Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Mie nakumbuka kuwa tulikuwa tunakwenda uwanjani kupigana bila sababu yeyote!
Yaani ilikua tu inaamriwa kuwa leo ni flani na flani basi tukiruhusiwa tu ni lazima kwenda hata kama hutaki! (utoto bana)

Sasa zamu yangu ikafika bana daah nikapangiwa dogo mmoja ana mikwara balaa! Nikaamua nitoroke ila nikamshirikisha dogo mwingine nae akakisanua kuwa nna mpango wa kutoroka!

Mda ulipofika nikawekwa mtu kati!! Mpka uwanjani na huo uwanja ulikuwa mbali kidog na shule na hakukua na wapitaji wengi.
Ile kufika tu mpinzani wangu keshavua shati anaruka ruka ki Bruce Lee kwakweli nikazidi kugwaya!!

Sijakaa sawa akawa anakuja mbio ili anirukie na bahati mbaya akajikwaa akapiga mweleka!! MUNGU anipe nn tena ukizingatia uoga nilokuwa nao nikamuwahi kabla hajaamka! Ebwana eh kumbe alikua mtupu balaa!!

Kwakweli nilimchakaza sana na ndo ikawa mwisho wa mchezo ule Kwan kesi ilikuwa kubwa na kubwa zaidi lile tukio likanifanya nipate na kidem kikali sana pale skul! Na mpk leo huwa tukikutana tunapasha kiporo!
 
Huu ni uongo ni kazi ya shigongo michezo hii inakuwaga la pili na la tatu umri ambao si wa kupenda madem
 
unakumbuka nini ukiwa shuleni.ni vingi sanaaa
kucheza dansii class
wizi wa vitabu

na mwisho kabsa sjui niliseme daah acha iwe sirii
 
Kukagua number kwa waliochelewa ilikuwa ni saa sita mchana, wakati wa kwenda mstarini wakati wa ukaguzi mimi najificha darasani, na hii ilikuwa ni akili na siri yangu tuu zima darasani.

Shule za mikoani ni viranja kuchapa kwa kwend a mbele km waalimu hiyo hawat iacha kamwe ni kama ma Mbwa halafu wote hakuna aliyekuwa anafaulu kwenda sec. yote ni mambulula.

Bora za mjini hawachapi watoto. halafu ndo wanashinda ni ile mbaya, ndo wamejaa kwenye mabenki, Afya-Hosp, wanamuziki maarufu, wale kule wa vijijini wanafundishwa ujinga na woga wa kuto dhubutu. shenzi kabisa waalimu wa vijijini.
 
SHULE YA MSINGI KIBUMAYE SLP172, TARIME- MARA

Mbona ha-mumo humu ina maana wote mlibaki kijijini kweli? wale wajanja Bhoke Mahindi, Daniel Mugaya, Japhet Mugaya, Marwa Ghesara. Ngochiro, Yosubho Kaka mkuu, Mwita Wambula. Mwita kihughi, Kasisi Maghweina, Jane Lameck - Nasikia uko USA Unaosha wazee!, Josephina Shana, Masamaki Manyonyi, Dani shana- huyu afisa usalama huko Bongo. Pili Benigna machemba , Binti wa mwalimu benigna machemba darasa la kwanza, Mili samson. Mwalimu Ghikaro uko wapi wewe?

KIJIJI CHA UJAMAA MOGHABIRI. Daaaah! kweli
 
Nilikuwa mchafu kuoga, mchelewaji na mvivu wa kufanya usafi.

Darasani sasa... Kwanzia darasa la 4-7 nilikuwa ndani ya TOP TEN.

Kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la 4 (second term) niliingia TOP TEN nikiwa ktk nafasi ya 7. Kwanzia hapo nikaendelea kupanda hadi top 3 darasa la 6. Kufika darasa la 7 nikaenda namba 1.


ila Maths ilikuwa inaniletea usingizi :p :p :p . Mengine yote sikuwahi kupata B kwanzia darasa la 6.

Hakuna moment <3 <3 tamu <3 <3 kama za Primary school wallah!
 
Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa mkubwa kidogo kunizidi alikuwa swaiba sana,sasa walimu walimuamini sana wakawa wanamtuma kuwanunulia chapati,maziwa,supu,sasa jamaa akawa kila akiagizwa na walimu ananichukua tunaenda pamoja.

Sasa Tabia yake kila anachoagizwa na maticha lazima apunguze nusu anakula alikuwa hawezi kupeleka kitu kamili hata siku moja,akiagizwa supu lazima apunguze minofu ya nyama anakula nusu ndio anapeleka ikiwa ni sukari lazima alambe ,na hiyo ndio alikuwa Tabia yake cha ajabu walimu walimpenda sana kwa kuwa ektia tabia nzuri wakati akiwa nyuma ya pazia ni matusi!!

Mimi nilikuwa nachora sana picha za kwenye vitabu...magazeti ya kiu,sani..na haya ya michezo,tulikuwa tunafatilia sana habari za watu maarufu iwe ni wacheza mpira(enzi za Beckham),muziki(Eminem,Rkelly,Nas)siasa(habari za wabunge mawaziri).
Tulikuwa tunapenda kurap kwa kushindana kwa makundi tunatumia peni kama mic,kundi letu tulijiita 2boys Mimi na jamaa yangu hamisi B,sijui yupo wapi kwa sasa...tulishanda na kundi LA jamaa mmoja aliitwa ERIC tukishandania zawadi ya mapapai tukio lilifanyika nyuma ya shule.
 
Unajua nikiwa mdogo nilikua ka handsome.Afu enzi hizo napelekwaga shule na pegiot(enzi hizo usafir wa namanga)..
Sasa nilikua napendwapendwa sana na vibinti.Mchungaji mmoja mwenye asili ya kikenya alileta kesi ya binti wake kaniandika jina langu kwenye tisheti yake kwa lipstick.Akataka kunijua nafananaje.Aliponiona...sijui waliongea nini.

Kesi ilikua kubwa.sema iliisha juu kwa juu..Ki ukweli binti alikua mweusi tiii.Hakua anavutia.Dah!nikawa nataniwa kila siku na wanafunzi wenzang.Sema kalikua kananipenda kweli.Nimekula sana ngubiti,mihogo,barafu,ufuta,kachori n.k kwa pesa yake.Hata sijui yuko wapi sasa..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua nikiwa mdogo nilikua ka handsome.Afu enzi hizo napelekwaga shule na pegiot(enzi hizo usafir wa namanga)..
Sasa nilikua napendwapendwa sana na vibinti.Mchungaji mmoja mwenye asili ya kikenya alileta kesi ya binti wake kaniandika jina langu kwenye tisheti yake kwa lipstick.Akataka kunijua nafananaje.Aliponiona...sijui waliongea nini.

Kesi ilikua kubwa.sema iliisha juu kwa juu..Ki ukweli binti alikua mweusi tiii.Hakua anavutia.Dah!nikawa nataniwa kila siku na wanafunzi wenzang.Sema kalikua kananipenda kweli.Nimekula sana ngubiti,mihogo,barafu,ufuta,kachori n.k kwa pesa yake.Hata sijui yuko wapi sasa..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana nilikuwa na chawa! usisikie, kichwani nguoni, hata mashuka ! utitiri ndo yalikuwa maisha yangu! nililala na kuku. usiku hulali, ajabu ya Mungu nilikuwa sisinzii!

kaptura ya shule ina matobo matakoni, shati no vishikizo! basi si kuchekwa na wenzio, iktokea nimepata mpya naitunza km roho yangu. naogopa hata kuichafua nisije ifua.

Mafuta yangu ni sabuni ya Kwanga, kila siku asubuhi, naitunza napo jua ikiisha nanunua kipande ambacho leo ni sh 100/=

Sikutambua kuwa nina akili kiasi kile, wanafunzi ndo walikuwa wananipa hongera na baadaye kuniheshimu kwa hili sababu sikuwahi kupongezwa na watu nilio ishi nao, hata kuambiwa tu thamani ya shule, zaidi nilikuwa nakwepa taabu ya kuchunga ng'ombe na kilimo.
 
nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
🤣
 
Back
Top Bottom