Wakulima wa Afrika wafaidika na upendo wa wachina kwa tofu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Na Tom Wanjala

1636417653399.png


Tofu inayotengenezwa kutokana na maharagwe ya soya inapendwa sana na wachina, ni chakula kinachopatikana kwa rahisi na chenye faida nyingi za kiafya mwilini, na upendo huo wa wachina unaifanya China kuingiza kwa wingi maharagwe ya soya kutoka mataifa ya duniani.

Jua la utosini linachoma kama tanuri katika eneo la Migori nchini Kenya. Mary Luvanda amemaliza shughuli za kupalilia maharagwe ya Soya shambani kwake na yuko guu mosi guu pili hadi nyumbani kwake. Chini ya siku mia moja zijazo, mchumia juani huyu atakuwa anahesabu faida yake kivulini. Anaiambia CRI Kiswahili kwamba maisha yake yamebadilika sana tangu alipopata fursa ya kuuza zao lake nchini China.

“Awali tulikuwa tunapanda kwa lengo kuu la kuuzia wenye maduka ya kuuza vyakula vya ng’ombe. Faida haikuwa kubwa mno kwa sababu kwa kila kilo ya maharagwe ya soya, nilikuwa nauza kwa shilingi 30. Ila sasa kila kilo ni zaidi ya shilingi 40,’’ anasema bi Luvanda.

Mwaka 2018, wakulima wa zao la Soya eneo la Migori walipata mwamko mpya baada ya wataalam wa kilimo wa kaunti kuwaeleza kuhusu namna zao hili linapendwa sana na Wachina katika utayarishaji wa chakula aina ya tofu.

‘Kwa mara ya kwanza, nilipanda kilo sita pekee ya maharagwe ya soya. Nilipovuna, niliyauza kwa mawakala wa kununua soya, na ambao baadaye wanauza nchini China. Nilipata faida ya shilingi alfu nane. Pesa hizi zilinisaidia sana katika kulipia watoto wangu karo ya shule,’’ anaeleza Luvanda, ambaye ni mama ya watoto watatu.

‘Kwa mara ya kwanza, nilipanda kilo sita pekee ya maharagwe ya soya. Nilipovuna, niliyauza kwa mawakala wa kununua soya, na ambao baadaye wanauza nchini China. Nilipata faida ya shilingi alfu nane. Pesa hizi zilinisaidia sana katika kulipia watoto wangu karo ya shule,’’ anaeleza Luvanda, ambaye ni mama ya watoto watatu.

1636417695858.png


Mojawapo ya mikakati ya China kuinua maisha ya raia wa Afrika, ni kununua mazao yao ya shambani. Kutoka kwa parachichi, kahawa, maua, majani chai na sasa maharagwe ya soya, China imeonesha jinsi gani imejitolea kusaidia sekta ya kilimo cha Afrika, kwa kutoa soko kubwa kwa mazao yao ya shambani.

Bi Luvanda anadokeza kuwa hang’atuki kwenye kilimo hiki ambacho kimemfaa kwa hali na mali. Anavuna zao hili mara tatu kwa mwaka, kinyume na zao la mahindi ambalo alikuwa amezoea kupanda na kuvuna mara moja kwa mwaka.

Uwepo wa Wachina Nairobi na miji mingine, pia imeongeza sana ari ya wakulima wa maharagwe ya soya kwa sababu baadhi yao wanauza moja kwa moja kwa Wachina wenyewe.

Njangi Mutwiri, mtaalam wa kilimo cha soya, anasema kuwa Wakenya wameanza kuacha utamaduni wa kupanda zao moja kila mwaka, na sasa wamekumbatia mazao mengine ambayo wanaweza kuyauza nchini China.
 
Hapo mnaona kuna win win situation? Au Mchina ndio anajipatia zigo kwa being karibu na bure?

Pamoja na kwamba mchina ananufaika sana kwa sababu anabeba malighafi lakini soko la soya lilikua baya miaka yote lakini kwa sasa limechangamka na sio kenya tu Zambia na Tanzania pia ambao ni wazalishaji wa soya soko lake ni uhakika sana
 
Back
Top Bottom