Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Chips za 20/- na Sunvita
Kucheza kitenesi uwanja mmoja madarasa yote,kila darasa na kitenesi chake golini kuna makipa Saba((kila darasa na kipa wake) uwanjani sijui idadi,ukisikia usawa ndio huu.
 
1. Nakumbuka nilikuwa nachora Sana, Nakumbuka nilikuwa nikifanya kosa, Mwl wangu ananipa adhabu ya kumchora.

2. Nakumbuka sikwenda shule mwaka mzima darasa 4, nyumbani na shuleni walijua ntafeli kwenda Darasa la 5, mara paaap nikawa Mwanafunzi wa Mwisho kufanya vizuri kwenda Darasa la Tano.

3. Nakumbuka nilikuwa nikitoka shule nauza Mapapai, au napeta Pumba za Mpunga napata Chenga nauza, muda Mwingine natengeneza Magari ya mbao nauza Shule.

4.Nakumbuka Darasani liliwekwa shindano la U handsome nikawa mtu wa pili, tena wakwaza walimpa kwasababu alikuwa ana kilema cha jicho.

5.Nakumbuka tulitoka kubeba tofari na mchanga wa kujengea tumechoka vibaya, Mwl alie kuwa anasimamia ndio Mwl wa Darasa, tumefika Darasani anataka kuchapa walio chelewa namba nilitoka mbio hatari, karibu Darasa zima likaunga tela kunikimbiza kumbe wengi wao pia ndio walichelewa.


6. Nakumbuka nilikuwa full Comedy nikijibu swali Waalimu wanacheka mpaka basi, wengine walikuwa wanapenda kutembea na Mimi kila sehemu, walimu wengine tunaenda nao mpaka virabu vya Pombe.


Yoooh men trust me am full package at this life... Najua wapi tupo na wapi tunaenda.. Just show love kwa Jpm. Mengi yameshaanza kuwa Historia hapa Tanzania.
 
mi pia nakumbuka mambo mengi mengi ila kubwa zaidi kipindi hikohiko nipo primary ndipo nilipo mpenda mwanamke ambae hadi Leo anaishi moyoni mwangu(ifaamike wazi si kwamba huyo mwanamke ni mke wangu,ila ndiye hasa moyo wangu upo kwake,japo nasikitika kuwa huenda hata nikafa bila kumuona tens dah)popote ulipo miss Rose,dah plz kama upo humu ni pm tafadhari tupige story mbili tatu,tukumbushane ya long time ya kule yombo.
 
Nilikua najifanya mbabe darasani siku moja nikamchokoza dogo mmoja akanitia ngumi dah jino likatoka japo baadae likaota tangu hiyo siku nikawa sina ubabe tena
 
Chips za 20/- na Sunvita
Kucheza kitenesi uwanja mmoja madarasa yote,kila darasa na kitenesi chake golini kuna makipa Saba((kila darasa na kipa wake) uwanjani sijui idadi,ukisikia usawa ndio huu.
Hapo hakuna wa timu nyingine anayegusa mpira wa timu nyingine, na wote mnatambuana. Mara zote huwa nasema, pamoja na sisi Waafrika hatujawa na uwezo wa fikra madhubuti za kuondoa umasikini wetu, ila tuna Upendo wa dhati sana kuliko mataifa mengine
 
Madam Salome Haule kama upo humu jf mm ni mwanafunzi wako,ulihama shule ile (huko simiyu) baada ya sisi kumaliza,ninakumbuka mambo mengi ulinitendea mazuri na yaliyofungua njia ya mafanikio yangu,nimejitahd sana kukutafta kwny mitandao ya kijamii sijafanikiwa kukupata,Tafadhali sana madam,mm mwanafunzi wako nakutafta sana japo niseme asante kwako,nafsi inanilazmisha nihtaj kuonana naww ila nashindwa sabab sjui nianzie wapi,please ukisoma ujumbe huu jua mwanafunzi wako BUFFET anakutafta sana
Teh ...
 
Nakumbuka siku nilivyobiwa nguo za shule na kila kitu pale ferry na muuza mayai baada ya kumpa niogelee baharini

Nakumbuka enzi za kuvua samaki kwa mashati ya shule msimbazi

Nakumbuka tulivyoenda kuiba vitabu kwenye mv dolphin kisha tukakamatwa

Maisha ya utoto yamejaa vioja sana
 
Aisee umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka siku tuliyohangaika kutafuta URUSI. Yaani tulitokwa jasho maana sisi tulikuwa tunatafuta maandishi madogo kumbe yenyewe makubwaaa
Mnakariri kila anayeomba ni vimaandishi vilivyojificha.
 
Teh ...

Mi Beijing

Made in china tulkua tunasoma madeni china
Aisee umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka siku tuliyohangaika kutafuta URUSI. Yaani tulitokwa jasho maana sisi tulikuwa tunatafuta maandishi madogo kumbe yenyewe makubwaaa
 
Mimi ninacho kumbuka nikiwa shule ya msingi nipale nilipo mtongoza mwl wa chuo sito sahau ilo tukia
 
Back
Top Bottom