Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Nakumbuka nilikuwa mpole tu lkn sionewi na mwanamkee, ata akiwa bonge na mkubwaje mwanamke napigana nae lkn staki walimu wajue naenda kupigana hukoo viwanjani, lkn mwanaume ata akiwa mdogo vp sithubutu ata kurusha ngumi niliwaogopa balaa

Sitasahau darasa la pili nilikutana namvuta bangi mmoja akanikalisha chini huku akinisihi nisiogope kisha kuanza kuomba nimpe changu na yeye anipe chakee nikamwambia mpaka tuende hospital vikakatwee na kipindi hicho nilitaman sana kuzaliwa mwanaumee nikaenda kusema nyumbani wakacheka kuzimia lkn sijuelewa, nilikuja kuelewa alimaanisha nini nikiwa form one hahahahaaa

Sitasahau jamani nilikuwaga naakili primary lkn pacha wangu hajui ata kutofautisha daftar la kiswahili na english au sayancee hahahaa nilikuwa naumia sana akichapwa au akipewa adhabu nzitoo

Sitasahau kakaangu alimaliza la saba na sisi kukataa kwenda chekechea eti na sisi tumemaliza bushiii hahaaa

Sitasahau zile msituumizieeee inapochezwa mechi ya la sita na la sabaa au shule tofaut na vingine vingiiiii
 
Nakumbuka wakati wa kuvaa nguo za shule nasahau kuvua skert ya kushindia nikifika njian najikuta nimevaa skirt mbili navua nachimbia shambani kwa watu nikitoka napitia siku nikasahau nilikochimbia ilikuja kuonekana msimu wa kulima ikiwa imeozaa hahahaaa
 
Daaahh, umenikumbusha sana, Atlas niliifanyia haki sana.

Ramani ya Tanzania, Afrika mashariki, Afrika na Dunia kuonesha Utawala, Tabia ya Nchi, Kilimo, Ufugaji, Utalii, Sura ya Nchi, Uchukuzi na Mawasiliano(hasa usafiri wa Anga), Uvuvi, Viwanda, Madini n.k, niliviweka kichwani kwa msaada wa Atlas.

Swali la Ramani kwenye Maarifa ya Jamii lilikuwa haliachwi salama.
Teh

Kuna jamaa nlmwambia nionyeshe faga soni ilipo alikaa mpaka jioni

Ni jamaa angu sana now
 
Nakumbuka primary tulikua tunasoma Mimi na Dada yangu.... Tulikua tunatoka saa kumi hatukuwa tumelipiwa ela ya lunch shuleni Kuna madam mmoja Mungu amlinde akatuambia mda wa lunch ukifika tuwe tunakula freee Kama vile tumelipa Tena na majina yetu yakasndikwa kwenye daftari la waliolipa ela ya chakula.... Kuna baadhi ya walimu Ni ma heaven sent etiiii
 
Kutajiana majina yaliyojificha kwenye atlas.

Dah aisee, sijui hata hawa broiler wanajua hata atlas ni nini
Umenikumbusha mbali na hii kitu aisee!

Nilikuwa bingwa wa kutoroka kazi za nje hasa za kilimo na kufyatua tofali.
 
Mwalimu Kimbengele wa somo la hisabati pale Naura Primary school alikuwa na tabia ya kumuita mwanafunzi mbele ya darasa na kumuambia asolve hesabu fulani, ukikosea yeye alikuwa anachapa fimbo kwenye vigimbi ilikuwa hatari tupu, huyu mwalimu alikuwa anaishi mtaa wa Bondeni pale Arusha mjini na alikuwa na mtoto wake anaitwa Hamza. Sijui kama mwalimu huyu bado yuko Arusha.
Dah dunia ni ndogo!!! Alifundishaga pia na Meru Primary, Na yuko Arusha bado ila kwa sasa nahisi anaishi kisongo sina uhakika sana though
 
Hii ilitufanya tuwe na uwezo wa kutambua miji mikuu ya kila nchi na kufaham kila nchi iko upande upi wa dunia.
Leo hii kuna mwanafunzi yuko mwaka wa nne chuo, ila ukimwambia burma ni nchi jirani na ipi, hajui hata iko wapi.
 
Nakumbuka nilikua siingii darasana naenda kushinda mtoni mpka masomo yanaisha jioni narud hom kama nimetoka shule ilikua karibu na mitihani mwez wa tano ila nikaja nikashika nafasi ya tatu likizo mwez wa 6
 
Majina kwenye Atlas,,,tumetoka mbali jmn

Kutajiana majina yaliyojificha kwenye atlas.

Dah aisee, sijui hata hawa broiler wanajua hata atlas ni nini

Hii I'd yako n kichekesho tosha
Nyela mumo dah nmecheka mm

1. Nakumbuka nilikuwa nachora Sana, Nakumbuka nilikuwa nikifanya kosa, Mwl wangu ananipa adhabu ya kumchora.

2. Nakumbuka sikwenda shule mwaka mzima darasa 4, nyumbani na shuleni walijua ntafeli kwenda Darasa la 5, mara paaap nikawa Mwanafunzi wa Mwisho kufanya vizuri kwenda Darasa la Tano.

3. Nakumbuka nilikuwa nikitoka shule nauza Mapapai, au napeta Pumba za Mpunga napata Chenga nauza, muda Mwingine natengeneza Magari ya mbao nauza Shule.

