Tetesi: Wakulima Tandahimba kuandamana kupongeza kurudishiwa korosho zao

Wasalaam, baada ya takribani miezi3 tangu serikali ikusanye korosho za wakulima kwa nia ya kuzinunua hatimae serikali hiyo imewarudishia wakulima korosho hizo kwa madai hazina ubora. Kutokana na kitendo hicho kunatetesi kwamba wakulima hao wamepanga kuandamana kuunga mkono juhudi, pia kushukuru kwa kurudishiwa korosho ambazo hazina ubora.

Ikumbukwe wakati korosho hizi zinakusanywa wakulima hawa waliandamana kuunga mkono juhudi za rais kuwaondolea umasikini kwa kununua korosho hizo kwa bei nzuri , hivyo wanaomba na safari hii waruhusiwe kuandamana km ilivyokua awali kushukuru kwa mzigo kurudi maana wengi wao walijua wameshadhulumiwa mzigo baada ya kusubiri malipo kwa takribani miezi3.
Rubbish ever !
 
Kwanini hawakuandamana waliponyang`anywa?
Waliandamana kuunga mkono juhudi za Serkali kununua korosho zote kwa being nzuri. Sasa wanataka kuandamana kwa kurudishiwa korosho zao salama maana zingeweza kutupwa baharini. Waliokwisha lipwa wanatakiwa warudishe pesa za walipa kodi. Awamu hii inajali sana walipa kodi.
 
... kama hii habari ni ya kweli then automatically itakuwa imekuwa proved, beyond reasonable doubts, kwamba eneo/ukanda huu wa dunia ndilo eneo lenye binadamu wajinga kuliko eneo lingine lolote duniani.

Scientific researches have to be conducted to prove the reasons for that behavior; is it a genetic issue? harmful materials (in the land? air? waters? grains? foods?); or what?
my ribs
 
Wasalaam, baada ya takribani miezi3 tangu serikali ikusanye korosho za wakulima kwa nia ya kuzinunua hatimae serikali hiyo imewarudishia wakulima korosho hizo kwa madai hazina ubora. Kutokana na kitendo hicho kunatetesi kwamba wakulima hao wamepanga kuandamana kuunga mkono juhudi, pia kushukuru kwa kurudishiwa korosho ambazo hazina ubora.

Ikumbukwe wakati korosho hizi zinakusanywa wakulima hawa waliandamana kuunga mkono juhudi za rais kuwaondolea umasikini kwa kununua korosho hizo kwa bei nzuri , hivyo wanaomba na safari hii waruhusiwe kuandamana km ilivyokua awali kushukuru kwa mzigo kurudi maana wengi wao walijua wameshadhulumiwa mzigo baada ya kusubiri malipo kwa takribani miezi3.
uko na uhakika mkuu, kweli hao watu wanasitahili kupimwa akili
 
... kama hii habari ni ya kweli then automatically itakuwa imekuwa proved, beyond reasonable doubts, kwamba eneo/ukanda huu wa dunia ndilo eneo lenye binadamu wajinga kuliko eneo lingine lolote duniani.

Scientific researches have to be conducted to prove the reasons for that behavior; is it a genetic issue? harmful materials (in the land? air? waters? grains? foods?); or what?
Masalia ya mijusi wakubwa!
 
Hawa sio wajinga, wanataka kuandamana kwa dhihaka kumvua mtu nguo. Aibu aone yeye.
 
Ingelikuwa nchi za mabeberu ndio hili limetokea sasa hivi ungesikia mahakamani imefunguliwa kesi ya mkataba

Wakulima wa korosho v Serikari ya mabeberu (2019)

Mkataba sio lazima kuandikishiana unapotoa kauli hadharani watu wakaitikia wito wa kauli yako na mkabadilishana vitu vyenye thamani huo tayari mkataba unaotambulika kisheria.

Ikitokea baadae tena uwezi kuwalipa kama ulivyoahidi adharani that is just 'material breach' mahakama itakulazimisha ulipe tu; ndio kilichotakiwa kitokee kusudi siku nyingine usikurupuke na kujiropokea. But then this is Tanzania wanasheria sio wajasiriamali wenzetu sasa hivi mtu angeichukua hii kesi bila ya malipo hila 5% yake wakishinda .Sasa ukipata 5% ya wakulima wa korosho si unaweza retire kabisa na kazi yenyewe kwa amani.
Sio kesi tu kuunguruma mahakamani, bali watu wangejiuzulu kwa kushindwa kutekeleza na kutimiza majukum yao ipasavyo
 
Back
Top Bottom