Wakuu, hatua lilipofikia hili jiji la Dar es Salaam, hakuna tena hamasa watu kwenda Ulaya au US kupiga picha

Ulaya umewahi kufika wewe???!tambua unavyoona tz inazidikuendelea mara tano yake amka wewe
 
Nalinganisha Picha zawadau wangu walio Ulaya wanazopiga kwa kutumika nguvu nyingi kutafuta background zenye mvuto wa kimiundombinu naona hata huku ni zaidi.

Sio lazima ufike. Hata Googlesatellite unaweza kutembezwa manispaa nzima za Mimi mingi ya Ulaya. Tena ukapewa na 3D view.

Kuna mlaya mmoja tulikuwa tuazunguka akinitembeza kwa google satellite mitaa ya Ireland yote hadi chumba alichopanga tunavuta hadi Dirisha. Kawaida sana
Uzi ufungwe. Nadhani tumeona mtoa mada ni nani.
 
Ungekuwa umefika hata Jburg au Pretoria ungegundua kuwa ulichoandika siyo kweli.
Hebu tazama utofauti wa picha hizi mbili
Hii ni ubungo
View attachment 1682166

Hii Gothenburg Sweden
View attachment 1682168
ni suala la muda tu hivyo vibanda vya pembeni vyote vibomolewe pajengwe majengo, kumbuka stendi ya ubungo unahamia mbezi louis hivyo majengo vibiashara vyote vya hapo ubungo inabidi vihame kufuata wateja wao, na hivyo kuacha nafasi ya hivyo vijumba vidogo kubomolewa kujenga vitu vipya
 
Mtoa naona unajitahidi sanaaa kufananisha tembo na sisiminzi lkn umeshimdwa kutushawishi ...embu utuletee picha izo zinazo kupagawisha za Dsm then tukushishie picha miji ya izo nchi za ulaya ..unaweza ukazimia mtoa UZI acha zarau nenda CHATO ukaishi
Chato huwezi kuilinganisha na kijiji chochote ulaya Mkuu. Uwe na adabu.

Uwanja wa ndege runway almost vizio kama vya JKNIA.
Bank,referal hospital, MSD, Mbuga etc, ukileta kijiji ulaya CHANYA yote hayo nitajisaidia hadharani.

Hakuna. Ila usilete nyumba za wanavijiji maana huko bado hatujawafikia
 
Tulizoea zamani mtu akienda Ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania.

Jana baada ya miezi kama tisa hivi kukaa upande mmoja wa jiji LA DSM bila kuzunguka niliachwa mdomo wazi.

1: Kuna Majengo Mapya makubwa mazuri hatari. Mfano mitaa ya Makumbusho Victoria yaani hadi unatabasamu tu kwa jinsi miundombinu na design zilivyosambazwa pale. Lililoniacha hoi ni jengo moja hivi maeneo ya palm beach. Ile kitu ni matata sana. What a design!

2: Kale kadaraja ka masaki baharini mwanzoni nilidhani ni vile kama vya Miti chini kwa chini Jana nimeshangaa kunastructure za hatari wanazimount pale kumbe ni kitu hatari Sana.

3: Nikapita Ubungo Simu2000 na stand ya mabasi napo kuna road zimesukwa pale ndani ya muda mfupi utapenda. Naona wanajiandaa kuweka taa za barabarani ukiongezea Interchange. Alafu ukichungulia kuelekea Mlimani city aisee pako Bomba sana.

4: Nikachungulia CCBRT, hadi nikadhani nimekosea njia. Kuna zinga la hospitali. Yaani Majengo mengi Mapya mageti mengi ya kuingilia hawajaifungua. Hadi nikajiuliza kwa nini hata Mloganzila ilijengwa. Maana kile nilichokiona Wenda hata Muhimbili inaweza isifue dafu licha ya Eneo kuwa dogo.

Nikapita Mbagala, kuna structure flani barabarani zinainuliwa pale nadhani ni kwa ajili ya mwendokasi au sijui ni daraja basi napo patakuwa poa sana.

Kimsingi nina mpango wa kwenda nchi kadhaa Ulaya lakini nikifika nitapiga Picha kwenye mabarafu tu ila Majengo kama background sidhani maana hicho nilichokiona Jana hata Ulaya hakuna.

Msema Kweli ni mapenzi wa Mungu. Natamani kupata Picha ya aerial views current ya maeneo mengi ya jiji.
Picha jamani, habari gani hizi za nusu nusu!
 
ni suala la muda tu hivyo vibanda vya pembeni vyote vibomolewe pajengwe majengo, kumbuka stendi ya ubungo unahamia mbezi louis hivyo majengo vibiashara vyote vya hapo ubungo inabidi vihame kufuata wateja wao, na hivyo kuacha nafasi ya hivyo vijumba vidogo kubomolewa kujenga vitu vipya
Basi ni mpaka huo muda ufike ila kwakuwa haujafika bado watu wana sababu ya kwenda kupiga picha huko ulimwenguni
 
Unafànya mkuu haupo seriously na mada yako Ilaya next levels sisi hata Kigali hatuwafikii.
Acheni dharau?! Yaani unafananisha utopolo Kigali na Dsm,?!! Kuwa na heshima na jiji la Kunenge usilifananishe na vi miji vidogo vidogo, Kigali ni size ya moshi au Arusha.
 
Chato huwezi kuilinganisha na kijiji chochote ulaya Mkuu. Uwe na adabu.

Uwanja wa ndege runway almost vizio kama vya JKNIA.
Bank,referal hospital, MSD, Mbuga etc, ukileta kijiji ulaya CHANYA yote hayo nitajisaidia hadharani.

Hakuna. Ila usilete nyumba za wanavijiji maana huko bado hatujawafikia
Hahaha ukada utakuumbua TEMBEA UJIONE
 
Ndio maana nme muacha kumbe ni mwehu
Ushabiki huu ndio maana huwa tunawaacha mtapeliwe.
Mwenzako anzungumzia 1880s wakati Mimi nazungumzia 1890 Wakati Tesla aliposikimika magurudumu Niagara falls na kwa Mara ya kwanza New York Umeme usiku ukawaka kama Mchana.

Edson na viumeme vyake vya DC New York ilikuwa kama vijiji vinavyotumia tusolar TWA DC. Umeme kama kibatari. Huwezi kulinganisha na surprise ya Tesla ambayo wazungu walirukaruka usiku kama wehu kushangaa taa zinavyotoa mwanga wa kutosha.

New York ilikuwa ya kipuuzi kuliko vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa REA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom