Wakuu, Barua Yangu Kwa WABUNGE Wetu HIII HAPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakuu, Barua Yangu Kwa WABUNGE Wetu HIII HAPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Feb 12, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JOSEPHAT SIMON SANDA
  S.L.P 13914 DAR ES SALAAM
  SIMU YA MKONONI: 0659 281964 BARUA PEPE: josephatsanda@yahoo.com

  8 FEBRUARI 2011

  KUMB: JSS/BLT/0802/03

  WAHESHIMIWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  S.L.P 941
  DODOMA
  TANZANIA

  Waheshimiwa Wabunge,

  YAH: NAMNA YA KUIBADILISHA NA KUIENDELEZA TANZANIA KUPITIA WABUNGE, WANANCHI NA MIFUKO YA MAENDELEO YA MAJIMBO

  Waheshimiwa Wabunge, naomba kuchukua fursa hii kujitambulisha. Mimi naitwa Josephat Simon Sanda. Ni Mtanzania na ninaishi mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo.
  Waheshimiwa Wabunge, kutokana na nafasi mliyonayo katika nchi yetu na umuhimu wenu katika kuonyesha njia ya maendeleo kwa wananchi mnaotuwakilisha, naomba mniruhusu kuwasilisha mapendekezo yafuatayo kwenu ili utekelezaji wake uweze kuisaidia kiuchumi nchi yetu pamoja na sisi Watanzania kwa ujumla wetu na kufuta kabisa umasikini katika nchi yetu ndani ya kipindi kisichozidi miaka 20 toka sasa.
  PENDEKEZO KUU
  Inapendekezwa kuwa Wabunge wetu muanzishe Mfuko mkubwa wa uwekezaji ambao unapendekezwa uitwe MAENDELEO FUND (MF) au TANZANIA NATIONAL INVESTMENT FUND (TNIF). Mfuko huu wa uwekezaji uwe kama Umoja Fund unaosimamiwa na kuendeshwa na Unit Trust of Tanzania. Mfuko huu unapendekezwa pia uwe na nguvu za kisheria utakaouwezesha kuanzisha kampuni na shughuli mbalimbali za uwekezaji ndani na nje ya nchi yetu. Fedha za mtaji za Mfuko huu inapendekezwa zitokane na vyanzo vifuatavyo:
  1. Kila mwezi kila Mbunge anunue vipande vya Mfuko vyenye thamani ya angalau shilingi milioni mbili.
  2. Kila Mfuko wa Jimbo uwekeze angalau shilingi milioni tano kila mwezi kwa kununua vipande vya Mfuko huu unaopendekezwa.
  3. Kila mwananchi awekeze angalau shilingi 300 kila wiki kwa kila namba ya simu yake ya mkononi katika Mfuko huu kwa kununua vipande vya Mfuko. Wananchi wawekeze katika Mfuko huu kwa kununua vipande vya Mfuko kwa kulipia kupitia simu zao za mkononi kwa kutuma ujumbe kwenda namba maalum.
  4. Serikali kuu iwekeze angalau shilingi bilioni 200 kila mwaka kwa kununua vipande vya Mfuko na kisha kuanza kuviuza kwa Watanzania kwa bei nafuu baada ya miaka mitano.
  5. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iwekeze angalau shilingi bilioni 150 kwa pamoja kila mwaka kwa kununua vipande vya Mfuko huu.
  Iwapo vyanzo hivi vitatumiwa ipasavyo, kila mwaka Mfuko unaopendekezwa utakuwa na uhakika wa kukusanya mtaji usiopungua shilingi bilioni 700.

