Wakurugenzi mnacheza na nauli za likizo za watumishi

Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,126
1,405
Mwanzoni mlikuwa mnacheza na mishahara ya watumishi utakuta wilaya X mshahara tarehe 24 na wilaya Y mishahara tarehe 37. Ila tangia mishahara ihamie hazina sasa hivi watumishi wote kikibonyezwa kitufe tu salary imeingia siku moja kuanzia mbunge, askari, daktari, mwalimu hadi dereva.

Baada ya kubanwa huku sasa hivi wajanja wa halmashauri wamehamisha michezo yao kwenye nauli za likizo.

Mtu anaenda likizo ya malipo disemba 2020 anakuja kulipwa Aprili 2021. Hela mnazungushia kwenye mabenki au mnaweka fixed account mpate faida. Someni alama za nyakati acheni michezo yenu lipeni watu haki zao ndani ya muda husika.

Waziri Jaffo tupia jicho kwa wakurugenzi wa halmshauri janja janja sana hawa jamaa.

"Naomba wachina mtusamehe madeni yetu"
 
Kwanza fedha zenyewe za likizo kipindi hiki zipo? Nilimsikia mama mmoja Zanzibar wakati Dr. Mwinyi anaongea na wafanyakazi wa kada ya afya akisema hawapati fedha za likizo.
 
Sio hivyo tuu ajira mpya wilaya X wamelipa pesa za kujikimu na halmashauri X hawajalipa pesa za kujikimu. Sasa nashindwa kuelewa tatizo lipo wapi hasaa.
 
Lete ushahidi. JF siku hizi inakosa mvuto Kama zamani. Tuhuma zinawekwa bila ushahidi uliochambuliwa na kuunganishwa
 
Kuna tatizo kubwa sana kwenye hizi halmashauri zetu
 
Kwanza fedha zenyewe za likizo kipindi hiki zipo? Nilimsikia mama mmoja Zanzibar wakati Dr. Mwinyi anaongea na wafanyakazi wa kada ya afya akisema hawapati fedha za likizo.
Fedha zipo ndio maana wananunua magari ya milioni 400.
Ingekuwa hakuna hela wangenunua IST
 
Sio hivyo tuu ajira mpya wilaya X wamelipa pesa za kujikimu na halmashauri X hawajalipa pesa za kujikimu. Sasa nashindwa kuelewa tatizo lipo wapi hasaa.
Hapo ndipo janja janja inapoanza mkija kutahamaki hela imeshazaa benki
 
Leta ushahidi sio kuongea paukwa pakawa taja halmashauri na mkurugenzi wake na afisa mwajiri tuanzie hapo kujua walikotoka
 
Huyo mkurugenzi anazihamishia vipi hizo pesa kwenye akaunti yake ya muda maalum. Mfano, tuseme umejilipa mil. 400 ya madai au malipo ya watumishi halafu ukazifungulia fixed account huko benki, tunaomba ka ufafanuzi kidogo..
 
Ni ukweli kuwa wakurugenzi hukalia madeni ya watumishi na kuzifanyia fedha hizo kazi nyingine ambazo kupitia humo wanajinufaisha kwa namna moja au nyingine. Mh JAFFO fuatilia suala hili. Kuna nauli za likizo, kuna uhamisho nk hawa wakurugenzi hawajali. Wao na maofisa wao wako bussy wakijilipa extra duty allawances huku madaktari, manesi , na watumishi wengine kama walimu wakisotea madai hayo bila mafanikio. Mh waziri Jaffo fuatilia hili suala. Watumishi wanakosa imani na serikali kutokana na uzembe, na kutokujali kunakofanywa na wakurugenzi na maofisa wake katika halimashauri nchini. Natamani katika ziara zako utenge muda pia kusikiliza kero za watumishi isiwe tu ni hiyo miradi pekee.
 
Haya pengine ni majungu. Weka mambo hadharani tuanzie hapo. Halmashauri X, na Mkurugenzi X. Ndo nn?
 
Back
Top Bottom