Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Nakumbuka jambo moja kama sio mawili niliwahi kupenda tena nikiwa la tano nilibeba mahindi na mihogo kumpelekea kipenzi, ila sikuwahi kumwambia zaidi ya kumjali sana, sikuwahi kumuona tena huyo binti mpaka leo alihama tukiwa la sita.

Ila hii ndio kubwa kwa sababu nilikua kichwa maji darasani nilikua wa pili toka mwisho toka la tatu mpaka darasa la nne'la tano hivyo hivyo ya huko mbele siwezi sema maana ni maajabu matupu.
Nilinunuliwa baiskeli nikiwa la sita, tukiwa likizo nikaanza kuitumia naenda nayo hapa na pale baada ya kufungua nikaanza kwenda nayo shule. Siku ya kwanza nikaungana kimsafara na wenye baiskeli nikampakiza na rafiki yangu mmoja tukaenda,siku iliyofuata nikampakiza tena rafiki yangu,ikawa hivyo kama wk mbili,tukawekewa utaratibu wa kurudi even class hapo ndio visa vilianza sasa.
Siku hiyo ilifika ya evenclass ,nilivyo rudi even class wakati wa kutoka mida ya jioni nikaungana na wenzangu huku tunatembea mpaka nyumbani na ilikua ijumaa kumbe bwana!! nimesahau baiskeli shule! , nikafika home nikara nikamaliza natoka nikachukue baiskeli siioni,uliza huku na kure bila kuwaambia home sikuipata nikakaa kimya nikajua imeibiwa,jumatatu nikaamka mapema sana ilinisiulizwe ile nafika tu shule naiona baiskeli ipo na unyevunyevu.
Hilo tu kusahau baiskeli siku mbili liliniacha hoi mpaka leo .

Nilpofika la sita nilichange na la saba nilishika namba 3 kwa darasani kabla ya mitihani ya mwisho kuanza,mtihani wa kata nilikua wa 4,wilaya 17,mkoa 7 na kitaifa 1327. Nw nipo netherland nasoma masters.
Shule ilikuwa nzega english medium.
 
unakuwaje wa 17 kiwilaya halaf uwe wa 7 kimkoa???kama kiwilaya wamekupita watu 16 premise yake ni kwamba kimkoa watakuwa wamekupita watu zaid ya 16,weka vzuri kumbukumbu zako jombaa maana wilaya ni subset kwny mkoa
 
Ni mitihani tofauti (au ya maandalizi kabla ya mtihani wa taifa au wanaita moko kata,wilaya,mkoa ) hiyoo ina level kama huku elewa,mnaanza mitihani ya darasani,mnakuja mitihani ya kata inaisha, inakuja ya wilaya inaisha,inakuja ya mkoa inaisha,halafu unkuja wa taifa kwa ujumla(ambao unamatokeo yake kikata,wilaya na mkoa nadhani hapa ndio sikueleza vizuri na nilikuchanganya bila shaka) ambao shule yetu ilikua ya kwanza kimkoa baada ya mtihani wa taifa. So kama ilikua ya kwanza kimkoa kiwiliya ilikua ya kwanza pia,na kata kwa mana hiyo nilikua wa saba kwa kila level ,darasani .katani.wilayani na mkoani lakini kitaifa nikwa elfu moja na kitu.
 
unakuwaje wa 17 kiwilaya halaf uwe wa 7 kimkoa???kama kiwilaya wamekupita watu 16 premise yake ni kwamba kimkoa watakuwa wamekupita watu zaid ya 16,weka vzuri kumbukumbu zako jombaa maana wilaya ni subset kwny mkoa
Jamaa kasema yupo Uholanzi anatafta master
 
Nakumbuka ile moment mkimaliza shule mnaandika kwenye kuta za vyoo na fens AKUMBUKWE OCHUMERAA
 
Nilijinyeaga LA tano mama akakataa kunifulia ile uniform sikuigusa tena hiyo ni manundu primary kodogwe tanga mwaka 1992 enzi za mwaliaje na dogoli
 
Nikiwa Jamhuri Primary school pale Moshi mjini mtaa wa Lusaka, nilitokea kupendana kupita kiasi na mwanafunzi aliyekuwa anaitwa Fatuma Ramadhani Mawalla dah! sasa hivi sijui yuko wapi huyu dada nilitengana naye baada ya baba kupata uhamisho wa kikazi kutoka Moshi kwenda Arusha,ndipo na mimi nilipohamia shule ya msingi Naura iliyopo nyuma ya Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Arusha. Dada Fatuma popote ulipo bado uko kwenye kumbukumbu zangu.Hata Nelson Omari Mwariko alikuwa anatambua mapenzi yetu yalivyokuwa, siku moja nilitoroka naye shule nikaenda nae maskani police line,Mzee alikuwa ameingia kazini asubuhi nikajua kurudi kwake mpaka 1400 hrs,wakati nataka kuanza show nikasikia sauti ya father huko nje akisalimiana na jirani yetu,ikabidi nifungue mlango faster Duh! moyo ukanipasuka kitu kikasinyaa nikajua ntachezea stick za kufa mtu wakati huo Fatuma alikuwa anatetemeka kishenzi, Mzee akaingia tukamsalimia alikuwa katika mood nzuri nikamwambia nilisahau daftari ndio huyu mwenzangu akanisindikiza kuja kulichukua, Mzee alitabasamu na kupotezea.Tulimuaga na kurejea shuleni. Sikuamini kama nimesalimika siku hiyo,maana father alikuwa mtata!
 
Kuna mwamba mmoja alikua anapata 49/50 Hesabu, yaani anajikosesha makusudi kila pepa, Somebody Budeba George, alikua akija shuleni mnasema tulieni tu marking scheme imefika, sijui mwamba huyu yupo wapi sahivi
 
Yaani kama kawaida,nakumbuka tukiwa eneo la uwanja wa ndege tulifukuzwa na gari ya zimamoto haloo! tulitoka mkuku vibaya mno!
 
Kutajiana majina yaliyojificha kwenye atlas.

Dah aisee, sijui hata hawa broiler wanajua hata atlas ni nini
Daaahh, umenikumbusha sana, Atlas niliifanyia haki sana.

Ramani ya Tanzania, Afrika mashariki, Afrika na Dunia kuonesha Utawala, Tabia ya Nchi, Kilimo, Ufugaji, Utalii, Sura ya Nchi, Uchukuzi na Mawasiliano(hasa usafiri wa Anga), Uvuvi, Viwanda, Madini n.k, niliviweka kichwani kwa msaada wa Atlas.

Swali la Ramani kwenye Maarifa ya Jamii lilikuwa haliachwi salama.
 
Nakumbuka nilipigana na rafiki yangu mpaka akazimia kwa masaa manne nilitandikwa mboko na mwalimu wa zamu sintosahau maishani
 
Back
Top Bottom