Rubi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,615
- 326
tehe tehe nakumbuka baba alikuwa ananipeleka bora ukifika kuna sehemu ya kupimia size ya mguu ndo unachagu kiatu kinachokutosha.umesahau cha cha cha,au zile raba za bora
tehe tehe nakumbuka baba alikuwa ananipeleka bora ukifika kuna sehemu ya kupimia size ya mguu ndo unachagu kiatu kinachokutosha.umesahau cha cha cha,au zile raba za bora
zingine ni
sikiri mimi maskini,
uvivu wangu nyumbani,
ukiwa huu njiani,
nakufa hapa kwa nini......
kofia nyekundu tarabushi inanipendeza mama..........
Nalalia kulia leo...................... Bibi tarabushi. Nakwambia hapo ndio darasa la tatu nafikiri.
asiyependa shule ni mjinga kabisa, barua ikija aitembeza kote....
karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja ili kumtaka hali............
halafu pia enzi hizo watu wa mazingaombwe wanakuja kutuletea mazingaombwe yao mara unatolewa shati jipya la shule, mara hela do!
azimio, azimio, azimio la arusha, lilitangazwa tano mbili sitini na saba azimio la arusha.
kaka yangu sikiliza
nataka kukuambia,
azimio la arusha,
lilizaliwa arusha.............
halafu mambo ya kucheza rede, uki, mdako, kujipikilisha, kiboleni, hahahaaaa we acha tu...
Bila shaka wewe ndiye huyo aliyeshikilia nyeti.Tulikuwa tunapenda sana kuchezea maji na utelezi hasa mvua inponyesha tena bila viatu kama picha hii inavyoonyesha
..........Nakumbuka nyimbo tu za darasa la kwanza, maana madarasa mengine sikusoma hapa bongo.
Mabata madogo madogo yanaogelea, yanaogelea ktk shamba nzuri la bustani.............
Hesabu mama ohhh hesabu, hesabu ninakupenda ahhhh hakika.....................
...........Vile vile nakumbuka kababu, ice cream, sambusa na uji wa mchele...........I wish enzi hizo zirudi.
nilikuwa mvivu sana kuamuka asubuhi mama akiniamsha nilikuwa namdanganya leo tumeambiwa twende mchana, sikumoja nikakosea step nikamwambia shule imefungwa eebwanaa.. alinibeba kimsobesobe hadi shuleni nikakuta wenzangu wako mstarini mwl mkuu alikuwepo nililambwa mboko kwanza mama akaja mwl wa darasa akaja mwl wa zamu mwisho mkuu mwenyewe wiki nzima matak o yakawa yamevimba sikurudia tena.
wandugu,
thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.
Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma issale primary school kule wilayani mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za mwenge au kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;
" chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa sifa tanzania..."
ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya baba wa taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na raisi wa tanzania.
Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa jkt basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;
" mchaka mchaka chinja... Aliselema....na mbuga za wanyama tanzaniaaaah ya kwanza ni serengetiii ngorongoroooh manyaraaa na mikumiii oooh tanzania hoooye....
ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???