Wakulima tushauriane kampuni zinazouza mbegu bora

Hahahahahaaa..hili la mbegu aisee ni Tatizo..mi niliingizwa mkenge na consultation ya the so called afisa kilimo akaniambia ninunue mbegu HYBRID ya Kenya... yaani mahindi yalianza kuchanua yakiwa hayajafika hata urefu wa magotini....

Kuna kila haja hawa wataalam waji update maana wanachangia kutuangusha......

Wajuzi mje jamani tunawahitaji mnooooi
Hilo ni tatizo kubwa sana....na limekosa msaada...
 
nadhani balton wako good, ila kufanya kazi na wabongo walio wengi ni changamoto sana bora uwe na pesa ya kutosha upate mbegu zisizo na mfungamano na wabongo
Watz huwa hawako kibiashara kabisa...tunabaguana...mtu unaweza ukamfata ofisini kwake akakufanya ujute kumfuata....hao niliwatafuta waniuzie Kit (box maalum la drip system) chaajabu Arusha waliniambia laki 4 na 20 huku Dar wakaniambia laki 6 na 70 na hiyo ni kampuni moja ambayo ina matawi Arusha na Dar...kwanini utofauti uwe kwa kiasi kikubwa namna hiyo¿ wabongo pasua kichwa sana
 
mkuu Tatiana mie nilikua na horticulture hasa kwenye matikikiti zilifanya vizuri sana ukanda wa pwani ila kwenye mahindi kwa ushauri wangu nenda tanganyika farmers association maana hapo enzi nipo home tulikua tunanunua na hamna ujanja ujanja
Ulinunua mbegu aina gani...¿ imezalishwa na kampuni gani? Ni aina zipi ya mbegu nyingine za matikitiki ni nzuri...tusaidiane ndugu
 
Asantee sana.....msimu ujao nitafanya mabadiliko ya mbegu...

mimi nipo kwenye uzalishaji wa mahindi, karanga,chorizo na vitunguu na ufugaji kuku ndio nimeanza

But nilikuwa nataka pia nilime bamia kidogo
Mkuu mahindi unalimia wapi?
 
cae6aee950c6ef9a69c54977a5dd977b.jpg
7e3d1d818f4a2ad7eea678f53eb3aa87.jpg
d5540bb75eae2f0de6719fc574dc86e7.jpg

Wadau msaada tafadhali bamia langu linakumbwa nahiyo kitu sijui shida nini nifanyeje niweze kukabili hiyo ndio kwanza zinaanza kuza
 
M biashara ya kununua mbegu maduka ya pembejeo nimeachana nayo.Maana ukijirengesha wana maneno mazuri kweli,hivyo mbegu za Katanga nanua kwa wakulima kwa bei ya chini then wakati ukifika nazigrade napanda.Hivyo hivyo kwa mahindi,m zimenishinda bei zao kubwa
 
Africasia wapo vizuri, cha kuzingatia ni zile specification kama purity,germination na ziwe zimeandikwa kwa maandishi madogo madogo yakiwa makubwa sana hiyo inaweza kuwa fake..!
 
Natafuta mbegu za mahindi za asili nitaipata wapi?
Mbegu za asili...nenda kijijini kwenu...ukipewa zawadi ya mahindi kapande....au omba kijijini huko bado wanazo mbegu za zamani ambazo ndizo mbegu za asili.
 
Back
Top Bottom