Wakurugenzi watano MSD waenguliwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,792
4,444
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Wizara hiyo imewaondoa kwenye nafasi zao wakurugenzi watano wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) kutokana na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa.

Waziri Ummy amesema hayo jana Jumatatu Mei 16, 2022 jijini Dodoma wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, baada ya kuchangiwa na wabunge mbalimbali.

Amesema kuwa “Pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kubadilisha uongozi wa juu wa MSD na kumteua mwenyekiti mpya wa bodi, hatua hiyo ilikuwa haitoshi kutokana na malalamiko mengi yaliyokuwa yakitolewa.

Waziri Ummy ametaja wakurugenzi wanaoondolewa kuwa ni pamoja na “Mkurugenzi wa Fedha anaondoka MSD, Mkurugenzi wa manunuzi MSD, Mkurugenzi wa Logistics MSD, Mkurugenzi wa Sheria MSD na Mkurugenzi wa Utawala wa MSD anaondoka.” amesema Waziri Ummy

Mei 9 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye ofisi za MSD aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwashughulikia watumishi wote watakaoonekana wamehusika katika ubadhirifu wa manunuzi na fedha katika Bohari ya Dawa (MSD).

Takukuru ambao walikuwa tayari wameweka kambi katika taasisi hiyo, walikuwa wanafanya ukaguzi katika yale yaliyoonekana katika ripoti ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere pamoja na maeneo mengine ikiwemo fedha za Uviko-19.

Pia soma:
- Maofisa watano wa TMDA waliokuwa na tuhuma ya kuhujumu uchumi waachiwa huru

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo wa mkurugenzi hr tulipata malalamiko yake mengi alikuwa hana usaidiz kwa taasisi taasisi alipofika pale akafurahia fursa za pale.frank Nkone ni meneja aliyewahipachikwa ukurugenzi wa manunuzi alikiuka Sana taratibu kipindi chake Hana sifa yeye ni mwalimu na hr ni kafisadi na kijeuri mno, siku moja baada ya waziri mkuu kutoa maelekezo wa mwenendo wa ufisadi wao yule bwana Frank na mkurugezi wake wamejipatia safari ya ulaya wiki nzima yaani sikio la kufa hawa MAMENEJA wa mcd. yaani Kikubwa MAMENEJA wa msd wapowapo tu hawana hadhi Wala ubunifu Wala weledi, wataendelea kumkwamisha hata huyo mpya ni mizigo hasa wale wa Kanda ndio hovyo hovyo hawana majawabu kabisa ya huduma kwa wateja, overhaul kubwa iende kule.
 
Kazi nzuri,haya majizi yalifugwa kwa maslahi binafsi ya genge la wazalendo wa Chato..

Ilitakiwa yule boss wao pia apandishwe kizimbani sema tuu wamemstahi sababu ni Mjeshi..
 
Kuna majizi wengine walikuwa hawana hata sifa ila wapo,Safi Sana futilia mbali hao👇

Screenshot_20220517-151810.png
 
Back
Top Bottom