  MAENEO YA UWEKEZAJI YANAYOPENDEKEZWA
  ENEO LA KWANZA
  Kupitia Mfuko huu, inapendekezwa Wabunge wetu mtuongoze katika kuanzisha mashamba makubwa ya mfano (hasa kwa njia ya umwagiliaji) ya mazao mbalimbali na ufugaji wa kisasa, katika sehemu mbalimbali hapa nchini pamoja na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vya kusindika na kuyaongezea thamani mazao mbalimbali ya wakulima wetu. Viwanda hivi ndiyo vitakuwa soko kuu na la uhakika la mazao toka kwa wakulima wetu. Kwa upande wa ukulima wa mashamba makubwa ya mfano na ya kisasa, baadhi ya mazao yanayopendekezwa ni Miti mbalimbali ya Mbao, Mahindi, Mpunga, Alizeti, Karanga, Kahawa, Migomba, Chai, Cocoa, Pamba, Pareto, Karafuu, Maharage, Kunde, Maua, Mtama, Tangawizi, Ufuta, Korosho, Michikichi, Mihogo na Dengu. Kwa upande ya miti ya mbao lengo linapendekezwa liwe ni kupanda angalau ekari 2,500,000 kila mwaka kwa angalau miaka 15 mfululizo. Iwapo mpango huu wa kupanda ekari milioni 2.5 kila mwaka za miti ya mbao utafanikiwa, baada ya miaka 10 mpaka 12, kwa bei za sasa, Mfuko utakuwa na uhakika wa kupata faida isiyopungua shilingi bilioni 65,000 kila mwaka. Ukulima wa mashamba haya makubwa ya miti ya mbao, ufugaji wa kisasa na mazao mbalimbali inapendekezwa ufanyike kwa ushirikiano wa karibu na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Halmashauri zetu, MVIWATA na Vituo vya Utafiti wa Kilimo, Mifugo na Misitu vilivyoko hapa nchini. Kwa upande wa viwanda, ni muhimu sana kutosahau kuanzisha viwanda vya kusindika matunda, kutengeneza mafuta ya Mawese na Alizeti pia kiwanda kikubwa kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya kuzalisha umeme utokanao na Nguvu za Jua. Kwa upande wa mashamba ya miti tusisahau pia kupanda ekari za kutosha za miti ya Mipingo.
  ENEO LA PILI
  Mfuko uanzishe utaratibu wa kununua angalau trekta 5,000 kila mwaka kwa ajili ya kulima mashamba yake makubwa na pia kusaidia kuwalimia mashamba yao wakulima wetu wasio na trekta kwa gharama nafuu.
  ENEO LA TATU
  Kwa kufuata ushauri wa Wataalam wetu, Mfuko uanzishe shughuli za uvuvi kwa kiwango cha kimataifa katika Bahari yetu na Maziwa yetu.
  ENEO LA NNE
  Ili kuhakikisha kuwa Watanzania tunapatiwa kila wakati elimu bora ya Uwekezaji, Uzalishaji Mali na Ujasiriamali kwa gharama ndogo, inapendekezwa Mfuko kwa kushirikiana na taasisi zetu za elimu, vituo vya redio na televisheni, uanzishe na kutoa mafunzo maalum na ya kudumu ya Uwekezaji, Uzalishaji Mali na Ujasiriamali kwa angalau saa tatu kila siku kwa njia ya Redio na Televisheni. Pia Mfuko, kwa kushirikiana na vyuo vyetu vikuu, wizara husika na TBC na kwa kutumia miundombinu yake, uanzishe Channel ya Elimu ambayo itarusha matangazo yake kwa saa 24 kila siku.
  ENEO LA TANO
  Ili kuhakikisha kuwa huduma za kibenki na mikopo zinapatikana mpaka ngazi ya kijiji bila tatizo, Mfuko ushirikiane na halmashauri zetu kuanzisha benki za kijamii kwa kuwekeza angalau shilingi milioni 300 kila mwaka katika kila benki jamii kwa miaka mitano mfululizo.
  ENEO LA SITA
  Ili kuhakikisha kuwa Watanzania tunapata maji yaliyo safi na salama, Mfuko uwekeze angalau shilingi bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kuchimba visima vya maji safi na salama hasa maeneo ya vijijini.
  ENEO LA SABA
  Mfuko uwe na utaratibu wa kununua sehemu kubwa ya Hisa za Kampuni za Simu, Nishati na Madini zilizowekeza na zitakazowekeza hapa nchini.
  ENEO LA NANE
  Kwa kuwatumia wataalam wa kitanzania Mfuko umiliki maeneo makubwa mbalimbali yaliyo na madini na gasi hapa nchini na kuanzisha uchimbaji wake.
  ENEO LA TISA
  Mfuko umiliki angalau ekari 200,000 katika maeneo mbalimbali ya vijijini kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za bweni za kidato cha tano na sita hasa kwa masomo ya sayansi. Shule hizi kwa kuwa zitakuwa na vifaa vyote muhimu vya mawasiliano na miundombinu inayohitajika, zinaweza pia kutumika kama sehemu ya kutolea mafunzo ya elimu ya chuo kikuu kuanzia muda wa mchana mpaka usiku kwa kushirikiana na vyuo vyetu vikuu.
  Waheshimiwa Wabunge, ni matumaini yangu kuwa mtapata wasaa wa kuyatafakari yale yaliyopendekezwa katika barua hii na kisha kukubaliana kwa pamoja nini kifanyike kwa faida ya nchi yetu na kwa faida yetu sisi sote kama Watanzania.
  Kama Kampuni za Madini, Nishati na Simu za Mkononi zimekopa na kufanikiwa sana hapa nchini, hakuna sababu itakayoizuia MAENDELEO FUND/TANZANIA NATIONAL INVESTMENT FUND isifanikiwe katika lengo lake kuu la kufuta umasikini hapa nchini.
  Waheshimiwa wabunge, nawatakia mafanikio makubwa katika kutimiza wajibu wenu wa kutuwakilisha sisi Watanzania.

