Wakurugenzi wa mashirika ya umma na idara kazi kuuza sura kwenye maonyesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakurugenzi wa mashirika ya umma na idara kazi kuuza sura kwenye maonyesho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nndondo, Jul 3, 2011.

 1. n

  nndondo JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hebu jamani niwaulize, leo nimeona watu wazima na akili zao wengine wakijiita wasomi wenye phd akiwemo mkurugenzi wa EPZ na Twiga bancorp wanamdanganya nani kwamba kuwepo sabasaba kuna tija kwenye kampuni zao. Hivi wanaweza kutuambia wame recruit wawekezaji wangapi huko sabasaba kuwekeza EPZ kama si ufisadi wa pesa za umma, hivi hizi organization haziongozwi na strategic plans, bali hisia za cheap popularity za viongozi wao, kujikomba kwa JK, viongozi wenyewe hoi wako so cheap eti the whole top government, pinda, bilali Jakaya atakwenda tarehe 6 kufanya nini? hivi hawa wanalaana gani jamani? hivi serikali imejaa huko yenyewe inafanya biashara gani? hivi haya maonyesho sio ya makampuni ya biasharara? after all wametoka wiki iliyopita mnazo mmoja kwenye wiki ya utumishi my foot" wako sabasaba wakitoka hapa wanaelekea morogoro kwenye nane nani ni matumizi tu ya kodi zetu bila sababu. *priority kwao ni kuuza sura, hivi kwenye TV asingeweza kuwa msemaji mwingine yoyote kama afisa habari, PRO hawapo ni lazima wakurugenzi wakuu hawa na sura zao mbaya ndio wajae kwenye TV zetu? no wonder hakuna umeme, njaa imetapakaa kila mahali , hao the so called washauri na watendaji wa kikwete hawana tofauti na yeye mwenyewe kwa ukilaza, hata watendaji wao wamechoka wanalalamika hawana tu la kufanya maskini, ma afisa wazima na visomo vyao, hawapewi nafasi ya kufanya kazi wana parediwa huko kurasini kukutana na vitoto vya shule ya msingi na wakina mama wanaoenda kununua vyombo vya plastic, maana nzima ya trade fair imeuawa, imegeuzwa ni ufisadi mwingine wa allowances na suti za bei mbaya na cha ajabu hakuna kwenye serikali hii ya vilaza anaekemea hilo. Kazi kupena vyeti vya ushindi wa mapambo na matarumbeti which have nothing nothing to do with their line functions. Jamani saa ya ukombozi ni sasa hebu tusaidieni kuiondoa serikali hii madarakani, 2015 is too far. Yaani inakuaje nchi nzima hii hakuna mwenye uzalendo, mwenye akili timamu, mwenye uchungu, mwenye haya? kweli kweli kweli huku kuuza sura ndio ufanisi? tumewageuza wasomi wetu kuwa vituko visanamu vya kushinda kwenye mabanda ya maonyesho kwa posho za chips za kuku za lunch? hebu angalieni hivyo vi fulana cheap product za china low grade wanazovalishwa ili mradi tu ten percent za procurement ziende, nchi ya chenji za rada, Jamani Jamani help me nakufa kwa hasira ndugu zangu, hawa watu tukizidi kuwaachia watatula kama samaki manake mbele wameshatumaliza karibu watatugeuza
   
 2. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sasa kiongozi mkuu hakai ofisini anauza sura nje, wao wafanyaje!
   
 3. Researcher

  Researcher Senior Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naona hapa kuna hoja ya msingi sana.
  Ni kweli kwamba taasisi yoyote ina wajibu wa kujitangaza...lakini kujitangaza lazima kuwe na malengo yake na katika namna itakayoongeza tija.

  Jiulize kuhusu gharama za ushiriki. Chukulia CARMATEC ambao wanatoka mkoani, anza na posho ya timu nzima, kisha gharama ya kusafirisha vile wanavyoonyesha (matrekta, power tiller...) ada za ushiriki n.k

  Halafu unajiuliza kwamba wanaokwenda sabasaba, nane nane au wiki ya utumishi, watanunua hizo trekta?, au ni wawekezaji ambao watasaini mikataba ya kuzizalisha? maana kila mwaka ni hizo hizo mbili wanakuja nazo.

  Na je hakuna njia nyingine ya taasisi hizi kuwataarifu wananchi juu ya huduma wanazotoa, maana wengi hawana websites, au siyo updated, hakuna namba za simu ambazo ukipiga utapata majibu au msaada mara moja..hakuna majarida, hakuna publications....ni maonyesho tu?

  Something needs to be done for sure!
   
Loading...