Wakulima wa Machungwa aina ya Valencia walivyopata pesa msimu huu

wegman

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,190
2,000
Ndugu tusaidie sisi wengine wazee wa kutafuta fursa,hiyo mbegu ya Valencia ina tofauti gani na zingine?Je kwa mkoa wa Tanga inakubali sana katika wilaya zipi au maeneo yapi?Vipi upatikanaji wa miche yake kama nataka kulima at large scale?
Swali zuri ila limekosa majibu Mkulima na Mfugaji tusaidie hapa tujue what is so special kwenye mbegu ya Valencia kulinganisha na mbegu nyingine.
 
MLUGURU

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
2,276
2,000
Ndugu tusaidie sisi wengine wazee wa kutafuta fursa,hiyo mbegu ya Valencia ina tofauti gani na zingine?Je kwa mkoa wa Tanga inakubali sana katika wilaya zipi au maeneo yapi?Vipi upatikanaji wa miche yake kama nataka kulima at large scale?
Tofauti ya mbegu ya valencia na nyingine ni kama zifuatazo : -

- huchelewa kukomaa shambani hii inampa mkulima nafasi ya kupanga bei.

- baada ya kuiva mtini,linaweza kukaa kwa muda mrefu bila kuchumwa na lisidondoke chini kama aina nyingine ya machungwa yakichelewa kuchumwa na kupelekwa sokoni yanadondoka na kuoza.
mfano ni hapo kwenye picha niliyotuma umeona yameiva mpaka yamebadilika rangi lakini bado ubora wake ni ule ule.

- kipindi cha usafirishaji wa valencia inavumilia shuruba za njiani kwani ina ganda gumu hivyo yanaweza safiri kwa umbali mrefu.

- pia ina maji mengi,tamu na sukari ya kutosha.
 
Aqua

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
1,632

Nashukuru ndugu kwa hiyo hapo naona hilo chungwa linauwezo wa kukaa muda mrefu baada ya kuchumwa kabla halijaharibika.Vipi upatikanaji wa miche yake na gharama zake,lakini pia nilitaka kujua kwa wilaya za Tanga inakubali maeneo yote au kuna maeneo inafanya vizuri zaidi?Natanguliza shukurani
 
Oct 4, 2021
7
45

Ili uwe na uhakika wa kupata mchungwa wa valencia ni bora ununue mche wa limao halafu unaupanda shambani baada ya Hapo unafanya grafting mwenyewe ila ukinunua mche wa mchungwa moja kwa moja wafanya Biashara wengi wamekua sio waaminifu, anaweza kukuuzia aina nyingine ya mchungwa akakwambia ni valencia, unakuja kugundua baada ya mchungwa kuanza kuzaa, inakua umeshapoteza, garama, nguvu na Muda wako
 
Nashukuru ndugu ni kweli mlimau unavumilia magonjwa na hivyo hushauriwa kuutumia kama "rootstock" kwa miti inayifanyiwa grafting,sasa hujanieleza kwa Tanga hiyo chungwa inafanya vizuri zaidi wilaya ipi?Handeni,Pangani,Lushoto,Muheza?
 
Muheza mkuu.
 
Inafanya vizuri zaidi muheza ila hata Handeni, korogwe na mkinga inakubali ila sio sana kwani yanawahi kuiva hivyo hayakai Muda mrefu kwenye mti
 
penadu

JF-Expert Member
Dec 24, 2016
714
1,000
Wazigua tatizo ushirikina ,hata wauze chungwa moja 500 ataishia kuoa wanawake,hawezi jenga nyumba ya maana
Kwa taarifa yako wakulima wa machungwa mheza walio sio wazigua, kule wenyeji hasa ni wabondei, na wakulima wengi ni wageni
 
penadu

JF-Expert Member
Dec 24, 2016
714
1,000
Ili uwe na uhakika wa kupata mchungwa wa valencia ni bora ununue mche wa limao halafu unaupanda shambani baada ya Hapo unafanya grafting mwenyewe ila ukinunua mche wa mchungwa moja kwa moja wafanya Biashara wengi wamekua sio waaminifu, anaweza kukuuzia aina nyingine ya mchungwa akakwambia ni valencia, unakuja kugundua baada ya mchungwa kuanza kuzaa, inakua umeshapoteza, garama, nguvu na Muda wako
Kama uko Tanga nenda pale Tari mlingano sasa hivi licha ya kuuza miche ya mkonge wana miche ya michungwa, pale uhakika wa kuto chakachuliwa, bei zao pia rafiki
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom