Wakulima wa miwa wakopeshwa mil 550/-

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
WAKULIMA 17 wa mashamba ya miwa wilayani Kilosa, wamenufaika na urasimishaji mashamba kwa kutumia hatimiliki za kimila kukopa Sh milioni 550 kutoka Benki ya Maendeleo ya Wakulima; imeelezwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amesema hayo mjini hapa alipozungumzia manufaa ya urasimishaji ardhi na mashamba wilayani hapa unaoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita).

Alisema kupitia Mkurabita na wadau wengine, wilaya ya Kilosa inanufaika na urasimishaji mashamba na ardhi kwa kuwa umekuwa chachu ya maendeleo na kilimo chenye tija kinachoongeza pato la wananchi na halmashauri kwa jumla.

“Kwa kipindi cha miaka miwili wakulima 17 wa miwa huko Luhembe wametumia urasimishaji wa ekari zao 6,000 za miwa kupata fursa ya kukopa na hivyo wameongeza uzalishaji wa mavuno,” alisema na kuongeza:

“Kama mtu alikuwa anavuna tani 15 hadi 20, sasa anavuna tani 35 hadi 40 na haya ni matokeo ya mitaji yao kukua kutokana na fursa ya ukopaji waliyoipata baada ya Mkurabita kuratibu urasimishaji wa mashamba yao na kwa msingi huo, pato lao limekua na hata pato la halmashauri yetu linaongezeka.”amesema.

Mkuu wa wilaya huyo wa Kilosa alitoa mwito kwa taasisi za fedha zikiwamo benki wilayani humo kuendelea kuzitambua hati za hatimiliki za kimila na kuzitumia kama dhamana ya mikopo kwa kuwa ni hati halali za kisheria zinazotolewa na serikali.
 
Hii benk nilisha wai kuiandika vibaya mno na niliandika ukweli hawajielew hiv wanadhani hayo mashamba waliyo kopesha ni ya kweli? Hayo mashamba ni dhamana kwa benki nyingime na hiyo miwa inaenda kulipa kwingine mm nipo hapa mtaona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii benk nilisha wai kuiandika vibaya mno na niliandika ukweli hawajielew hiv wanadhani hayo mashamba waliyo kopesha ni ya kweli? Hayo mashamba ni dhamana kwa benki nyingime na hiyo miwa inaenda kulipa kwingine mm nipo hapa mtaona

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii benk inatatizo gan lakini mbna malalamiko mengi?
 
Back
Top Bottom