Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo, je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini?
 
Tulikuwa tunapenda sana kuchezea maji na utelezi hasa mvua inaponyesha, tena bila viatu kama picha hii inavyoonesha.

kitt-713792.jpg
 
Shule zetu nyingi tulizosoma zilikuwa hivi na akili zilikuwemo leo hii mazingira mazuri na facility kwenye shule nyingi hasa za mjini zipo ila mitoto bomu bomu sijui tatizo ninini hasa au ndio hivyo tena nchi imeharibika na haina mwenyewe kuanzia chini hadi kwa wenye nchi???
3583548_orig.jpg
 
nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
 
nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
.......halafu ulikuwa mwoga sana kukoga...!unakaa hadi wiki nzima...!:D
 
.......halafu ulikuwa mwoga sana kukoga...!unakaa hadi wiki nzima...!:D

hahaa ka ulikuwepo na kule kwetu baridi kama makambako....i used to do it once a week (aftarol si nilikuwa mtoto kwani nini mbaya?)
 
Nilikuwa nasubiri wakati wa mapumziko kukunua bagia,mabumunda,visheti na ubuyu,na iskirim alafu unatemea mate ili usiombwe

hahaaaa hivi wewe nani kakuamsha leo lakini!!!!!!!!!!!!!!! aaaaaaaaaaah mule mule tuuuu LOL!!!!!!!! U ARE KILLING ME PEARL!!
 
alafu kwa sisi wasichana break unasubiri kucheza lede
hahaaaa hivi wewe nani kakuamsha leo lakini!!!!!!!!!!!!!!! aaaaaaaaaaah mule mule tuuuu LOL!!!!!!!! U ARE KILLING ME PEARL!!
 
Back
Top Bottom