Chief Kumbyambya
JF-Expert Member
- Jun 16, 2022
- 490
- 1,460
Nawasalimu wote kwa jina la upendo wa dhati.
Ebwana mimi kuna kitu nimekinot kwangu na kwa muda mrefu nikajua hali itakaa sawa tu mbeleni ila sasa naona hebu niwashirikishe na wadau humu ili kama kuna mtaalam yeyote anaweza akanieleza hali hii husababishwa na nini……..!!!!!!
Ni hivi….. nikiwa kwenye mazungumzo yale yasiyo rasmi mfano vijiweni ama kwenye umati wowote wenye mazungumzo ambayo mtu yeyote anaweza akaongea vyovyote vile huko nipo vizuri sana.
Mfano ubishani unapozuka katika vyombo vya usafiri iwe basi ama kosta mimi ni muanzisha mada mzuri sana na pia hata mada nikiikuta wanajadili sehemu barabarani na kuna watu wengi nikisikia tu wanachojadili lazima niingilie kati tena kwa hoja nzito na ubishani mkali sana kiasi kwamba mpaka niliowakuta mada ikiisha lazima waniambia “aisee bora umetusaidia bwana maana walitaka kutudanganya hawa”.
Na hao watu nakuwa wala siwajui na hawanijui ila nimevamia tu mada na kufanikiwa kuwateka wasikilizaji (yaani nakuwa na makomfidensi ya kufa mtu).
Shida sasa inakuja kwenye yale mazungumzo ambayo yanahitaji mpangilio wa kuongea eidha unakuta ni vikao vya kiofisini au kwenye vikao flani muhimu….. yaani labda inapangwa kabisa ataongea flani… akitoka flani atachangia flani kisha akitoka huyo flani bwana chief kumbyambya itakuwa zamu yako….
Unakuta wametangulia kuongea waliotangulia na tumewasikiliza vizuri kisha kile kile kitendo tu cha kijua sasa ni zamu yangu ya kuongea ndiyo inafuata.. hapo hapo ndiyo naanza kuvibrate sasa…
Yaaani naongea kwa hofu… pumzi inakuwa kama inabana hivyo kupelekea sauti itoke kama ya kutetemeka hivi…. Kwa mtu mwelewa akiwepo eneo hilo anajua tu huyu kijana ana hofu kubwa sana na hajazoea kuongea mbele za watu ndiyo maana anapata shida hivi wakati sio kweli….. mimi nikiwa uraiani huko naweza kuongea na watu hata mia tatu siwajui na hawanijui tena kwa confidence ya hali ya juu mno mpaka najishangaa inakuwaje hapa!!!?
Sasa wadau swali langu…..……
Ni kwanini nakuwa vizuri katika mazungumzo yale yasiyo rasmi…. yaani mtu flani anaongea alafu akishamaliza tu mimi nikidakia bila kuchaguliwa nakuwa na comfidence moja matata sana mpaka utasema hakika huyu kijana ni toleo jipya la Malcolm X.
Hata watu wawe mia tatu nitashusha nondo matata sana na wote wanatulia kusikiliza na wanakubali.
Ila yale mazungumzo ya mpangilio wa uongeaji kwa kufuata zamu kama niliyoyaeleza kule juu nakuwa vibaya utafikiri sio mimi.
Hapo kitaalamu kuna nini. Ama natakiwa kurekebisha nini?
Naamini humu kuna wajuvi wa mambo.