaa kunastructure za hatari wanazimount pale kumbe ni kitu hatari Sana.
3: Nikapita Ubungo Simu2000 na stand ya mabasi napo kuna road zimesukwa pale ndani ya muda mfupi utapenda. Naona wanajiandaa kuweka taa za barabarani ukiongezea Interchange. Alafu ukichungulia kuelekea Mlimani city aisee pako Bomba sana.
4: Nikachungulia CCBRT, hadi nikadhani nimekosea njia. Kuna zinga la hospitali. Yaani Majengo mengi Mapya mageti mengi ya kuingilia hawajaifungua. Hadi nikajiuliza kwa nini hata Mloganzila ilijengwa. Maana kile nilichokiona Wenda hata Muhimbili inaweza isifue dafu licha ya Eneo kuwa dogo.
Nikapita Mbagala, kuna structure flani barabarani zinainuliwa pale nadhani ni kwa ajili ya mwendokasi au sijui ni daraja basi napo patakuwa poa sana.
Kimsingi nina mpango wa kwenda nchi kadhaa Ulaya lakini nikifika nitapiga Picha kwenye mabarafu tu ila Majengo kama background sidhani maana hicho nilichokiona Jana hata Ulaya hakuna.
Msema Kweli ni mapenzi wa Mungu. Natamani kupata Picha ya aerial views current ya maeneo mengi ya jiji.