4.Nakumbuka Darasani liliwekwa shindano la U handsome nikawa mtu wa pili, tena wakwaza walimpa kwasababu alikuwa ana kilema cha jicho.

5.Nakumbuka tulitoka kubeba tofari na mchanga wa kujengea tumechoka vibaya, Mwl alie kuwa anasimamia ndio Mwl wa Darasa, tumefika Darasani anataka kuchapa walio chelewa namba nilitoka mbio hatari, karibu Darasa zima likaunga tela kunikimbiza kumbe wengi wao pia ndio walichelewa.


6. Nakumbuka nilikuwa full Comedy nikijibu swali Waalimu wanacheka mpaka basi, wengine walikuwa wanapenda kutembea na Mimi kila sehemu, walimu wengine tunaenda nao mpaka virabu vya Pombe.


Yoooh men trust me am full package at this life... Najua wapi tupo na wapi tunaenda.. Just show love kwa Jpm. Mengi yameshaanza kuwa Historia hapa Tanzania.

huu mtindo wa kutaja maneno makubwa halafu watu wanakomaa kutafuta tumaandishi tudogo

Aisee umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka siku tuliyohangaika kutafuta URUSI. Yaani tulitokwa jasho maana sisi tulikuwa tunatafuta maandishi madogo kumbe yenyewe makubwaaa



Nakumbuka jambo moja kama sio mawili niliwahi kupenda tena nikiwa la tano nilibeba mahindi na mihogo kumpelekea kipenzi, ila sikuwahi kumwambia zaidi ya kumjali sana, sikuwahi kumuona tena huyo binti mpaka leo alihama tukiwa la sita.

Ila hii ndio kubwa kwa sababu nilikua kichwa maji darasani nilikua wa pili toka mwisho toka la tatu mpaka darasa la nne'la tano hivyo hivyo ya huko mbele siwezi sema maana ni maajabu matupu.
Nilinunuliwa baiskeli nikiwa la sita, tukiwa likizo nikaanza kuitumia naenda nayo hapa na pale baada ya kufungua nikaanza kwenda nayo shule. Siku ya kwanza nikaungana kimsafara na wenye baiskeli nikampakiza na rafiki yangu mmoja tukaenda,siku iliyofuata nikampakiza tena rafiki yangu,ikawa hivyo kama wk mbili,tukawekewa utaratibu wa kurudi even class hapo ndio visa vilianza sasa.
Siku hiyo ilifika ya evenclass ,nilivyo rudi even class wakati wa kutoka mida ya jioni nikaungana na wenzangu huku tunatembea mpaka nyumbani na ilikua ijumaa kumbe bwana!! nimesahau baiskeli shule! , nikafika home nikara nikamaliza natoka nikachukue baiskeli siioni,uliza huku na kure bila kuwaambia home sikuipata nikakaa kimya nikajua imeibiwa,jumatatu nikaamka mapema sana ilinisiulizwe ile nafika tu shule naiona baiskeli ipo na unyevunyevu.
Hilo tu kusahau baiskeli siku mbili liliniacha hoi mpaka leo .

Nilpofika la sita nilichange na la saba nilishika namba 3 kwa darasani kabla ya mitihani ya mwisho kuanza,mtihani wa kata nilikua wa 4,wilaya 17,mkoa 7 na kitaifa 1327. Nw nipo netherland nasoma masters.
Shule ilikuwa nzega english medium.


Kusahau baiskeli shule
 
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
Jaman mi nakumbuka nlisoma shule flan ipo pale Kahama.. kuna siku nlichezea kichapo jaman mpk nkajikolea jamankisa tu nliongea kwa utan tukiwa mstarini kwamba mwalimu anachawa duh huwa siwez kabisa kusahau kitu hko naona ni kama jana tu nmefanyiwa jambo hlo!!
 
Kuiba Pencil then unaibadili rangi kwa wino wa Pen
1562056251763.jpeg
 
Daah... Darasa la sita nilijishaua kutaka kugerezea kwenye mtihani... Sikuwai jaribu na siku niliojaribu nilikamatwa hapohapo, nikapelekwa staff room... Nilichapwaaa. ... Sijarudia tena kubeba vitu kwenye mtihani

Nyingine tulikamatwa mimi na rafiki yangu tunachezeana zile fimbo sintasahau... Tulichangiwa na walimu kuchapwa
 
Jaman mi nakumbuka nlisoma shule flan ipo pale Kahama.. kuna siku nlichezea kichapo jaman mpk nkajikolea jamankisa tu nliongea kwa utan tukiwa mstarini kwamba mwalimu anachawa duh huwa siwez kabisa kusahau kitu hko naona ni kama jana tu nmefanyiwa jambo hlo!!
 
Daah... Darasa la sita nilijishaua kutaka kugerezea kwenye mtihani... Sikuwai jaribu na siku niliojaribu nilikamatwa hapohapo, nikapelekwa staff room... Nilichapwaaa. ... Sijarudia tena kubeba vitu kwenye mtihani

Nyingine tulikamatwa mimi na rafiki yangu tunachezeana zile fimbo sintasahau... Tulichangiwa na walimu kuchapwa
Mlikuwa mnachezeanaje?

Unaweza kufafanua angalau kidogo?
 
Back
Top Bottom