Wakurugenzi Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Wakurugenzi Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi.

Akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa agenda ya mapato inaenda sambamba na kigezo cha kupima kiasi cha fedha kilichotolewa na Halmashauri katika kutatua kero za wananchi hususani katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, barabara, Masoko, na kuwekeza kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Waziri Ummy amewataka kuhakikisha wanatenga asilimia 40 ya mapato ya ndani yasiyolindwa inatengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ambazo zinapata mapato chini ya Bilioni 5 na wale wanaokusanya zaidi ya bilioni tano wanatakiwa kutenga asilimia 60

Anaendelea kusema kuwa Halmashauri nyingi zinatenga fedha lakini bado hazigusia moja kwa moja wananchi kutatua kero za wananchi , niwaagize kuwa fedha hizo zisitumike kwa matumizi ya kuendesha ofisi bali zitumike katika miradi ya maendeleo

“Sitegemei kuona fedha hizi zinatumika kwa ajili ya matumizi ya ofisi, nategemea fedha hizi zijenge zahanati, madarasa, mabweni, maabara, barabara, masoko, stendi na si kugharamia posho za vikao” amesisitiza Waziri Ummy

Amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendelo katika Halmashauri zao lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika maeneo yao

Aidha amesema kuwa mapato na matumizi kwa maendeleo ya wananchi si kazi nyingine
IMG_20210924_152359_706.jpg
IMG_20210924_152359_622.jpg
IMG_20210924_152359_706.jpg
 
Safi, ni hatua nzuri ya kuibua uwajibikaji na uadilifu ingawa kuna baadhi ya halmashauri zina vyanzo dhaifu sana!
 
Kigezo pekee kisiwe mapato tu ingawa kiwe kigezo muhimu
Mapato ndio muhimu kwa halmashauri
 
Ni kweli ndo maana Waziri amesisitiza Mapato, lakini pia kigezo kingine ni namna Halmashauri zinatenga mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri zao
 
Hii serikali wasaidizi wa Rais wanatoa matamko yanayoleta ukakasi sana, hili tamko la waziri linaweza sababisha wakurugenzi waanze uporaji kwa wafanyabiashara ili kutimiza malengo ya ukusanyaji mapato.

Tumeona kwenye ilivyotokea kwenye Corona, Rais anasema watu wavae barakoa wakati mwenyewe anaitisha mikusanyiko huku watu hawana barakoa.
 
Wakurugenzi Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi.

Akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa agenda ya mapato inaenda sambamba na kigezo cha kupima kiasi cha fedha kilichotolewa na Halmashauri katika kutatua kero za wananchi hususani katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, barabara, Masoko, na kuwekeza kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Waziri Ummy amewataka kuhakikisha wanatenga asilimia 40 ya mapato ya ndani yasiyolindwa inatengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ambazo zinapata mapato chini ya Bilioni 5 na wale wanaokusanya zaidi ya bilioni tano wanatakiwa kutenga asilimia 60

Anaendelea kusema kuwa Halmashauri nyingi zinatenga fedha lakini bado hazigusia moja kwa moja wananchi kutatua kero za wananchi , niwaagize kuwa fedha hizo zisitumike kwa matumizi ya kuendesha ofisi bali zitumike katika miradi ya maendeleo

“Sitegemei kuona fedha hizi zinatumika kwa ajili ya matumizi ya ofisi, nategemea fedha hizi zijenge zahanati, madarasa, mabweni, maabara, barabara, masoko, stendi na si kugharamia posho za vikao” amesisitiza Waziri Ummy

Amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendelo katika Halmashauri zao lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika maeneo yao

Aidha amesema kuwa mapato na matumizi kwa maendeleo ya wananchi si kazi nyingineView attachment 1951124View attachment 1951125View attachment 1951126
Wakurugenzi wana-enjoy maisha V8, Posho, nyumba, Safari (per diems@250,000/=) hpao ukiacha deals. Sasa unashindwaje kukusanya mapato?
 
Back
Top Bottom