Wakuu hapa sheria inasemaje? Nani yuko sahihi?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,276
14,512
Jamaa alikuwa na shamba pori.
Serikali ikalitifaisha kwa sababu ya kutoendelezwa muda mrefu.

Wakauziwa wengine kama viwanja na wana hati za serikali za mitaa.
Miaka mingi imepita, jamaa kaibuka anadai kashinda kesi na wanunuzi wote ni wavamizi.

Kwa Harakaharaka nani yuko sahihi.
Mwenye shamba baada ya kudai kushinda kesi?

Serikali baada ya kutaifisha shamba pori?

Wananchi walionunua maeneo kihalali kupitia serikali za mitaa kwa uhakika kuwa eneo hilo limetaifishwa?

Ikitokea wamebomolewa, wahahaki kuishtaki serikali ya mitaa iwalipe fidia kwa kukubali kuwauzia eneo ambalo wanajua lina migogoro?
 
Wanasheria mjee huku. Mimi naona kama kulikuwa na kesi mahakamani, na kama mahakama iliweka zuio la shughuri yoyote kwenye pori, mmiliki wa pori kashinda.
 
Anadai tu kashinda kesi bila uthibitisho .Ameshinda kesi mahakama ipi.Kama ilichukuliwa na serikali kwa abandonment anashinda vipi kesi.Hiyo kesi ilikuwa kati yake na nani maana hapo ni yeye dhidi ya serikali na siyo hao waliogawiwa.Huyo mdau mpaka hapo hana mamlaka na hilo eneo
 
balibabambonahi
na kisheria rais ana mamlaka kufuta umiliki wa ardhi yoyote iwe shamba au Kiwanja, imetokea hata kwa kina Sumaye na wengineo, Kwaiyo kama umiliki ulifutwa na Serikal then wananchi wakagaiwa, hapo wananchi wana haki ya ilo eneo
 
Mina cute
Tatizo linaweza kuwa jinsi alivyonyang'anywa.
Huenda serikali za mitaa hazikuwa na mamlaka hiyo. Au Kuna taratibu zilikiukwa katika kumnyang'anya. Kimsingi alitakiwa kumshtaki aliyemnyang'anya yaani serikali ya mitaa
 
Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999 (r.e 2002) imeweka taratibu za kubatilisha hati za kimila.

Kama utaratibu haukufuatwa, bado ardhi ni ya jamaa aliyeshitaki. Huwezi kununua kitu kisicho mali halali ya mtu. Itabidi wavunje tu maeneo yao.
 
Anadai tu kashinda kesi bila uthibitisho .Ameshinda kesi mahakama ipi.Kama ilichukuliwa na serikali kwa abandonment anashinda vipi kesi.Hiyo kesi ilikuwa kati yake na nani maana hapo ni yeye dhidi ya serikali na siyo hao waliogawiwa.Huyo mdau mpaka hapo hana mamlaka na hilo eneo
Yeye aliwashtaki viongozi wawili waliohusika katika zoezi hilo miaka hiyo.
Sasa ndio maana anaambiwa kama kawashinda akachukue mali zao maana hilo liligawiwa na serikali sio hao watu.
Ila anatanua mtaani na wanasheria na kudai atabomoa nyumba zote ndani ya siku kama kumi zijazo baada ya kubandika matangazo.

Kesi yenyewe anadai alishinda miaka 10 iliyopita, ila alikuwa hana pesa ya kubomolea.
 
Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999 (r.e 2002) imeweka taratibu za kubatilisha hati za kimila.

Kama utaratibu haukufuatwa, bado ardhi ni ya jamaa aliyeshitaki. Huwezi kununua kitu kisicho mali halali ya mtu. Itabidi wavunje tu maeneo yao.
maelezo mazuri.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom