kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
- “Utakuta mtumishi mmoja ni kiongozi wa kikundi kwenye makundi saba ya Whatsapp, kila muda yupo ‘online’ anachangia kwenye kikundi, unajiuliza huyu mtu anafanyakazi saa ngapi?”
“Utakuta mtumishi mmoja ni kiongozi wa kikundi kwenye makundi saba ya Whatsapp, kila muda yupo ‘online’ anachangia kwenye kikundi, unajiuliza huyu mtu anafanyakazi saa ngapi?” alisemai Jafo.
Jafo pia aliwataka wakurugenzi hao kwenda kusimamia watendaji katika maeneo yao ili kuhakikisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki iliyofungwa inafanyakazi na kuleta tija iliyokusudiwa.
“Juzi wakati Waziri Mkuu anafungua mkutano huu aliwasisitiza suala la matumizi ya mashine hizo, sasa nendeni mkahakikishe mifumo hiyo inafanyakazi, mameya na wenyeviti watapata nguvu ya kufanya kazi endapo nyinyi wakurugenzi mtasimamia vizuri maeneo yenu,” alisema na kuongeza:
“Usikubali kuangushwa na mtendaji wako wa chini ukaonekana hufanyi kazi, pangianeni malengo yenu, mkurugenzi mpangie mkuu wa idara, mkuu wa idara ampangie wa chini yako na asiyetekeleza jukumu lake achukuliwe hatua.”
Jafo aliwahimiza viongozi hao kusimamia miradi iliyopo chini ya halmashauri zao na kuwataka mameya na wenyeviti kuhakikisha miradi yoteinasimamiwa vizuri na kuingizia mapato halmashauri bila ya rushwa.
Akizungumzia kuhusu watumishi hewa, Jafo alizitaka halmashauri nchini kuhakikisha fedha zilizolipwa kwa watumishi hewa zinarudi serikalini.
“Ni lazima pesa hizo zirudi serikalini na tayari kuna halmashauri zimeshaanza kurejesha fedha hizo, hivyo inapaswa halmashauri zote zilizobaini watumishi hewa fedha hizo zikatiwe risiti zirudi serikalini,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Alat, Gulam Mukadam, aliwataka wajumbe wa jumuiya hiyo kwenda kuyafanyia kazi yote waliyojifunza na kukubaliana katika mkutano huo kuweka mbele maslahi ya Watanzania wanaowatumikia.
Chanzo: NIPASHE