Wakurugenzi wa Halmashauri kwenye vikao vya CCM, kutoa taarifa ni sawa?

Chama kushika hatamu kaka.Chama kinaisimamia serikali kuhakikisha yote iliyoahidi wakati wa kampeni yanatekelezwa.Mkurugenzi ni serikali anafikisha taarifa kwenye chama kilichomwajiri au ulitaka apeleke ufipa?
Subiri ukichukua nchi utamwambia taarifa awe anapeleka wap.
 
Mkuu wa wilaya anasimamia wilaya mtendaji mkuu ni mkurugenzi so anawajibika kwenda kujibu alivyosimamia shughuli za maendeleo.
 
Ni sawa kabisa.Serikali hii inaongozwa na CCM,kwa hiyo ni lazima CCM ihakikishe kwamba malengo yake kama yalivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi yamefikiwa.Kwa vile wakurugenzi ndio wasimamizi wakuu wa maendeleo katika kila wilaya,ni lazima wahudhurie vikao vya chama ngazi ya Wilaya na Mkoa ili watoe taarifa kuhusu utekelezaji wa malengo ya CCM.Nina wasi wasi hata hivyo kama kweli chama kina wataalam wa "Monitoring and Evaluation!" Chama kinahitaji wataalam hawa ili kuweza kuisimamia serikali kikamilifu.
Hii imetokea Mtwara ambapo wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa kwenye vikao vya chama ambapo walitoa taarifa za utendaji wao. miongoni mwa taarifa walizotoa ni kufungwa kwa soko la ununuzi wa korosho. source TBC

Binafsi sijaelewa kama wakurugenzi ni wanasiasa au watumishi wa umma? Mbona serikali hii inafanya mambo kinyemelanyemela? sasa kama wakiwa sehemu ya wachangia Sera kwenye chama wataweza kusimamia chaguzi kwa haki? Tume ya uchaguzi inatakiwa kutoa onyo otherwise iwaamuru kuhudhuria vikao vya vyama vyote na watoe taarifa equally
 
Sasa mkurugenzi bosi wake ni nani kama sio serikali..? na serikal iliyopo ni ya CCM so kelele za nini sasa watu wa ufipa jamn?
 
Hii imetokea Mtwara ambapo wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa kwenye vikao vya chama ambapo walitoa taarifa za utendaji wao. miongoni mwa taarifa walizotoa ni kufungwa kwa soko la ununuzi wa korosho. source TBC

Binafsi sijaelewa kama wakurugenzi ni wanasiasa au watumishi wa umma? Mbona serikali hii inafanya mambo kinyemelanyemela? sasa kama wakiwa sehemu ya wachangia Sera kwenye chama wataweza kusimamia chaguzi kwa haki? Tume ya uchaguzi inatakiwa kutoa onyo otherwise iwaamuru kuhudhuria vikao vya vyama vyote na watoe taarifa equally
Chama tawala wanao wajibu wa kuisimamia serikali, hivyo wanaweza kuomba taarifa za serikali kama wakizihitaji ili kupima kama ilani yao inatekelezwa ipasavyo.

vyama vya upinzani kazi yao ni kuikosoa serikali pale wanapoona jambo haliende sawa. sio lazima sana wapewe taarifa za utekelezaji, maana hata hivyo serikali haitekelezi ilani zao (wapinzani)

kuhusu uchaguzi.. mie naona hawa wakurugenzi, toka wajipambanue kwamba wameteuliwa miongoni mwa makada wa ccm, wamepoteza uhalali wa kusimamia uchaguzi. nadhani tume inapaswa kuteua wasimamizi wa uchaguzi wengine wanaowajibika kwa tume na sio hawa wakurugenzi wa sasa ambao ni makada wa chama tawala.

Mkuu tambua kuna mambo mengi sana kwa awamu hii yanafanyika kinyume na taratibu za inch kwa mwamvuli wa 'NIA NJEMA YA SERIKALI' mimi binafsi kuna baadhi nayaunga mkono na mengine siyakubali.

naendelea kuchambua mbivu na mbichi, 2020 nitafanya maamuzi.
 
Hii imetokea Mtwara ambapo wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa kwenye vikao vya chama ambapo walitoa taarifa za utendaji wao. miongoni mwa taarifa walizotoa ni kufungwa kwa soko la ununuzi wa korosho. source TBC

Binafsi sijaelewa kama wakurugenzi ni wanasiasa au watumishi wa umma? Mbona serikali hii inafanya mambo kinyemelanyemela? sasa kama wakiwa sehemu ya wachangia Sera kwenye chama wataweza kusimamia chaguzi kwa haki? Tume ya uchaguzi inatakiwa kutoa onyo otherwise iwaamuru kuhudhuria vikao vya vyama vyote na watoe taarifa equally
Hapo ndipo umuhimu wa kulinda kura unapoonekana.
 
Bado viongozi wa kitaifa na halmashauri pamoja na wananchi wengi hawaujui mfumo wa vyama vingi unavyopaswa kufanya kazi.Lakini tatizo kwa sasa limekuwa kubwa kwa sababu linaanzia ikulu.Serikali na chama tawala kuna mipaka yake japo wenye mamlaka wanajifanya vipofu ktk hilo
 
Kuna tatizo
 
Hii imetokea Mtwara ambapo wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa kwenye vikao vya chama ambapo walitoa taarifa za utendaji wao. miongoni mwa taarifa walizotoa ni kufungwa kwa soko la ununuzi wa korosho. source TBC

Binafsi sijaelewa kama wakurugenzi ni wanasiasa au watumishi wa umma? Mbona serikali hii inafanya mambo kinyemelanyemela? sasa kama wakiwa sehemu ya wachangia Sera kwenye chama wataweza kusimamia chaguzi kwa haki? Tume ya uchaguzi inatakiwa kutoa onyo otherwise iwaamuru kuhudhuria vikao vya vyama vyote na watoe taarifa equally

Ni sawa kwa sababu CCM ndio wanaoshika hatamu, ni chama tawala, ilani yake ndiyo inayotekelezwa!!!!
 
kwani hao wakurugenzi wameajiriwa na kulipwa mishahara na serikali ya nani?
 
Back
Top Bottom