Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Nilikuwa mkorofi sana darasani. Siku moja nikafumwa nikabananishwa na walimu. Mbona nilitoka na dirisha.

Ila juzi juzi hapa mwaka huu nilitoa hela lile dirisha nililovunja lijengwe.

Achana na mimi kabisaaa.....!!!
 
Kuomba vitu mapumzikoooo, Nilikuwa natafuta rafiki ambaye mda wa kula ana nunua vitu vizurii
 
Tabia ya kupigana kesi kila wakati home sharti langu la shule vifungo vitatu au viwili mama kashona kachoka.
 
Nakumbuka ilikua j3 siku ya ukaguz /usafi.jpil nilichelewa kufua nguo sasa inafka siku ya j3 asubuh shat la shule alijakauka nikaona isiwe kesi nikakata kola ya shat kisha nikalipiga pasi vizuri nikavaa na sweta langu Ile kola nikaitoa kwa nje.mda tukiwa mstarini mwalim Kafika kwangu kwa nyuma akabinua kola yangu aone kama nimefua.kakuta kola ina ng'aa balaah akaanza kuni mwagia sifa kede kede.dadek kimbembe nikaambiwa nitoke mbele nivue sweta wanione nilivyo smart kilicho tokea Mungu anajua 🤣🤣🤣
 
Mm nilikuwa mwizi sana hasa wakati wa michezo ya umitashumta. Nilikuwa mtaalamu wa kudokoa vyakula vya wale kinamama Waliokuwa wanakuja kuuza. Sasa kuna fimbo ndefu walikuwa wanakaa nayo ili kulinda Mali zao, inaitwa 'nnlo'. Sasa wakiniona tu, utasikia chukua nnlo amekuja. Hata hivyo kwa utaalamu niliokuwa nao, nilikuwa nawasukumizia wanunuaji wengine waliosimama kwa wale kina mama then mm natoka na karai la ndizi kiulani!!! Hata hivyo nilishaenda kutubu, na nina imani nilishasamehewa hahaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ilikua j3 siku ya ukaguz /usafi.jpil nilichelewa kufua nguo sasa inafka siku ya j3 asubuh shat la shule alijakauka nikaona isiwe kesi nikakata kola ya shat kisha nikalipiga pasi vizuri nikavaa na sweta langu Ile kola nikaitoa kwa nje.mda tukiwa mstarini mwalim Kafika kwangu kwa nyuma akabinua kola yangu aone kama nimefua.kakuta kola ina ng'aa balaah akaanza kuni mwagia sifa kede kede.dadek kimbembe nikaambiwa nitoke mbele nivue sweta wanione nilivyo smart kilicho tokea Mungu anajua
Hahahahahaha dah jeiefu ni mwisho wa matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SI
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
KUWAHI KUVAA MPAKA NILIPOFIKA DARASA LA NNE, TENA SIKU YA MTIHANI WA TAIFA. NA NILIAZIMA KWA MANZI JIRANI YETU NILIYESOMA NAE CLASS MOJA
 
Daaah... nakumbuka nilikuwa nikinunua kachori nakimbia kwenda kujificha kwenye Korongo. ili wenzangu wasiniombe.. siku moja nilikimbilia kule kumbe sikujua kulikuwa na madondola ya linipiga sindano za uso , Aise niliumuka sasa kama maandazi yaliyowekwa Amira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikuwa tunapenda sana kuchezea maji na utelezi hasa mvua inponyesha tena bila viatu kama picha hii inavyoonyesha

kitt-713792.jpg
nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
umenikumbusha mbali saaana mkuu!YOU HAVE MY THANKS
Shule zetu nyingi tulizosoma zilikuwa hivi na akili zilikuwemo leo hii mazingira mazuri na facility kwenye shule nyingi hasa za mjini zipo ila mitoto bomu bomu sijui tatizo ninini hasa au ndio hivyo tena nchi imeharibika na haina mwenyewe kuanzia chini hadi kwa wenye nchi???
3583548_orig.jpg
Bila kusahau kuruka ukuta na kutokea dirishani hasa wakati wa kwenda kufagia viwanja na kunyeshea maua sie "wajanja" tulikuwa tunasepa

1262.jpg
Ppp
 
Nlikua naingia mchana, kwahiyo kumwagilia maua mbele ya darasa letu na kiranja alikua ana tick madumu 15 kila mtu ole wako usifikishe
 
Nakumbuka tulitangaziwa kwamba tujiandae atakuja mtangazaji wa redio Tanzania kuturekodi kipindi cha watoto yaani mashairi, hadithi na ngonjera. Nikachaguliwa.

Siku iliyofuata mwalimu akapunguza majina na mimi akaniondoa, nikagoma kwa hoja kwamba ninaweza.

Darasa zima likashangaa mimi kumkatalia mwalimu. Sasa akasema basi atanitoa kwenye hadithi na ataniingiza kwenye shairi. Lakini shule haitatunga shairi bali mimi nitunge shairi na nilisome mwenyewe redioni.

Nilikuwa brilliant kuliko wote darasani lakini mwalimu alinikomoa kunipa shairi unajua wakati ule mashairu walikuwa wanakaririr wasichana tu.

Darasa zima na mwalimu wakajua ntashindwa na akanipa siku mbili niwasilishe shairi kabla mtangazaji hajaja.

Yule mwalimu hakujua uwezo wangu wa kujua na ktunga mashairi. Ndani ya siku moja nikampelekea na toka siku hiyo wasichana wakaniogopa kwenye mashairi.
 
Shule yetu ilikuwa imepakana na masista wa kanisa katoliki wana mti wa mapera. Tulikuwa tunaiba kila siku wanatufukuza.
 
Back
Top Bottom