  Wenu katika ujenzi wa taifa


  Josephat Simon Sanda
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mawazo mazuri, ila nina wasiwasi kama hii wanaitaka maana hakuna maneno kama Dowans, katiba, Arusha n.k sidhani kama itapokelewa.
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! yangu macho
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ... bora uende kabisa pale mjengoni ... omba kuwa mgeni wa bunge halafu wasilisha ..... pia mwaka 2015 kachukue fomu ya kugombea ubunge mapemaa
   
 5. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante. Kugombea hapana, ila tuombe MUNGU wayapokee na kuyafanyia kazi.
   
 6. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante Mjepu. Nilipeleka mimi mwenye nakala 357 kwa Wabunge wote siku ya Alhamisi asubuhi tarehe 10/Februari/2011 pale Mjengoni. Natumaini kufikia Jumatatu Mchana Kila MBUNGE atakuwa amepewa nakala yake. Tuombe MUNGU kusiwe na KIKWAZO CHOCHOTE KILE KATIKA KUWAPATIA WABUNGE WETU BARUA HII ILI KILA MMOJA WAO AISOME KWA UKAMILIFU WAKE.
   
 7. F

  FredKavishe Verified User

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu wazo zuri sana ngoja tusikie kutoka kwa wabunge wetu
   
 8. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli
   
 9. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wish ningekua rais watu kma nyie ningewapa kuongoza NDC au TIC nione kma mnaweza ku put in practice mawazo yenu mkiweza nawambia mfundishe wengine kma 1000 njia izo izo halaf tunakua kma tiger economy kwa maendeleo.

  Yan mfn ni wale walio nunua manchester city,nao si kma hv hv?ni vituo vya uwekezaji vya izo nchi,saiv wanawekeza mpk kwenye timu za mpira.

  Kaka big up mawazo chanya sana haya ila watekelezaji wana pamba masikioni,bt tusife moyo,big up
   
 10. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante Mkuu--Bahati nzuri sioni namna ambavyo yatakuwepeka.
   
 11. p

  princekerry Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa nami naunga mkono hoja 100%
   
 12. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cha ajabu ni kuwa nimeongea na Bwana John Joel na amenieleza kuwa watawagawia wabunge hizo barua Jumanne ya wiki ijayo (15/02/2011) wakati wao wamekuwa nazo toka tarehe 10/02/2011 asubuhi. Kazi ipo nchi hii.
   
 13. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waziri wa Elimu NA MAFUNZO YA UFUNDI Nimempigia Sana SIMU YAKE YA MKONONI Jana na Leo Asubuhi.
   
 14. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuendelee kuichambua Barua Ytu kwa Wabunge.
   
 15. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2013
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Habari za siku. Ni ngumu kuamini. taarifa nilizonazo ni kuwa mpaka leo hii Wabunge wetu bado hawajapewa hiyo barua yangu.
   
 16. C

  CHIGANGA JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2013
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaha,Wao hata makabrasha Yao tu Hawasomi,ITAKUWA hiyo document ,hebi Niibox NAMBA yako kaka,Mimi nikupigie tufanye mambo
   
 17. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2013
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mfuko mtaji wake bilioni 700 , unataka wanunue matrekta , wanunue zana za uvuvi, wanunue ardhi , wafanya kila kitu return yake ni kipindi cha miaka mingapi, wananchi ambao wanawekeza watanufaikaje na hisa zao, ............huu mfuko usimamiwe na nani bunge ama serikali , mgawanyo wa majukmu baina ya mihimili itakuwaje ? Vipi kuhusu majimbo ya mjini watanufaika vipi maana hawana mashamba, sio wavuvi nk sasa wao kwanini wawekeze fedha zao?
   
 18. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2013
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fedha si tatizo. Tunazo za kutosha.
   
Loading...