Wakulima 1,000 waandamana Kibaigwa na kuziba barabara ya Dar-Dom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima 1,000 waandamana Kibaigwa na kuziba barabara ya Dar-Dom

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 1, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  wakulima wapatao 1000 na matrekta yao zaidi ya 500 wanaandamana hivi sasa na kuziba barabara ya Dom-Dar maeneo ya Kibaigwa kupinga kuondolewa kutoka ardhi yao na kupewa mwekezaji.

  Source: radio One Sterio 30 mins ago.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami nimesikia habari hiyo nikiwa ndani ya daladala na kwamba polisi wako hapo kujaribu kuwabembeleza ili waondoke wafungue barabara. swali nililipata mara moja: Jee wakulima hao walikuwa na kibali cha polisi kufanya maandamano?

  Hakika walikuwa hawana amas sivyo polisi wangewyalinda maandamano badala ya kuamuru waandamanaji waondoke.

  Ingekuwa ni CDM ndiyo wamefanya hivyo, saa hizi viongozi wameshakamatwa na kutiwa pingu na kupelekwa selo!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Inasemekana hawa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM leo inakuwaje wanaingia barabarani kupingana na Serikali ya Chama chao na sera za kuuza Nchi ? Nilidhani ni Chadema pekee wanao andamana ?
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Mkuu wache watie akili maana wakiambiwa hawasikii !
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  si wangeandamana kipindi cha bunge wakazibe mageti ya bungeni hakuna mbunge kuingia mana hawawasemei wakiingia huko
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Walioko karibu na tukio watujuze kinachoendelea jamani.
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Utasikia ni CHADEMA haoo!!!!!!!
   
 8. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kila siku afadhali ya jana! Kwanini wasiwekeze kwenye mipori kibao, wanataka mashamba yaliyo tayari.
   
 9. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  acha watie akili. walijua ccm ndugu yao. hadi kufika 2015 watakuwa wametia akili. acha waendelee kujifunza kwa vitendo sababu kwa maneno hawasikii. over
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi, mbona inadaiwa kuwa Tanzania tuna ardhi bwerere? Kuna lazima gani ya kuondoa watu kwenye maskani yao ili mwekezaji apewe?
  Kwa nini huyo mwekezaji asipewe pori huko mbali alikuze? Nini maana ya uwekezaji?
   
 11. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Kuanzia Panda mbili(eneo maarufu kwa ajali), Kibaigwa, Narco(kongwa) chalinze(Kongwa),Mkoka, Zoisa hadi huku dosi dosi watu washavurugwa sana na huu uwekezaji feki.

  Kama mnakumbuka vizuri miaka michache iliyopita PM mstaafu Sumaye alikuwa na kashfa ya kumiliki Ekari mia tano, inawezekana ni ishu hii au kuna Mkoloni mwingine Mweusi kawaingiza mkenge.

  Ni mchanganyiko mzuri wa watu wabishi Warangi pia kidogo wamasai na Wagogo pia kidogo.

  Huo ni muziki, wananchi kuanza kuandama wenyewe
  ya kutorishwa na walioko madarakani.

  CCM Marufuku kanda ya ziwa,2005 Msanii alituahidi kiwanda cha Saruji Shinyanga, hadi leo hakuna lolote na Cement ni 20,000/= MZA, Matokeo yake 2010 tumeamua kuwapiga chini kwa kishindo, 2015 tunachoma kichaka chote kanda ya ziwa'

  "Aliye na masikio ya kusikia na asikie."
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hayo maandamano yalikuwa na kibali cha akina Mwema na Chagonja? kama hayakuwa na kibali kwa nini polisi hawakuwakamata viongozi wao na kuwasweka ndani kama vile wafanyavyo kwa akina magwanda?

