Mookiesbad98
JF-Expert Member
- Feb 1, 2015
- 2,300
- 2,716
Mh Makonda, Mkurugenzi wa Jiji na wengineo wote hali ya uzoaji takataka inatisha.
Tumesikia contract amepewa mtu mwingine lakini maajabu ya Mussa ni pale wakandarasi wa uzoaji takataka wanapokuwa hawana vifaa ikiwemo malori ya uhakika, hawazoi kwa wakati unaotakikana.
Kuna maeneo kama ya Upanga, Masaki huko mkandarasi wao anajitahidi sana kupita kwa wakati na kuzoa lakini maeneo mengi yaliyobaki kuna shida ya kuishi na uozo wa funza baada ya taka kukaa zaidi ya wiki majumbani mwa watu bila kuzolewa.
Unakuta ratiba labda ni Jumapili na Jumatano wazoaji na malori yao mabovu yanayoharibika kila mara hawapiti mpaka baada ya wiki 2.
Tumeona juzi Mjapani katoa msaada umesainiwa wa kujenga dampo la kisasa. Lakini hii isiwe sababu ya Procurement Unit ya jiji kutoa tenda kwa kampuni ambao hazina hata resources zingine hata ofisi hazina.
Na kwa ufuatiliaji, yupo mhasibu mmoja alikuwa katika kampuni ya takataka aliwahi kusema ni biashara ambayo inaleta pesa sana hapa Dar es salaam.
Ni wakati muafaka sasa mtekeleze vema ratiba za uzoaji taka mitaani, hili litapunguza magonjwa pia.
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app