Wakuu CUF wameanza kwa mguu mbaya Igunga, kila siku wao kuiga tu! No creativity? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu CUF wameanza kwa mguu mbaya Igunga, kila siku wao kuiga tu! No creativity?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chief Isike, Aug 14, 2011.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu mpaka jioni hii nilikuwa najua kuwa CUF wamemtangaza mgombea wao wa ubunge wao wa Igunga, lakini usiku huu wakati natazama taarifa ya habari ya ITV, nimekuwa shocked nilivyomuona kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu Naibu Katibu Mkuu wao (Bara), Julius Mtatiro (anatumia mishipa ya mwili mzima huyo kutamka kila neno du), akisema watamuuza mgombea wao huyo kwa kutumia Operesheni Changua Mahona! Nauliza hivi ni lazima kila kitu waige? Maana CHADEMA walitangulia kule kujenga chama chao kwa Operesheni Chukua Igunga (OCI), ambayo baadae hapa tulishauri iitwe Operesheni Komboa Igunga (OKI).

  Ilipoanzishwa Operesheni Sangara, CUF wakaamua nao kujenga chama chao katika mikoa miwili mitatu (wakachemkia njiani) kwa Operesheni Zinduka! Tehe tehe tehe. CCM wao ndiyo kabisa waliishia tu kutangaza kuwa nao watapita mikoani na Operesheni nini sijui vile (sikumbuki jina exactly mnaweza kunisaidia). Kuna madai kuwa katika moja ya mikutano mapema mwaka huu huko mikoa ya kusini (nafikiri Jimbo la Tandahimba), Mtatiro alikuwa akiwaambia wananchi waliohudhuria mikutano aliyohutubia waseme 'pipoooooooos....' halafu pia akawaambia waitikie 'uuuuuuuuwwiii' kila aliposema 'Kidumu Cha Mapinduzi'. Nafikiri mnajua hizo slogan ni za akina nani! Jamani CUF has got to reogarnize when it comes to catching up and attracting people's attention, propaganda na vitu vingine! They mostly lack creativity brothers
   
Loading...