  Polisi wetu hovyo kabisa -- wanaendeshwa na magamba kwa kuvutwa pua zao! Pambaff kabisa!!!!
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Land grab in the auspices of the soko huria...mtajuta mwaka huu watanzania....Ndio Kilimo Kwanza hiyo inatakelezwa...na bado SAGCOT haijaanza mtahama wote...walllahi tena
   
 14. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kuandamana bila kushurutishwa huu ndio ukombozi, sio hawa wanaharakati uchwara wanaotangaza kesho maandamano halafu polisi wakiwatishia al shabab wanaufyata. AMAUTI
   
 15. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Walale Hapo Hapo Mpaka waaoneshwe(sio kuambiwa) hatima yao.. Serikali ina mkono mrefu na inaweza kuamua. Andamaneni mpaka waamue

  Na si wana matrekta? Walime hiyo lami kabisa tukose wote.

  Hao ni mashujaa sio sisi wakungoja wanaharakati waoga watangaze maandamano au msiba
   
 16. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Hivi ni kwanini serikali yetu katika swala la wawekezaji mara nyingi utasikia wananchi ndio wanahamishwa katika makazi yao walioishi katika kuzaliwa kwao. Hivi kwanini serikali wasiwape wawekezaji pori wakaliendeleza ili wananchi ndio wawafuate huko. Serikali hii kwakweli si ya wananchi hii kitu kidogo ndio inayotuponza na bila katiba mpya kweli watanzania watateseka sana. Wawekezaji wapewe mapori kama ni mashamba waanze upya sio kuwahamisha wananchi. kwani nao walipoanza zilikuwa pori. Nionavyo wawekezaji hawaji kutunufaisha watanzania hapana wanakuja kuchuma na kuwanufaisha baadhi ya viongozi serikali ambao bila rushwa maisha yao hayaendi. Ila nasema yana mwisho hata kama sio leo lakini kesho wataumbuka, ila nawaonea huruma familia zao kwani hawatakuwa na amani.
   
 17. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanaandamania nini huko? mashamba waliyonyang'anywa si yao ni mapori ya akiba huko Kiteto. Wamekuwa wavamizi wa hifadhi kwa kisingizio cha kilimo kwanza kwa nini wasilime kwenye shamba la Narco Kongwa?.
   
 18. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Nitarudi ngoja nikapate [​IMG]
   
 19. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Imekuwa dhahiri kuwa kazi mojawapo kubwa ya polisi ni kuzima maandamano ya wananchi ambao hawaridhishwi na utendaji wa serikali. Kuna wakati polisi watashindwa kuzuia maandamano yakitokea sawia nchi nzima na ihali hii italeta madhara makubwa. Inatakiwa viongozi kuchukua tahadhari na kuanza kusikiliza malalamiko ya wananchi,

  Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, limezima maandamano ya wakulima wakubwa kutoka vijiji tisa vya wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, wameandamana wakiwa na matrekta takribani 200 kupinga kuondolewa katika mashamba yao ili kupisha hifadhi za mbuga za wanyama.

  Wanaotakiwa kupisha mbuga za wanyama ni wakulima wa mashamba makubwa kutoka vijiji vya Lendolai, Mlimahamba, Laitini, Mbigiri, Kutilemeinyi, Seseni, Laipela, Kimarai na Kisima.

  Tukio hilo lilitokea jana katika mji mdogo wa Kibaigwa, ambapo ilimlazimu Kamanda wa

  Polisi mkoani hapa, Stephen Zelothe, kutuma ujumbe kwa wakulima hao akiwataka kutoandamana na badala yake kuegesha matrekta yao pembeni mwa barabara ya kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.


  Lakini wakati wakiwasubiri viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwenda kuwasikiliza, baadhi ya wakulima hao waliingia barabarani na kuzuia magari yaliyokuwa yakiitumia barabara hiyo kwa muda, kabla ya kukubali kuondoka, baada ya Diwani wa Kata ya Kibaigwa, Richard Kapinye, kuwasihi waondoke njiani.


  "Nawaomba muondoke barabarani jamani, tumeahidiana kuwa tutawasubiri viongozi waje wazungumze nasi na kutoa majibu, sasa mkifanya hivi watashindwa kusaidia," alisema Kapinye kwa kutumia gari lililokuwa na kipaza sauti.


