Wakuu, hatua lilipofikia hili jiji la Dar es Salaam, hakuna tena hamasa watu kwenda Ulaya au US kupiga picha

Tulizoea zamani mtu akienda ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania...
Unaisikia tuu ulaya au umewahi kufika ndugu yangu. Yaani wale walishatiacha miaka Mia mingi iliyopita.

Mimi japo sijafika ulaya nilifanikiwa kuishi Thailand january 2018 mpaka mpaka December 2019 na mara kadhaa nikiwa jijini Bangkok, nikitembelee miji kama Huahin, Pattaya, Chiangmai, Nakorn Rachasima. Nasema hivi jiji la Dar es salaam bado Sana Kwa miundombinu huwezi kufananisha na ulaya .

Niliyoyaona Bangkok japo ni asia nasema hivi hata theluthi Yao hatujafikia . Tuna Miaka mingi ya kujifananisha nao . Nenda hata Johannesburg labda utaleta mrejesho
 
Hii nchi hela nyingi Sana Inaenda kwenye miundo mbinu hasa barabara Kwa Gharama za ufukara wa wananchi...... Kuna jamaa angu engineer huwa namwambia msipopiga hela utawala huu, utawala mwingine ukija mtalia na kusaga meno
Utawala gani ambao hautajenga miundombinu?
 
Unaisikia tuu ulaya au umewahi kufika ndugu yangu. Yaani wale walishatiacha miaka Mia mingi iliyopita. Mimi japo sijafika ulaya nilifanikiwa kuishi Thailand january 2018 mpaka mpaka December 2019 na mara kadhaa nikiwa jijini Bangkok, nikitembelee miji kama Huahin, Pattaya, Chiangmai, Nakorn Rachasima. Nasema hivi jiji la Dar es salaam bado Sana Kwa miundombinu huwezi kufananisha na ulaya . Niliyoyaona Bangkok japo ni asia nasema hivi hata theluthi Yao hatujafikia . Tuna Miaka mingi ya kujifananisha nao . Nenda hata Johannesburg labda utaleta mrejesho
Ndio maana sijasema far east nimesoma ulaya. Maana hata mafundi wa hizi design sidhani kama ni wazungu ni watu wa far east china na korea huko. Pia sijasema jiji zima. Natambua ulaya nzima hata uzungukeje huwezi kukutana mitaa kama ya kwetu KISEMVULE au MAHAKAMA YA MBUZI.

Mkuu usome vizuri, nimekuwa veerevere specific. Na hapa ndio huwa mnafeli wengi. Uwezo wa kutafsiri maandishi. Maana kusoma hata mtoto wangu ambaye hajaanza Shule anajua.
 
Hii nchi hela nyingi Sana Inaenda kwenye miundo mbinu hasa barabara Kwa Gharama za ufukara wa wananchi...... Kuna jamaa angu engineer huwa namwambia msipopiga hela utawala huu, utawala mwingine ukija mtalia na kusaga meno
And this is big shit maana kuna vipaombele vya kijinga ikiwemo mastendi Kila Mji wanashindana kujenga ya gharama.

Wakati baada ya watoto kufaulu nilialikwa shule ya jirani kwetu watoto 300 wamechaguliwa sekondari huku hakuna madawati wala vyumba wakawa wanatuambia Kila mzazi aje na dawati au 50,000 ,limu,10,000 ya ujenzi,pesa ya chakula,pesa ya walimu na msako utaanza siku chache zijazo

Hii ndio elimu bure ya Magu anaejenga Chato na miradi mingi ya sifa nchi nzima wakati Hali ya kipato ni ngumu,tena nimeona bora Dar wafanyabiashara wadogo hawafuatiliwi kama mikoani japo wanapata vipato vya angalau kuliko huku mikoani
 
Utawala gani ambao hautajenga miundombinu?
Ni vipaumbele Tu mkuu, utawala huu Zaid ya 75 % ya bajeti inaenda kwenye miundo mbinu , hela inamwagwa Sana kule boss.... Mwingine akija unaweza kuta anaegemea Sana kwenye Afya au Elimu ....
 
Alafu akifika Balozi wa nchi yangu nimeshafika na mimi. Maana anainawakilisha na Taarifa analeta.
Nyie jamaa mnauliza maswali yasiyo na ilimu kabisa.
"Eti umeshafika ulaya?" Hahahahah

Hata maswali wanatakiwa kuuliza RAIA wa north Korea ambaye nchi nzima internet cafe tu achilia mbali smartphone kuingia hadi ufanyiwe vetting na tiss wao kama unakidhi Viwango wa kuangalia mambo ya ulaya. Sio mimi
 
Wqnapigaje Mkuu. Maana naona kila mfanyakazi anahofu ya kukamatwa. Kila mtu anamuona mwenzake kama shushushu na informer wa Mkuu. Inabidi uwe na akili nyingi katika kupiga huko usimshike Mkono kipofu ukashtukiwa....
Zimesukwa Dar na Dom tuu huku mikoani ni hola huwezi amini Hadi leo hii kuna mikoa haijaunganishwa na lami mfano Kigoma na majirani zake wote, Katavi na majirani zake wote, Rukwa na Katavi, Tabora 2, Mbeya na Tabora/Singida, Ruvuma na Morogoro, Njombe na Morogoro,nk nk sasa nyie mlioko Dar na Dom ndio mnadhani Kila sehemu iko hivyo
 
Zimesukwa Dar na Dom tuu huku mikoani ni hola huwezi amini Hadi leo hii kuna mikoa haijaunganishwa na lami mfano Kigoma na majirani zake wote,Katavi na majirani zake wote,Rukwa na Katavi,Tabora 2 ,Mbeya na Tabora/Singida,Ruvuma na Morogoro,Njombe na Morogoro,nk nk sasa nyie mlioko Dar na Dom ndio mnadhani Kila sehemu iko hivyo
Labda hii ya DSM ni pilot project, ikifanikiwa mtaletewa interchange hadi huko masadukilo lupondya na legangabilili
 
And this is big shit maana kuna vipaombele vya kijinga ikiwemo mastendi Kila Mji wanashindana kujenga ya gharama...
Jamaa anafeli Sana kubalance mambo , Kwenye Afya ni terrible kabisa , watu wanakufa kama uyoga aisee , Corona nayo ni hatar tupu af mwamba kakimbia DSM anajua Corona itamkaba.

