Wakuu "changamoto ya kupumua" iliishia wapi?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,544
15,216
changamoto ya kupumua ilitafuna watu kwa kasi.

Bila, dawa wala kinga sioni tena amsha amsha tangu mkuu wetu alipoyarudia mavumbi.

Hata ile trend ya viongozi wetu kupukutika kwa mfuatano nayo imekoma mara tu mkuu kulala mavumbini.

Je Mungu katuokoa?
Je Zilikuwa njama tu za kututishia wakuu wetu?
Je ilikuwa ni vuguvugu la kuhalalisha tuchanjwe kama mifugo?

Je
Je
Je

Najiuliza, nikiwa nimekaa dukani kwa jirani hapa kijiwe changu cha kupatia matangazo ya vifo vya magonjwa ya milipuko.
 
Niliwahi kufundishwa kanisani kuwa Mungu anapotaka kukuonya anaweza asikuguse moja kwa moja akaanzia mbali na hutumia watu ili kukwambia kuwa hapendezwi na unavyoishi, ila ukiendelea kushupaza shingo mwisho wake huwa ni mbaya
 
Kama kweli ni binadamu katengeneza covid 19 akatwe shingo na azamishwe katikati ya bahari ili afutike katika uso wa dunia .
 
Mkuu unauliza changamoto ya upumuaji mbona bado ipo.
Hujaona video ya mheshimiwa rais Samia jana pale hospitali ya Mwananyamala-Dar.

Alipoonesha wodi ya wagonjwa wa upumuaji, mpaka akasikika anasema nyie tokeni kuwaambia timu aliongozana nayo. Wakatoka bila kuingia wodini.
 
changamoto ya kupumua ilitafuna watu kwa kasi.

Bila, dawa wala kinga sioni tena amsha amsha tangu mkuu wetu alipoyarudia mavumbi.

Hata ile trend ya viongozi wetu kupukutika kwa mfuatano nayo imekoma mara tu mkuu kulala mavumbini.

Je Mungu katuokoa?
Je Zilikuwa njama tu za kututishia wakuu wetu?
Je ilikuwa ni vuguvugu la kuhalalisha tuchanjwe kama mifugo?

Je
Je
Je

Najiuliza, nikiwa nimekaa dukani kwa jirani hapa kijiwe changu cha kupatia matangazo ya vifo vya magonjwa ya milipuko.
Sawa Mkuu, tusijeona humu Jf unatoa ushuhuda!!
 
Back
Top Bottom