  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima hao, walisema walianza kulima katika mashamba hayo mwaka 1990, baada ya kupewa na wenyeji.


  Mmoja wa wakulima hao, Clement Petro, alisema ilipofika mwaka 2006, walikwenda watu kutoka serikalini na kuwaambia waondoke katika eneo hilo ili kupisha hifadhi ya mbuga.

  Alisema walipeleka kesi mahakamani ambapo mahakama iliwapa ushindi wa kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo.

  Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ilikata rufaa kupinga hukumu hiyo ambapo ilishinda na wakulima hao wakaamuliwa kuondoka katika eneo hilo.


  Mkulima mwingine, Omary Athuman, ambaye anamiliki matrekta wilayani humo, alisema kutokana halmashauri hiyo kuwafukuza katika eneo hilo, ana wasiwasi kama ataweza kurejesha mkopo wa matrekta aliyokopa kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT) tawi la Dodoma.


  "Tumeamua kuja huku kwa kuwa eneo la Kiteto halina amani tena kwa sababu wafugaji wamekuwa wakipitisha mifugo katika mashamba yetu wakidai kuwa tumeshaambiwa tuondoke katika eneo hilo," alisema.


  Alisema pia wameamua kufanya maandamano hayo na kueleza kilio chao kwa kuwa wamekuwa wakiuza mazao yao katika soko la Kibaigwa na pia mkopo wa matrekta wameupata kutoka Suma JKT mkoani hapa.


  "Mimi sijui hii dhana ya Kilimo Kwanza inatekelezwaje, mwanzoni tulidhani ni sera nzuri, lakini hivi sasa tunadhani haitekelezwi kivitendo na sijui haya matrekta tutalipa kwa fedha kutoka wapi," alisema na kuongeza kuwa yeye ana ekari 300 ambazo analima mahindi.

  Kwa upande wake, Alli Khalifan Said, alisema kuwa tayari wameandaa mashamba kwa ajili ya kilimo hivyo kuamriwa kuondoka katika eneo hilo itakuwa ni hasara kubwa kwake.

  "Wanataka tuondoke katika eneo hili, lakini hawatuambii twende wapi wala nani atalipia matrekta tuliyokopa na nyumba tulizojenga," alisema Said.

  Wakulima hao waliomba viongozi wa ngazi za juu, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, kuingilia kati suala hilo ili waweze kurudishiwa ardhi hiyo na kuendelea na uzalishaji.

  KAULI YA DED KONGWA


  Akizungumza na wakulima hao, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Athuman Akalama, alithibitisha kupokea barua ya kuomba kusaidiwa kutoka kwa wakulima hao.

  Hata hivyo, alisema wilaya za Kiteto na Kongwa ni wilaya mbili tofauti ambazo kila moja ina utaratibu wake wa matumizi bora ya ardhi.
  "Ni kama vijiji vinapokuwa na utaratibu wake wa matumizi bora ya ardhi. Mimi siwezi kufahamu ardhi hiyo walipanga kwa ajili ya matumizi yapi," alisema.
  Alisema nchi imekuwa ikiendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kuwashauri wakulima hao kwenda kukata rufaa mahakamani kudai haki zao kwa kuwa kuandamana na kupanga matrekta mahali hapo hakutawasaidia kutatua tatizo hilo.

  WAKULIMA WAZOMEA


  Baada ya kumaliza kuzungumza na kuwahoji kama wamekubaliana, kundi la wakulima lilizomea.

  Hata hivyo, wakulima hao walikubali kutoka katika eneo hilo huku Akalama aliyeongozana na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiondoka chini ya ulinzi wa polisi katika eneo hilo.

  SOKO LA KIBAIGWA LATIKISWA


  Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Soko la Kibaigwa, Kusekwa Dalali, alisema wamekuwa wakipokea mazao katika baadhi ya maeneo kutoka katika mikoa mitano ambayo ni Dodoma, Morogoro, Manyara, Iringa na Tanga.


