Wakurugenzi wa Manispaa/ Halmashauri kuiba mali au fedha za serikali, nini kifanyike kukomesha tabia hii?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Kumekuwa na tabia endelevu kwa wakurugenzi kujirimbikizia Mali au kuiba fedha za serikali ambazo ni jasho la walipa kodi na watoa michango kwa ajili ya maendeleo ya nchi!

Hii hali haikomi?

Kwa mfano, zimepita siku kadhaa tumeshuhudia aliyekuwa mkurungenzi wa Temeke, Bw. Mwakabibi akiburuzwa Mahakamani kwa makosa ya namna hii.

Lakini jana mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale naye akaripotiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa mabati 1,100 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (Hapo ambapo alikuwa mkurugenzi kabla ya kuhamishiwa Gairo)

Bila shaka, wakurugenzi wanapata mshahala mzuri TU, nyumba wanapewa na serikali, maji, umeme bila shaka haviwahusu, maposho yapo kibao!

Kwa nini wanafuja Mali za Umma?

Je, nini kifanyike ili kuipata dawa ya kuzuia madudu ya wakurugenzi wa namna hii?
 
Tuachane na Halmashauri za wilaya

Tuwe na Halmashauri za kata.

Mtu anapewa eneo dogo na bajeti yake hapo.

Badala ya kusimamia bilioni 10 kwenye kata kumi.

Anasimamia bilioni moja kwenye kata moja
 
Madelu lamek keshatoa ushauri wa maana:

"wizi wao ufidiwe kwa kodi zaidi na tozo zikiwamo za uzalendo."

Cha kushauri zaidi ni kuwa, kwa vile tumeziridhia kwa bashasha waziongeze zaidi.

Kwanza zikiwa nyingi ndiyo tunazowea kuzilipa.
 
as long as CCM iko madarakani sahau mabadiliko. Kama Rais anaweza kumfunga/kumbambikia mtu kesi, basi acha waibe tu
 
Suluhisho ni kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani
Ikitokea bado CCM itaendelea kutawala, kufanyika Nini?

#Dawa itakayodhibiti kabisa suala hili bila kujali aina ya chama kilicho madarakani!
 
katiba mpya ile ya original iliyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba. Nje ya hapo tutulie sindano iingie
 
Jamaa wanaibaaa!
Na hao nadhan Kuna misunderstanding baina yao, kwa hyo wanachomeshana!.

Bila kupata solution ya hili, tutatozana tozo hatua 500, tutarudi Nyuma hatua 600
 
Solution kwa staili ya bunge lililopo ni ndoto tu mkuu. Na hatuna utamaduni wa maandamano wala mgomo
 
Kumekuwa na tabia endelevu kwa wakurugenzi kujirimbikizia Mali au kuiba fedha za serikali ambazo ni jasho la walipa kodi na watoa michango kwa ajili ya maendeleo ya nchi!

Hii hali haikomi?

Kwa mfano, zimepita siku kadhaa tumeshuhudia aliyekuwa mkurungenzi wa Temeke, Bw. Mwakabibi akiburuzwa Mahakamani kwa makosa ya namna hii.

Lakini jana mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale naye akaripotiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa mabati 1,100 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (Hapo ambapo alikuwa mkurugenzi kabla ya kuhamishiwa Gairo)

Bila shaka, wakurugenzi wanapata mshahala mzuri TU, nyumba wanapewa na serikali, maji, umeme bila shaka haviwahusu, maposho yapo kibao!

Kwa nini wanafuja Mali za Umma?

Je, nini kifanyike ili kuipata dawa ya kuzuia madudu ya wakurugenzi wa namna hii?
Atakaye bainika afilisiwe 🤔
 
Back
Top Bottom