Wakulima wa tumbaku wajipatia mabilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima wa tumbaku wajipatia mabilioni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Oct 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Wakulima wa tumbaku wajipatia mabilioni
  Na Lucas Macha  1st October 2009


  [​IMG]
  Shamba la tumbaku.  Wakulima mkoani hapa wamejipatia Sh bilioni 149 kwa kuuza tumbaku katika msimu wa mwaka huu.
  Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa Bodi ya Tumbaku nchini, Vitta Kawawa wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Msimba na Ibili kilichopo Wilaya ya Uyui.
  Kawawa, alisema kiwango hicho kimeongezeka maradufu kutoka Sh bilioni 60 ambazo wakulima hao walijipatia mwaka jana baada ya kuuza tumbaku.
  Kawawa ambaye pia ni Mbunge wa Namtumbo mkoani Ruvuma, alisema wastani wa bei ya kilo moja ya tumbaku kwa sasa ni mzuri kwa kuwa inauzwa kwa Sh 2,500 kwa kilo.
  Alisema wakulima wa tumbaku nchini wanaufaika na zao hilo kwani z ni imara na halijateteleka hasa katika kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi unaozikumba nchi mbalimbali duniani.
  Mwenyekiti huyo yuko mkoani hapa kwa ziara ya kukagua maendeleo ya zao hilo na kuwahamasisha wakulima kuboresha kilimo hicho ili kuongeza kipato.  CHANZO: NIPASHE http://www.ippmedia.com/
   
Loading...