  Alisema mazao ambayo wanayapokea katika soko hilo ni mahindi, alizeti, mbaazi, tetere, nyonyo na maharage na kwamba asilimia 60 ya mazao hayo yanatoka wilayani Kiteto, mkoani Manyara.


  "Kama wakulima wamezuiwa kulima katika maeneo hayo, sielewi itakuaje kwa sababu asilimia 60 ya mazao inatoka wilayani Kiteto," alisema na kuongeza kuwa katika msimu wa mavuno wamekuwa wakipokea tani 1,000 kwa siku.


  Alisema kutokana uamuzi huo wa serikali, soko hilo la kimataifa la mazao ya nafaka nchini, lililojengwa na Muungano wa Vikundi vya Wakulima nchini (Mviwata) na Ufaransa, huenda likashindwa kufanya kazi.


  POLISI, WAFANYABISHARA WAPAMBANA SINGIDA


  Wakati huo huo, mtarafaruku mkubwa umeibuka kati ya wafanyabiashara wa kuku na uongozi wa Manispaa ya Singida, hali iliyotishia uvunjifu wa amani na polisi kuingilia kati na kuwatia mbaroni watu kumi.


  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10:00 jioni, muda mfupi baada ya wajasiriamali hao kupakia kwenye lori matenga 27 yenye kuku, tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.


  Hata hivyo, baadaye lori hilo aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 125 BES, lilikamatwa na askari wa usalama barabarani waliokuwa na watumishi wa manispaa wakati likiwa nje ya mji katika barabara kuu ya Singida-Dodoma. Baada ya lori hilo kurudishwa mjini, na kushikiliwa katika ofisi za manispaa, kundi la wafanyabiashara wa kuku lilivamia eneo hilo na askari mmoja wa kikosi cha usalama barabarani alichaniwa sare yake ya shati.


  Kutokana na vurugu hizo kuwa kubwa, Jeshi la Polisi lilipeleka askari wengi katika ofisi za Manispaa ya Singida kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo na kuleta utulivu na kuwatia mbaroni wafanyabiashara kumi wa kuku.


  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Cordula Lyimo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ingawa hakuwa tayari kutaja jina la askari aliyechaniwa sare wala wanaoshikiliwa kwenye vurugu hizo, kwa maelezo kuwa hakuwa amepata taarifa rasmi.


  Hata hivyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Chama Cha Wauza Kuku Mjini Singida, Selemani Kuku, Mwenyekiti wa chama hicho, Karani Mahiki na Katibu wake, Msafiri Juma, ni miongoni mwa watu waliokuwa wanashikiliwa na jeshi hilo tangu juzi jioni. Kuku alifafanua kuwa pia wapo wafanyabiashara wengine sita ambao pia walikuwa wanashikiliwa, huku dereva wa lori hilo aliyetajwa kwa jina moja la Masawe, akiachiwa huru.


  Kwa muda mrefu, wafanyabiashara hao wamekuwa wakipinga kitendo cha manispaa kuongeza ada ya ushuru hadi kufikia Sh. 12,000 kwa tenga moja lenye uwezo wa kuchukua kuku 80, au kuku mmoja kulipiwa ushuru wa Sh. 300, ikilinganishwa na awali ambapo tenga moja lilipiwa Sh. 1,000.


  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Salome Singano, alisema kuwa ada hizo mpya zimetokana na maamuzi ya kikao cha Baraza la Madiwani cha Aprili, mwaka huu, kisha kusainiwa na Waziri Mkuu, kabla ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Oktoba7, 2011.


  Singano, alisema mchakato wa sheria hiyo inayojulikana kama 'Sheria ndogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ada na ushuru 2011', ilipelekwa kwanza kwa wananchi na kubandikwa katika mbao za matangazo kabla ya kurudishwa katika Baraza la Madiwani na baadaye kwa Waziri Mkuu.

  CHANZO: NIPASHE


   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mbegu hii imepandwa, imemea, na sasa inastawi!...Naam Mbegu ya maandamano!
   
Loading...