Kwenye Elimu nako ni taabani , shemeji yangu anafundisha sekondary moja hapa DSM , wanafunzi 900 darasa moja , mwalimu wa Physics mmoja , na kuna lundo la walimu mtaani aisee , still anamwaga tillion of money kwenye miundo mbinu ambayo kimsingi sio necessary saana.

Na bado pesa haitoshi anarudiwa mwannchi kukamuliwa kupitia tozo nyingi nyingi , na bodi ya mkopo nao wanakurundikia deni ili mradi miradi ikamilike si ajabu mtu akajiongezea mihula ya utawala ....

Wananchi wanapitia taabu Sana
 
Umekuja lini mjini? Unasifia mpka mlimani city dah
Mkuu nilileta ng'ombe mnadani, kwa niaba ya ukoo ikababidi nikague miradi ya maendeleo ya jiji letu hili ka kijivuni.

kwa kweli Kiu ya kwenda ulaya na kuuza sura kwenye Majengo imekata. Nikienda nafanya ishu zangu tu na kurudi faster Picha ntapigia huku huku posta hahahha
 
Tulizoea zamani mtu akienda Ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania.

Jana baada ya miezi kama tisw hivi kukaa upande mmoja wa jiji LA DSM bila kuzunguka niliachwa mdomo wazi.

1: Kuna Majengo Mapya makubwa mazuri hatari. Mfano mitaa ya Makumbusho Victoria yaani hadi unatabasamu tu kwa jinsi miundombinu na design zilivyosambazwa pale. Lililoniacha hoi ni jengo moja hivi maeneo ya palm beach. Ile kitu ni matata sana. What a design!!!!

2: Kale kadaraja ka masaki baharini mwanzoni nilidhani ni vile kama vya Miti chini kwa chini Jana nimeshangaa kunastructure za hatari wanazimount pale kumbe ni kitu hatari Sana.

3: Nikapita Ubungo Simu2000 na stand ya mabasi napo kuna road zimesukwa pale ndani ya muda mfupi utapenda. Naona wanajiandaa kuweka taa za barabarani ukiongezea Interchange. Alafu ukichungulia kuelekea Mlimani city aisee pako Bomba sana.


4: Nikachungulia CCBRT, hadi nikadhani nimekosea njia. Kuna zinga la hospitali. Yaani Majengo mengi Mapya mageti mengi ya kuingilia hawajaifungua. Hadi nikajiuliza kwa nini hata Mloganzila ilijengwa. Maana kile nilichokiona Wenda hata Muhimbili inaweza isifue dafu licha ya Eneo kuwa dogo.

Nikapita Mbagala, kuna structure flani barabarani zinainuliwa pale nadhani ni kwa ajili ya mwendokasi au sijui ni daraja basi napo patakuwa poa sana.

Kimsingi nina mpango wa kwenda nchi kadhaa Ulaya lakini nikifika nitapiga Picha kwenye mabarafu tu ila Majengo kama background sidhani maana hicho nilichokiona Jana hata Ulaya hakuna.

Msema Kweli ni mapenzi wa Mungu. Natamani kupata Picha ya aerial views current ya maeneo mengi ya jiji.
Ulaya ya buza Kwa mpalange labda
 
Jamaa anafeli Sana kubalance mambo , Kwenye Afya ni terrible kabisa , watu wanakufa kama uyoga aisee , Corona nayo ni hatar tupu af mwamba kakimbia DSM anajua Corona itamkaba .... Kwenye Elimu nako ni taabani , shemeji yangu anafundisha sekondary moja hapa DSM , wanafunzi 900 darasa moja , mwalimu wa Physics mmoja , na kuna lundo la walimu mtaani aisee , still anamwaga tillion of money kwenye miundo mbinu ambayo kimsingi sio necessary saana....
Na bado pesa haitoshi anarudiwa mwannchi kukamuliwa kupitia tozo nyingi nyingi , na bodi ya mkopo nao wanakurundikia deni ili mradi miradi ikamilike si ajabu mtu akajiongezea mihula ya utawala ....

Wananchi wanapitia taabu Sana
Hakuna corona wewe acha uchawi.
Kama IPO kweli, mbona iliisha kwa matamko na karantini tukafunga na hakuna ilichofanya.

Yangu siku hiyo Mimi naamini corona ni hofu sio kirusi wala plasmodia.

Mkuu ukiwaendkeza wazungu kila kitu utaishi maisha ya tabu sana
 
Ulaya ya buza Kwa mpalange labda
Ulaya pa kawaida sana. Tatizo wengi bado hawajapona uongo waliolishwa na wakina Carl peters na maazimio ya kikao cha Berlin miaka ya 1800. Ukicut na kupaste Eneo kama Makumbusho pale ukalipaste kijiji flani uingereza wote watakuja kupiga Picha za kurusha ista.
 
Kimtindo lakini sio sanaaView attachment 1681676View attachment 1681675
image_64ccd5ea-b2f9-4ad0-b958-97b3327d8f4220190320_225551.jpg
View attachment 1681677
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom