Wakurugenzi wa Taasisi nyingine mlioteuliwa kabla ya Magufuli kuwa Rais jiandaeni...

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,432
Kwa hiki kilichomtokea Mramba wa Tanesco ni dhahiri kuwa wakurugenzi wakuu walioteuliwa Enzi za kikwete wajiandae kuondolewa nafsi zao. Mchackato wa umeme umeanza mda mrefu na ilikuwa public.

Sheria inayolinda na kuelekeza mchakato huo ipo. Mkurugenzi lazima amepitia bodi ya wakurugenzi kuanzisha mchakato.Bodi ya wakurugenzi wakiisharidhia ndo Tanseco wanapeleka EWURA.

Hoja ya kupandisha umeme imeanza mda mrefu, je nikwanini serikali kupitia Waziri haikuingia mapema kupinga na kupitia reporti ya TANESCO?? Je wao hawakua nchini na hawakujua juu ya huu mchakato? Sababu zilizotolewa na Waziri na Mh Rais kutengua nafasi ya Mramba hazina mashiko na zinaonyesha walikuwa wanamvizia nakumutafutai sababu fulanifulani ili wamuondoe.

Mie ningemuelewa mh Rais kama angevunja bodi ya Tanesco na kumuondoa Waziri kwa Kushindwa kuintervene mapema, otherwise ni hali ya uonevu na sidhani kwa wasomi na wanaoelewa mambo watakubaliana na hili.

Kama anamuondoa kwa sababu ya kuingiz mkataba na symbion mwezi Dec 2015 kwa ajli ya kuzalisha umeme kwa miaka 20 wakati hata Mh rais alikuwa hajaunda Baraza la Mawaziri hapo aseme na wote tutakubali.

Kutokana na niliyeleza hapo juu ni vizuri wakurugenzi wakuu wa Mashirika makubwa nchini kama PPF,LPF,NHC wajiandae kuondoka.. wasidhani wako smart ila bado kuna kakitu kanatafutwa.

Mie ni mshabiki wa mh Magufuri na serikali yake na nimekuwa namtetea sana lakini kwa hili la Tanesco lazima lielezwe vizuri ili watendaji wawe na maamuzi la sivyo huenda utendaji na Ubunifu ukawa ovyo sana.
 
Hilo lipo kichwani kwake kama wale wote waliokuwa wakat wa jakay ni wapiga dili hata hao mawaziri walioteuliwa wengi ni sababu ya chama lkn jamaa hawataki perioood
 
Mramba alikuwa anajilipa bonus milioni 60 kila mwaka wakati Shirika linajiendesha kwa hasara!!!
 
Magu anajenga himaya yake yenye watu 100% wanaomuogopa na wapo kwa ajili ya kufanya apendavyo mtukufu bila kuhoji
 
Back
Top Bottom