Wakurugenzi wa Kigoma na Mpanda wasimamishwa kazi kwa kusababisha upotevu wa fedha

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb) amewasimamisha kazi Wakurugenzi Watendaji wa Manispaa za Kigoma, Mkoa wa Kigoma na Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza maamuzi ambayo yamesababishia Serikali hasara na upotevu wa fedha.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye Dhamana kama Sheria inavyo elekeza.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Ndugu Suleiman Lukanga ana kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha shilingi milioni tisini na mbili na laki saba na elfu hamsini (92,750,000/=) na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi milioni mia mbili, tisini na nne (294,000,000/=).

Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari Ndilowa ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Ndugu Lauteri John Kanoni ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Tarehe 18 Januari, 2016
 
WAKURUGENZI WA KIGOMA NA MPANDA MKOANI KATAVI WASIMAMISHWA KAZI KWA KUSABABISHA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI

Mpaka Mwaka uishe watu watumishi wa halmashauri watanyooka tu......
 
Sasa si mtamaliza watumishi wote halafu muanze kuhangaika. Nchi yenyewe hii wasomi wachache hii. Hayaa
 
Ukipiga wastani wa hiyo hela kwa hiyo miji miwili ni (92,750,000 + 294,000,000)/2 = 193,375,000

Nchi hii kuna jumla ya halmashauri (wilaya na mikoa) 190. Hivyo, kwa wastani huo, zimepotea 193,375,000 x 190 = 36,741,250,000. Na hayo ni yale maeneo yaliyogundulika tu, bado yako mengi ambayo yamejificha - nenda idara za mifugo, kilimo, mkukuta, mkurabita, elimu, maji, nishati, misitu, ujenzi, mawasiliano, afya, uvuvi, mazingira, uchukuzi, n.k. n.k. n.k! Kote huko ni wizi tu, si ajabu majipu yakafiki trillions!
 
Waziri Simbachawene awasimamisha kazi wakurugenzi watendaji wa Manispaa za Kigoma na Katavi kwa kuisababishia Serikali hasara.
 
Ukipiga wastani wa hiyo hela kwa hiyo miji miwili ni (92,750,000 + 294,000,000)/2 = 193,375,000

Nchi hii kuna jumla ya halmashauri (wilaya na mikoa) 190. Hivyo, kwa wastani huo, zimepotea 193,375,000 x 190 = 36,741,250,000. Na hayo ni yale maeneo yaliyogundulika tu, bado yako mengi ambayo yamejificha - nenda idara za mifugo, kilimo, mkukuta, mkurabita, elimu, maji, nishati, misitu, ujenzi, mawasiliano, afya, uvuvi, mazingira, uchukuzi, n.k. n.k. n.k! Kote huko ni wizi tu, si ajabu majipu yakafiki trillions!
....kwa hiyo halmashauri zote zilikuwa zinajenga skimu na kununua gari za taka sio!! Jipe muda kufikiri!!!
 
Ukipiga wastani wa hiyo hela kwa hiyo miji miwili ni (92,750,000 + 294,000,000)/2 = 193,375,000

Nchi hii kuna jumla ya halmashauri (wilaya na mikoa) 190. Hivyo, kwa wastani huo, zimepotea 193,375,000 x 190 = 36,741,250,000. Na hayo ni yale maeneo yaliyogundulika tu, bado yako mengi ambayo yamejificha - nenda idara za mifugo, kilimo, mkukuta, mkurabita, elimu, maji, nishati, misitu, ujenzi, mawasiliano, afya, uvuvi, mazingira, uchukuzi, n.k. n.k. n.k! Kote huko ni wizi tu, si ajabu majipu yakafiki trillions!
Huyu naye sijui anatumia nini kufikiri. Kwahiyo kesho wakisema Mkurugenzi wa Dodoma asimamishwa kwa kuishi hotelini, utapigia wakurugenzi wote Tanzania?
 
This is the kind of government this country has been missing for the past 30 years. Hongera sana Waziri Simbachawene. Ukweli ni kwamba, moja ya sababu ya kwanini watu huheshimu sana ajira kwa watu/kampuni binafsi ni uharaka wa kuwajibishwa kunapokuwa na utendaji mbovu, na ni kwa nini watu wamekuwa hawaheshimu utumishi wa uma, ni uslow wa kuwajibisha watu, huku huruma na humanitarian grounds zikitumika kutowaadhibu au kuwaadhibu isivyostahili (Ikiwemo kuhamishwa kituo cha kazi) watendaji wanaobainika na utendaji mbovu uendao kinyume na miendendo ya utumishi bora. Utaratibu huu umeligharimu taifa kwa kipindi kirefu, na imekuwa sababu kuu iliyopalilia ufisadi katika hii nchi kufikia kiwango ambacho hakikuwahi kufikiwa.

Natoa Pongezi za dhati kwa Waziri Simbachawene kwa uamuzi huu sahihi, uamuzi huu haukusudii kuwaadhibu hawa watumishi wa kigoma tuu, bali kwa kiasi kikubwa una lengo la kuwajulisha watumishi wengine (walio wengi zaidi) ambao wapo kwenye nafasi kama hizo, na zinginezo ya kwamba; ukurasa mpya umefunguliwa ktk Taifa la Tanzania, na wanatakiwa watazame namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku, wanatakiwa waongozwe na uzalendo na si vinginevyo.
 
Sasa si mtamaliza watumishi wote halafu muanze kuhangaika. Nchi yenyewe hii wasomi wachache hii. Hayaa

Aliyekuambia hii nchi ina wasomi wachache ni nani?. Wewe kama ni mtumishi wa uma, vurunda halafu utafahamu kama hii nchi inawasomi wachache ama laa baada ya wewe kufukuzwa na nafasi yako kuachwa wazi. Umesahau umati wa watu ulioitwa kufanya usaili pale uwanja wa Taifa??.
 
wasomi wengi vilaza.
 
msomi kama mie siwezi kukubali kusimamishwa na kazi na simbachawene ambaye alikuwa konda pale dodoma siasa imemuinua hadi kuwa waziri leo
 
Back
Top Bottom