Wakulima Rungwe wagoma kuuza chai kampuni ya Katumba ............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima Rungwe wagoma kuuza chai kampuni ya Katumba ............

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 3, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Wagoma kuuza chai kampuni ya Katumba Thursday, 02 December 2010 20:58

  Amanyisye Ambindwile,
  Tukuyu

  WAKULIMA 2,025 wa zao la chai wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameamua kuuza chai kwenye kampuni ya Mohamedi Enterprises limited (METL) kwa kuwa kampuni hiyo, inawalipa vizuri zaidi kuliko kiwanda chao cha Katumba.

  Wakizungumza na kwa nyakati tofauti hivi karibuni wakulima hao, walisema wameamua kupeleka chai yao katika kampuni ya METL kwa kuwa inanunua kilo moja ya chai Sh 170 wakati katika kiwanda cha Katumba kinanunua Sh 160 kwa kilo.


  Mzee Betweli Mwakalasya mkazi wa Kijiji cha Mumbuli Kata ya Mpuguso, wilayani hapa, alisema tangu waanze kuuza zao hilo Oktoba, mwaka huu amepata faida kwa muda mfupi kama vile kukarabati nyumba yake tofauti na awali.

  Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wakulima wa chai Rungwe (RUTECO), Timothy Kaswaga alisema wakulima wanafanya hivyo kwa maslahi yao na kwamba kampuni ya METL imewaahidi kuwaongeza bei ya zao hilo endapo watazalisha chai bora.

  Alisema kampuni hiyo haina makato yoyote kna kwamba katika kampuni ya Katumba wanakatwa zaidi ya Sh 30 kwa kilo jambo ambalo wamedai ni dhuluma kwa wakulima.

  Mkulima Stephen Mwakifuna wa Kijiji cha Bujela, wilayani Rungwe aliomba serikali iwasaidie wakulima na kuwapa uhuru wa kuuza mazao wanayozalisha katika masoko mbalimbali.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Biashara huria,Katumba tea factory(Wakulima) wadopokaa chonjo watajuta kushirikiana na makampuni ya kifisadi kama Caspian au Junejo
   
Loading...