Wakuu, alikuwa ni Mungu,Ibirisi,Bahati,nyota au ni kawaida?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,771
15,835
Kuna kipindi ilikuwa kila nikipanga jambo Kubwa na gumu lisilowezekana mwisho linatoboa. Ila najua baadaye likiwa limepita.

Nilipanga muda wa kupata KAZI bila kujuana wala kumpigia mtu MAGOTI. Kwa mateso makali lakini ilipatikana muda uleule.

Nilipanga kuoa nikiwa sijui hata pesa ya mahali na kulisha familia itatokea wapi maana nilikuwa na madeni kila Kona. Lkn siku na tarehe ileile nilioa na had I nikabaki mkononi na 1.8M kama free cash baada ya harusi.

Nilipanga kumiliki Gari siku na tarehe hiyohiyo nikawa na Garijapo baadaye kidogo nikaipiga chini.

Nilipanga kujenga nikiwa sins Kiwanja lkn muda uleule niliopanga nikawa na mjengo japo wa kuungaunga lkn location watu wanashangaa nilipataje.

Niliwahi kupata changamoto ya afya nikiwa na watoto, mke bila Bima wala kszi mfukoni na 2000, na natakiwa niwe na 1.5M ili nitoke hospital na siku ya kutoka ilipofika nilitoka na kukaa miaka 2 bila KAZI ya ajira lakn tulisonga japo kwa kuunga sana. Nikifikiri sioni vzr nilipitaje?

Huu ilikuwa msimu flani tu niliupitia sijui kipindi cha nyuma kidogo.
 
Ukisoma biblia utajua kweny maisha ya Binadamu kuna miaka ya neema na miaka ya laana

Yawezekana ilikua ni miaka yko ya neema

Ila kuna kitu watu wanashindwa kutofautisha Time and season!

Ila kwa kipindi ulicho pitia ni season!!

Kuna rafiki yngu mmoja baba yke alikua anatupa story ya kipindi cha ujana wake anasema chochote alicho muomba Mungu kwa wakati uo Mungu alikua anampa sawa sawa na mahitaji yke.

Ila inavoonekana (alizingua kimtimdo) kutoboa life.

Sasa akatuhasa kipindi hiko cha neema ukikipata don't play!!

Fanya maamuzi sahihi kabisa usije ukajutia baadae!.
 
Endelea kupanga jambo na itakuwa hivyo....
kuna watu Mungu alishawaandikia ukipanga jambo lako tiki na hutokwama....
 
thats what we call"THE POWER WITHIN"

amini katika unachowaza na kupanga utaona maajabu.
 
Back
Top Bottom