mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,049
- 4,904
Kumekuwa na tabia endelevu kwa wakurugenzi kujirimbikizia Mali au kuiba fedha za serikali ambazo ni jasho la walipa kodi na watoa michango kwa ajili ya maendeleo ya nchi!
Hii hali haikomi?
Kwa mfano, zimepita siku kadhaa tumeshuhudia aliyekuwa mkurungenzi wa Temeke, Bw. Mwakabibi akiburuzwa Mahakamani kwa makosa ya namna hii.
Lakini jana mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale naye akaripotiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa mabati 1,100 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (Hapo ambapo alikuwa mkurugenzi kabla ya kuhamishiwa Gairo)
Bila shaka, wakurugenzi wanapata mshahala mzuri TU, nyumba wanapewa na serikali, maji, umeme bila shaka haviwahusu, maposho yapo kibao!
Kwa nini wanafuja Mali za Umma?
Je, nini kifanyike ili kuipata dawa ya kuzuia madudu ya wakurugenzi wa namna hii?